Makamanda Monduli wasambaratisha ngome ya Lowassa

THINKINGBEING

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2010
Posts
2,779
Reaction score
1,304
Kikosi kazi maalum kikiongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Monduli Ndgu Japhet Sironga, Katibu wa CHADEMA Wilaya Ndugu Thomas Kilongola na Mwenezi Chadema wilaya Ndugu Patrick Ngala OleMong'i wamefanikiwa kuwaondoa wananchi wa Moita Bwawani (Ndidai) katika makucha ya Mafisadi wa CCM na kuwaweka katika Taa yenye Nuru ya Ukombozi CHADEMA na kuwapatia kadi zaid ya wanachama wapya 760 waliofika katika hadhara hiyo wakiwamo waakina Mama,Wazee (Laibon) Na Vijana (Or murani+Nyangulo) Huku mabalozi zaidi ya 21 wakikabidhi kadi na vifaa MbaliMbali vya CCM.

Huku Mwenyekiti akinukuuu Kauli ya Mwalimu Nyerere Kuhusu Lowassa: NEC Dodoma 1995 na kuwaasa wanamoita wasirubunike tena na wasonge mbele kwa kasi ya kusimamisha wenyeviti wa vijiji na vitongoji
"Hapa hatuchagui mtu maarufu, tunachagua mtu safi na huyu si safi. Kama unapenda sura yake basi nenda kanywe naye chai. Wengine mnasema aaah ni tuhuma tu.

Samuel (Sitta)! Yusuf (Makamba)! Mnasimama hapa mnasema ni tuhuma tuhuma tu! Lakini mtakumbuka mke wa Kaisari alipotuhumiwa kwa ugoni Kaisari akaagiza uchunguzi ufanyike.

Uchunguzi ukafanyika na ikabainika kwamba sio kweli. Lakini Kaisari bado akamuacha, akasema mke wa Kaisari hapaswi hata kutuhumiwa.

Na sisi hapa Mgombea wetu hapaswi hata kutuhumiwa wakati wapo wengine safi ambao hawana tuhuma. Kama mkimteua huyo mimi sitapiga kampeni. Siko tayari kumsafisha mtu matope halafu ndio nimuombee kura. Hapana kabisa. Huyu mimi najua si msafi na nchi nzima inajua si msafi. Hafai kuwa mgombea wetu." - Mwl. Julius Nyerere, NEC Dodoma, Juni 1995
Ahsante sana Wanamoita kwa kuhitaji ukombozi huku mkigharamika kwa kuweka mafuta kwenye gari kufika mpaka hapo na kuwalipa waandish wenyewe kweli mmeamua mabadiliko Tu pamoja sana.
Pipoooooooooooooooooooooooooooooooz 1610826_746227942079433_7441839751039654007_n.jpg 150733_746231808745713_4754755539883366342_n.jpg
 
Umati unatisha kwa kweli! Lazima Lowassa atetemeke! Hehehehe
 
Siasa mchezo mbaya sana.Hivi bado kuna wanaoamini huyu Mh. ni mtuhumiwa wa ile kashfa ya Richmond?
.Ndugu zangu mpaka leo bado hatujapata maelezo ya upande wa pili juu ya kashfa ile na hiki ndicho kinazidi kumpa umaarufu Mh.Lowassa na hivyo kumuweka kwenye uadilifu na nidhamu ya hali juu kwa mkuu wake.
Na jambo hili wanaoliona ni wachache sana na kadri zinavyokwenda wengi ndivyo watakavyouona ukweli huo.
 
.Ndugu zangu mpaka leo bado hatujapata maelezo ya upande wa pili juu ya kashfa ili na hiki ndicho kinazidi kumpa umaarufu Mh.Lowassa na hivyo kumuweka kwenye uadilifu na nidhamu ya hali juu kwa mkuu wake.
Na jambo hili wanaoliona ni wachache sana na kadri zinavyokwenda wengi ndivyo watakavyouona ukweli huo.

Hivi hii nchi yenye watu karibu milioni 50 haina mtu msafi mpaka mhangaike kumsafisha huyu fisadi au ndio mmekufa kimahaba na ufisadi.
 
Mbona tuadanganyana mchana kweupe hao ndo watu 750? Hivi hawa ndg.wa cdm wakisema ukweli huwa wanapungukiwa na damu kwa bahati sitaki kuamini huo uwongo na sintakaa niamini kamwe ukweli ni hiyo picha jamani nisaidieni hao watu ni wangapi?
 
Mkuu wewe ni GT mzuri kabisa jibu hoja kwa hoja.Hivi ni lini na wapi ulisikia utetezi wa Mh.Lowassa juu ya Richmond?
Hukumu siku zote kwa kusikiliza pande zote mbili,sina hakika kama utakuwa umenielewa.Ila namaanisha ili mtu awe mtuhumiwa ni juu ya mamlaka kumfungulia jalada na kufanya chochote juu yake kwa mujibu wa sheria lakini mpaka leo hilo halipo.
Hivi uoni kwamba mtu huyu ni Innocent aliyewaokoa watu wake na gharama za kurudia uchaguzi..?
Mtu huyu angelikuwa ni fisadi angeliwachongea wenzake na yeye kuwa mkuu wa Nchi enzi ile lakini hakufanya hivyo sababu ya uadilifu wake.
Mnapoleta thread kama mtegemee kuwa na watu wenye mitazamo tofauti,hivyo hoja za matusi,kejeli na dhihaka hazifai.
 
