Makala ya leo: Ukweli utakuweka huru

mizambwa

JF-Expert Member
Oct 8, 2008
4,422
1,790
By Padri Baptiste Mapunda

Makala katika Gazeti Mwananchi - 30/12/2015

Waziri Mkuu Majaliwa.jpg

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea zana za jadi kutoka kwa mzee Abdallah Hamis wakati wa ziara yake Ruangwa hivi karibuni.Picha ya Maktaba.

Awali ya yote napenda kuwatakia heri na Baraka za Mwenyezi Mungu kwa wasomaji wangu wote na wananchi kwa ujumla “ Heri ya Mwaka Mpya na Baraka tele kwenu nyote.”

Siku ya kwanza ya kila mwaka ni siku ya kumshukuru Mungu kwa yote tuliyotendewa na kuyapitia, ni siku ya kufanya tathmini katika maisha yetu. Pia, siku huu ni siku ya kutakiana mema bila kujali dini, itikadi, kabila wala rangi kwa sababu Baraka za Mungu hazibagui.

Tunapokaribia kuuanza mwaka mpya nimedhamiria kuandika makala haya ya “Mwaka mpya Serikali iache woga wa wapinzani” ili kufungua milango mipya ya kuishi kama ndugu, kujenga amani na ustawi katika taifa letu linalopitia changamoto lukuki. Ukweli ni kwamba Watanzania walio wengi hawakushangilia ushindi wa Rais John Magufuli kwa sababu hawakutegemea kwamba atashinda kiti hiki na pili kama inavyosemekana kwamba alipata kura zaidi ya milioni kumi hali hii imewafanya wananchi wengi waliotegemea kupata “mabadiliko ya kweli nje ya CCM” wakate tamaa.

Ukweli utakuweka huru umebaini kwamba tangu Uchaguzi Mkuu upite na mshindi kutangazwa Serikali na vyombo vya dola vyote vikiwa vinaongozwa na kuelekezwa na chama tawala (CCM) vimekuwa vikiwabana wapinzani kwa njia mbalimbali.

Moja ya njia hiyo ni ile ya mgopmbea wa upinzani kuhutubia mkutano pale Jangwani kwa nia ya kuwashukuru wapiga kura wake. Kama wakati wa kampeni na kutangaza matokeo wapinzani hao hawakufanya fujo ni kwa nini wafanye fujo wakati wa mgombea wao akiwashukuru? Ni kwa nini Serikali na vyombo vya dola vimeendelea kupiga marufuku mikutano ya siasa ikilenga hasa Ukawa au wapinzani wakati wanaCCM wanaendelea kuhutubia wananchi mfano halasi ni Waziri Mkuu aliyekuwa akihutubia na kuwashukuru wananchi mkoani kwake Lindi?

Hali hii inajenga picha kwamba Serikali ya CCM pamoja na vyombo vyake vya dola wanahofu kuhusu upinzani nchini. Swali la msingi nini wanahofia kiasi cha kupiga marufuku mikutano ya kisiasa bila sababu ya msingi? Je, demokrasia na utawala bora wanaouhubiri kila wakati majukwani vipo wapi sasa.

Tukumbuke kwamba wananchi sasa siyo wajinga na kwamba hawaelewi kinachoendelea katika nchi hii la hasha! Niliwahi kuandika katika moja ya magazeti mwaka jana wakati wa mchakato wa mabadiliko ya Katiba kwamba “ CCM ilikuwa imekumbwa na hofu kuu kama ya Mfalme Herofe aliposikia kwamba Mfalme mwingine kazaliwa tena mfalme wa amani, yaani mtoto Yesu Kristo.” Kumbe inaonekana wazi kwamba hofu ile bado inaendelea kukitafuna chama hiki kikongwe barani Afrika kwa sababu kubwa ya kulewa madaraka na kutaka kuendelea kutawala.

Tunapoanza Mwaka Mpya Serikali na vyombo vyake vya dola watafakari wanaipeleka wapi nchi yetu iliyoasisiwa na Baba wa amani Mwalimu JK Nyerere. Mwaka Mpya tunataka ukomavu wa demokrasia na utawala bora utamalaki nchini katika medani za siasa za vyama vingi badala ya kuturudisha nyuma kwenye siasa za chama kimoja, kinachoshika hatamu. Hakika inatia moyo kusikia karibu kila kona ya nchi jinsi Rais Magufuli “mtumbua majipu” na anayewasomesha namba wanaCCM wenzake kuwa ameanza kwa mkwara wake wa kuchimbua uozo wa Serikali ya Awamu ya Nne na huenda hata ile ya tatu na ya pili huwezi kujua kwa uhakika. Pamoja na Rais mpya kuanza kwa mkwara wake na kuonyesha kwamba amedharimia kuiendeleza Tanzania, sasa wananchi wengi wanajiuliza vipi kuhusu demokrasia na utawala bora?

