Mimi nashangaa Mheshimiwa Yusuf Makamba kwa nini anajitetea?
hata Mwalimu J.K. Nyerere alikuwa ni mpinzani mkubwa sana wa RUSHWA, UBINAFSI, HONGO.
Rais Nyerere alitetea Taifa na wananchi wake, siyo familia yake.
Rais Nyerere alikuwa na mshahara mmoja, kama alipewa posho ilikuwa ni lazima, lakini hakutoa mikopo ya magari kwa mawaziri wala pensheni za wabunge. Nakumbuka badala ya kuwakopesha wabunge na mawaziri magari, alimwambia Mh. Rashidi kwamba " Na sisi tuanze kwenda kazini kwa kuendesha baiskeli".
Leo makamba anawatetea wazee wa CCM, ambao hawana jipya bali rushwa, kununua viwanja kila mahali, kunyang'anya wananchi mashamba yao, kuidhinisha kupiga kura kwa karatasi za bandia, kitu ambacho enzi za mwalimu hakikuwepo.
Mimi ningependa kumuuliza Makamba, kama kweli wazee wa CCM wana akili za kubuni mbinu mpya, yeye na Kikwete walipanda ndege wakaenda Mwanza siku ya kupiga kura. Kufika Mwanza wakakuta hapakaliki na mtu wao waliyekuwa wanamtegemea akaishia Bugando baada ya kuzirai. Kuona hivyo wakachoma wakaelekea Shinyanga na mkoba wao wa kura za bandia. Kufika Shinyanga wakakuta habari kwamba CHADEMA imeshinda, loooh! Hapo wakachanganyikiwa. Hawahawa wazee wa CCM wakamuamuru Mkurugenzi wa usimamizi wa kura atangaze kuwa ni CCM ndiyo imeshinda. Hata mtu wao wa CCM wa hapo Shinyanga akawaambia kuwa ukweli ni kwamba CHADEMA wameshinda, lakini Makamba na Kikwete wakamwambia huyo Mkurugenzi: " Sisi tunakwambia tangaza kuwa CCM imeshinda" Hizi ndizo busara za wazee wa CCM. Mkurugenzi akatangaza, kilichofatia Shinyanga watu wote tanzania nzima wanajua. Baada ya kutangazwa, huyo Mkurugenzi na familia yake akaihama Shinyanga bila kupenda, mpaka leo hatujui alikimbilia wapi.
Makamba naposema atajiudhuru mwakani ni kwa sababu ameisha kula vya kutosha na amejiwekea misingi mizuri ya pensheni, mashamba, viwanja na majumba ya kutosha kiasi kwamba watoto wake na wajukuu hawatakuwa na shida akisha staafu.
Hawa ndio wazee wa CCM wanaojidai eti wana mbinu mpya za kuliendeleza taifa Tanzania. Jamani hebu acheni uongo na muanze kuwa wakweli. Jaribuni kusikiliza na kuona habari zinazotokea Afrika ya kaskazini na nchi za mashariki ya kati.
Nasema " MWOGA UKIMKIMBIZA, ATAKIMBIA LAKINI AKICHOKA NA KUSIMAMA, BASI UJUE HAPO KUNA MAWILI - KUFA AU KUPONA". Na haya ndiyo yaliyotokea Misri na Tunisia. Kwa hiyo CCM msijidanganye. Kubalini kwamba mmezeeka na nchi sasa inahitaji nguvu mpya ya VIJANA, sio wazee wanaojifikiria wao tu na familia zao badala ya kuliendeleza taifa.