Siasa mchezo mbaya sana.Hivi bado kuna wanaoamini huyu Mh. ni mtuhumiwa wa ile kashfa ya Richmond?
.Ndugu zangu mpaka leo bado hatujapata maelezo ya upande wa pili juu ya kashfa ile na hiki ndicho kinazidi kumpa umaarufu Mh.Lowassa na hivyo kumuweka kwenye uadilifu na nidhamu ya hali juu kwa mkuu wake.
Na jambo hili wanaoliona ni wachache sana na kadri zinavyokwenda wengi ndivyo watakavyouona ukweli huo.
Azidi kugawa hela labda idadi ya "wanaoliona" itaongezeka.
 
CHAMA CHA SIASA ni MABARABARANI NA MAJUKWAANI - JK NYERERE .
 
Mkuu wewe ni GT mzuri kabisa jibu hoja kwa hoja.Hivi ni lini na wapi ulisikia utetezi wa Mh.Lowassa juu ya Richmond?
Hukumu siku zote kwa kusikiliza pande zote mbili,sina hakika kama utakuwa umenielewa.Ila namaanisha ili mtu awe mtuhumiwa ni juu ya mamlaka kumfungulia jalada na kufanya chochote juu yake kwa mujibu wa sheria lakini mpaka leo hilo halipo.
Hivi uoni kwamba mtu huyu ni Innocent aliyewaokoa watu wake na gharama za kurudia uchaguzi..?
Mtu huyu angelikuwa ni fisadi angeliwachongea wenzake na yeye kuwa mkuu wa Nchi enzi ile lakini hakufanya hivyo sababu ya uadilifu wake.
Mnapoleta thread kama mtegemee kuwa na watu wenye mitazamo tofauti,hivyo hoja za matusi,kejeli na dhihaka hazifai.

UONGO UTAKUSAIDIA NINI ? NANI KAKUAMBIA KUSHIRIKIANA WIZI NA MKUBWA WAKO NDIO UTAKUWA SALAMA ? NJAA ITAKUTEKETEZA WEWE , LOWASA NI FISADI ALIYETHIBITISHWA NA BUNGE , HaLAFU MTU MMOJA MCHUMIA TUMBO UNATAKA KUPOTOSHA HAPA !
 
Mbona tuadanganyana mchana kweupe hao ndo watu 750? Hivi hawa ndg.wa cdm wakisema ukweli huwa wanapungukiwa na damu kwa bahati sitaki kuamini huo uwongo na sintakaa niamini kamwe ukweli ni hiyo picha jamani nisaidieni hao watu ni wangapi?
Hiyo picha inaonesha cross section ya wanaume tu bado kuna kina mama na watu wengine wengi ambao hatukuweza kuwapiga picha.Ukumbuke kazi iliyotupeleka huko sio kupiga picha.Ukitaka uhakika wa hii kazi tuma magamba mmoja aje ofisi ya Monduli a'approve kilichoandikwa hatafichwa kitu.
 
Mbona tuadanganyana mchana kweupe hao ndo watu 750? Hivi hawa ndg.wa cdm wakisema ukweli huwa wanapungukiwa na damu kwa bahati sitaki kuamini huo uwongo na sintakaa niamini kamwe ukweli ni hiyo picha jamani nisaidieni hao watu ni wangapi?

Futa delete ccm inakuja kwa kasi sana
 
Wanamkataa mkubwa wao? kweli sasa nimeamini yaliyosemwa yanatimia ...change is coming tomorrow,this time tomorrow, things gonna change.
 
Mkuu wewe ni GT mzuri kabisa jibu hoja kwa hoja.Hivi ni lini na wapi ulisikia utetezi wa Mh.Lowassa juu ya Richmond?
Hukumu siku zote kwa kusikiliza pande zote mbili,sina hakika kama utakuwa umenielewa.Ila namaanisha ili mtu awe mtuhumiwa ni juu ya mamlaka kumfungulia jalada na kufanya chochote juu yake kwa mujibu wa sheria lakini mpaka leo hilo halipo.
Hivi uoni kwamba mtu huyu ni Innocent aliyewaokoa watu wake na gharama za kurudia uchaguzi..?
Mtu huyu angelikuwa ni fisadi angeliwachongea wenzake na yeye kuwa mkuu wa Nchi enzi ile lakini hakufanya hivyo sababu ya uadilifu wake.
Mnapoleta thread kama mtegemee kuwa na watu wenye mitazamo tofauti,hivyo hoja za matusi,kejeli na dhihaka hazifai.

Kama hakuwa na makosa kwanini alijiuzulu? Maana JK hakutengua uteuzi wake!Kaka utakakamaa sana kumtetea EL, na kamwe hautafaulu; at least kwa kiwango cha kumjengea uhalali wa kisiasa na kuaminika pan territorially kwa wananchi ili aweze kusogea Magogoni creek! EL anahitaji uhalali wa kisiasa tu kuliko uamuzi wa kimahakama au tume ya maadili.EL akifanikiwa kuivua laana ya Baba wa Taifa na kashfa ya Richmonduli atafika Magogoni,na hilo utakuwa muujiza wa Karne kwani the guy made too many enimies also when he had it his way, power and influence, slick EL stepped on too many toes for his own good, now it is payback time.
 
Huo ndio mkutano kweli..!!? hawafiki hata watu 10...!!!!

Mnajipa moyo nyie kama mgonjwa wa ukimwi...!!"
 
Back
Top Bottom