Tanzania yenye neema na baraka zote bila kujenga msingi mizuri ya demokrasia na utawala bora ni sawa na kutwanga maji katika kinu kitu ambacho ni kuchelewesha ukuaji na ukomavu wa demokrasia nchini.

Hadi uchaguzi upite wananchi tumeshuhudia madudu mengi ambayo ni kinyume na demokrasia na utawala bora, lakini pia kinyume na haki za binadamu vikitendeka bila ya Rais wala Serikali yake kukemea vitendo hivi. Hivi maana yake nini? Tunaweza kusema kwamba mwaka huu tunaouanza basi mambo yatakuwa mabaya zaidi.

Sitarajii mabadiliko katika siasa za Tanzania, ninaona kutakuwa na maovu mengi, ukandamizaji mwingi kwa wapinzani kutoka kwa vyombo vya ulinzi na usalama kwa sababu ya kuibeba CCM ambayo imelewa madaraka.

Sijui ni muujiza gani utatokea ili siasa za Tanzania zibadilike, hata kama tutaendelea kuwaomba viongozi wa dini waiombe nchi hii kwa upande wangu naona ni kufuru kubwa kwa Mwenyezi Mungu.

Swali langu ni hili, kwa nini Serikali na vyombo vyake hawabadiliki? Na ni mara ngapi hata viongozi wa dini wameishauri na kuikemea Serikali ya CCM. Kwa nini haiwasikilizi na badala yake inawakejeli na mwishowe ni kuwatukana kama ilvyotokea katika Bunge Maalumu la Katiba? Hivi ukiona hayo yanatendeka unaweza kujidanganya kwamba siasa za Tanzania siku moja zitakuwa za kistaarabu, nikiwa mkweli naona hii ni ndoto ya mchana.

Nawaomba viongozi mkae chini na kutafakari kuhusu siasa zetu za mwaka 2015 na sasa mjaribu kupiga picha bila ushabiki mwakani mambo yatakuwaje?

Ukweli utawaweka huru. Nimebaini mwakani hali ya kisiasa nchini itazidi kuwa mbaya zaidi hii ni kwa sababu pia upinzani unazidi kukua kwa kasi na kukomaa na hivi kuongeza hofu kwa Serikali ya CCM.

Tutake tusitake Tanzania ni sehemu ya dunia inayobadilika yaani kiuchumi, kijamii, kitekinolojia na kisiasa pia ukweli huu haukwepeki.

Nazidi kujiuliza hivi siasa za mwaka 2016 zitakuwa za namna gani ukiangalia yale yanayoendelea kutendeka wakati huu. Nawatakieni heri na baraka tele kwa Mwaka Mpya 2016. Mungu ibariki Tanzania.
 
Last edited:
asante mapunda sikia na hii tanzania ni nchi ya amani asubuhi!usiku unasikia aliyekuwa mwandishi wa habari chanel ten daudi mwangosi amepigwa risasi na dubwana kubwa huko iringa
 
....ni maandiko ya padre baptiste mapunda hayo....!

Ni Makala yake katika Gazeti. Anataka tuanze mwaka 2016 vizuri kwa serikali kutowaogopa wapinzani. Endapo kama kampeni zilifanyika bila vurugu itakuwaje wafanye vurugu kipindi cha shukrani????

Hawakufanya vurugu baada ya matokeo kutangazwa... iweje wafanye vurugu wakati wa shukrani?????
 
....shukrani ya nini kwa alieshindwa?......mbona suala liko wazi? mbowe akienda hai kuwashukuru waliompigia kura zilizompa ushindi, inaeleweka...! hata majaliwa, au msigwa itaeleweka...lkn lowassa! anashukuru kwa kitu gani?
 
Kwani wewe ikiwa umeniomba nikupe Tshs. 5,000/= lakini mimi nikakupa Tshs. 3,000/=

Je hutosema Ahsante????????
 
.....omba omba hushukuru kwa chochote anachopewa...lowassa hakuwa akiomba kiasi fulani cha pesa akapewa pungufu ya alichoomba, alikuwa mgombea uraisi na alishindwa...! asitake kutuletea mbwa kachoka na paka chongo zinazojulikana miaka nenda miaka rudi ! washindi wenyewe ambao ndio haswa tukitegemea kuwaona wakipita kutoa shukrani kwa wapiga kura, wengi wao wako kwenye kutekeleza ahadi walizotoa wakakti wa kampeni..
 
