Makala ya Mwananzela Raia Mwema: Inafaa wanasheria waende mahakamani kupinga Sheria ya katiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makala ya Mwananzela Raia Mwema: Inafaa wanasheria waende mahakamani kupinga Sheria ya katiba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Nov 30, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Nov 30, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0


  Wadau:

  Kama mmesoma kwa makini sana makala ya Lula wa Ndali Mwananzela katika RAIA MWEMA la leo ukurasa 9, ni dhahiri kabisa kwamba Mswada wa Mchakato wa kubadilisha katiba uliopitishwa na Bunge na kusainiwa na JK siyo halali kabisa – kutokana vipengele Na. 97 na 98 ya Katiba ya sasa.

  Anachosema Mwananzela (ambaye mimi naamini ndiye Mzee Mwanakijiji) ni kwamba ilitakiwa kwanza marekebisho ya Katiba ya sasa yafanywe marekebisho hasa katika Ibara ya 98 ya Katiba hii ya sasa.

  Sehemu husika Mwananzela anasema:

  “Kwanza mchakato (huu) usitishwe na mabadiliko ya Katiba ya sasa yafanyike kwanza. Ni lazima tuweke kwenye Katiba ya sasa namna ya kuhalalisha uandikaji wa katiba mpya ya nchi yetu. Sasa hivi tunaruhusiwa kufanyia marekebisho tu katika Katiba ya 1977 chini ya Ibara ya 98. Ina maana ipo haja aidha ya kuongeza Ibara ya 98B, itakayoelezea ni wakati gani nchi inaweza kuangalia uwezekano wa kuandika Katiba Mpya.”


  Kwa maana nyingine marekebisho hayo ya Ibara 98 yaeleze pia namna ya kuanzisha mchakato huo ili uwe halali.

  Wadau mwenye soft copy ya makala hiyo nzuri ya Mwananzela na aiweke hapa.

  Aidha nawaomba wanaharakati, na wanasheria waliangalie hili kwa namna jinsi ya ya kwenda mahakamani kutaka litolewe tamko kwamba Muswada wa sheria iliyopitishwa na Bunge wiki iliyopita ni kinyume cha Katiba ya sasa – yaani uhalali wake umetoka ‘hewani’ tu.

   
 2. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #2
  Nov 30, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kwanini unaamini kuwa huyo ni mzee mwanakijiji?
   
Loading...