We kwel sifur umetengenezewa lugha ya picha upate maana halis matokeo yake unatafsir picha badala ya ujumbe wa picha,kwa ufup wanataka kuwashukuru wale waliowaamin kwa kumpa kura ingawa hakufanikiwa kushinda
 
Ni Makala yake katika Gazeti. Anataka tuanze mwaka 2016 vizuri kwa serikali kutowaogopa wapinzani. Endapo kama kampeni zilifanyika bila vurugu itakuwaje wafanye vurugu kipindi cha shukrani????

Hawakufanya vurugu baada ya matokeo kutangazwa... iweje wafanye vurugu wakati wa shukrani?????

Hivi sheria ya vyama vya siasa inasemaje? Je, serikali inaweza kuamka tu asubuhi moja na kuzuia shughuli za vyama vya siasa ikiwa ni pamoja na kufanya mikutano ya hadhara? Haingii akilini kuwa serikali iliyochaguliwa kidemokrasia inaweza kufanya maamuzi ya aina hii. Sickening, to say the least.
 
We kwel sifur umetengenezewa lugha ya picha upate maana halis matokeo yake unatafsir picha badala ya ujumbe wa picha,kwa ufup wanataka kuwashukuru wale waliowaamin kwa kumpa kura ingawa hakufanikiwa kushinda
...sasa walioshinda uchaguzi ambao ye alishindwa wameona kuwa hilo la mshindwa kutaka ati kushukuru ni hoja koko na muflisi ktk kipindi hiki ambacho uchaguzi umekwisha na watu wakiwa wamejikita ktk kujenga nchi. hiyo mikutano yake itachangia nini ktk ujenzi wa nchi baada ya uchaguzi?.....na kama nia yake ni njema mbona hakutaka kuanzia monduli kwake?
 
Hivi sheria ya vyama vya siasa inasemaje? Je, serikali inaweza kuamka tu asubuhi moja na kuzuia shughuli za vyama vya siasa ikiwa ni pamoja na kufanya mikutano ya hadhara? Haingii akilini kuwa serikali iliyochaguliwa kidemokrasia inaweza kufanya maamuzi ya aina hii. Sickening, to say the least.

Serikali iliyopo madarakani inaogopa Upinzani kwa sababu hawakupita kihalali. Hivyo wamekuwa na HOFU. Ndio maana wamekuwa na kauli za kibabe katika utekelezaji wa majukumu yao.

Wanazuia mikusanyiko ya kisiasa hasa ya UKAWA kwani wanajua watu watajitokeza wengi na kuonyesha udhaifu kwa serikali.

Lakini yote haisaidii kitu kwa sababu kila kitu kitakuwa wazi. Kitaeleweka tu.
 
...sasa walioshinda uchaguzi ambao ye alishindwa wameona kuwa hilo la mshindwa kutaka ati kushukuru ni hoja koko na muflisi ktk kipindi hiki ambacho uchaguzi umekwisha na watu wakiwa wamejikita ktk kujenga nchi. hiyo mikutano yake itachangia nini ktk ujenzi wa nchi baada ya uchaguzi?.....na kama nia yake ni njema mbona hakutaka kuanzia monduli kwake?

Mkuu unaelewa unachosema lakini???????

Aanzie Monduli kivipi na ikiwa serikali wamepiga marufuku mikutano???

Una elewa kwua LOWASA ni mwananchi wa Monduli na kwa sasa siyo Mbunge, je kule atasimama kama nani???

Hata ikiwa Monduli kama serikali wakitoa ruhusa anaweza kwenda kufanya mkutano, kwani yote ni Tanzania.
 
By Padri Baptiste Mapunda

Makala katika Gazeti Mwananchi - 30/12/2015

View attachment 313825

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea zana za jadi kutoka kwa mzee Abdallah Hamis wakati wa ziara yake Ruangwa hivi karibuni.Picha ya Maktaba.

Awali ya yote napenda kuwatakia heri na Baraka za Mwenyezi Mungu kwa wasomaji wangu wote na wananchi kwa ujumla “ Heri ya Mwaka Mpya na Baraka tele kwenu nyote.”

Siku ya kwanza ya kila mwaka ni siku ya kumshukuru Mungu kwa yote tuliyotendewa na kuyapitia, ni siku ya kufanya tathmini katika maisha yetu. Pia, siku huu ni siku ya kutakiana mema bila kujali dini, itikadi, kabila wala rangi kwa sababu Baraka za Mungu hazibagui.

Tunapokaribia kuuanza mwaka mpya nimedhamiria kuandika makala haya ya “Mwaka mpya Serikali iache woga wa wapinzani” ili kufungua milango mipya ya kuishi kama ndugu, kujenga amani na ustawi katika taifa letu linalopitia changamoto lukuki. Ukweli ni kwamba Watanzania walio wengi hawakushangilia ushindi wa Rais John Magufuli kwa sababu hawakutegemea kwamba atashinda kiti hiki na pili kama inavyosemekana kwamba alipata kura zaidi ya milioni kumi hali hii imewafanya wananchi wengi waliotegemea kupata “mabadiliko ya kweli nje ya CCM” wakate tamaa.

Ukweli utakuweka huru umebaini kwamba tangu Uchaguzi Mkuu upite na mshindi kutangazwa Serikali na vyombo vya dola vyote vikiwa vinaongozwa na kuelekezwa na chama tawala (CCM) vimekuwa vikiwabana wapinzani kwa njia mbalimbali.

Moja ya njia hiyo ni ile ya mgopmbea wa upinzani kuhutubia mkutano pale Jangwani kwa nia ya kuwashukuru wapiga kura wake. Kama wakati wa kampeni na kutangaza matokeo wapinzani hao hawakufanya fujo ni kwa nini wafanye fujo wakati wa mgombea wao akiwashukuru? Ni kwa nini Serikali na vyombo vya dola vimeendelea kupiga marufuku mikutano ya siasa ikilenga hasa Ukawa au wapinzani wakati wanaCCM wanaendelea kuhutubia wananchi mfano halasi ni Waziri Mkuu aliyekuwa akihutubia na kuwashukuru wananchi mkoani kwake Lindi?

Hali hii inajenga picha kwamba Serikali ya CCM pamoja na vyombo vyake vya dola wanahofu kuhusu upinzani nchini. Swali la msingi nini wanahofia kiasi cha kupiga marufuku mikutano ya kisiasa bila sababu ya msingi? Je, demokrasia na utawala bora wanaouhubiri kila wakati majukwani vipo wapi sasa.

Tukumbuke kwamba wananchi sasa siyo wajinga na kwamba hawaelewi kinachoendelea katika nchi hii la hasha! Niliwahi kuandika katika moja ya magazeti mwaka jana wakati wa mchakato wa mabadiliko ya Katiba kwamba “ CCM ilikuwa imekumbwa na hofu kuu kama ya Mfalme Herofe aliposikia kwamba Mfalme mwingine kazaliwa tena mfalme wa amani, yaani mtoto Yesu Kristo.” Kumbe inaonekana wazi kwamba hofu ile bado inaendelea kukitafuna chama hiki kikongwe barani Afrika kwa sababu kubwa ya kulewa madaraka na kutaka kuendelea kutawala.

Tunapoanza Mwaka Mpya Serikali na vyombo vyake vya dola watafakari wanaipeleka wapi nchi yetu iliyoasisiwa na Baba wa amani Mwalimu JK Nyerere. Mwaka Mpya tunataka ukomavu wa demokrasia na utawala bora utamalaki nchini katika medani za siasa za vyama vingi badala ya kuturudisha nyuma kwenye siasa za chama kimoja, kinachoshika hatamu. Hakika inatia moyo kusikia karibu kila kona ya nchi jinsi Rais Magufuli “mtumbua majipu” na anayewasomesha namba wanaCCM wenzake kuwa ameanza kwa mkwara wake wa kuchimbua uozo wa Serikali ya Awamu ya Nne na huenda hata ile ya tatu na ya pili huwezi kujua kwa uhakika. Pamoja na Rais mpya kuanza kwa mkwara wake na kuonyesha kwamba amedharimia kuiendeleza Tanzania, sasa wananchi wengi wanajiuliza vipi kuhusu demokrasia na utawala bora?

Tanzania yenye neema na baraka zote bila kujenga msingi mizuri ya demokrasia na utawala bora ni sawa na kutwanga maji katika kinu kitu ambacho ni kuchelewesha ukuaji na ukomavu wa demokrasia nchini.

Hadi uchaguzi upite wananchi tumeshuhudia madudu mengi ambayo ni kinyume na demokrasia na utawala bora, lakini pia kinyume na haki za binadamu vikitendeka bila ya Rais wala Serikali yake kukemea vitendo hivi. Hivi maana yake nini? Tunaweza kusema kwamba mwaka huu tunaouanza basi mambo yatakuwa mabaya zaidi.

Sitarajii mabadiliko katika siasa za Tanzania, ninaona kutakuwa na maovu mengi, ukandamizaji mwingi kwa wapinzani kutoka kwa vyombo vya ulinzi na usalama kwa sababu ya kuibeba CCM ambayo imelewa madaraka.

Sijui ni muujiza gani utatokea ili siasa za Tanzania zibadilike, hata kama tutaendelea kuwaomba viongozi wa dini waiombe nchi hii kwa upande wangu naona ni kufuru kubwa kwa Mwenyezi Mungu.

Swali langu ni hili, kwa nini Serikali na vyombo vyake hawabadiliki? Na ni mara ngapi hata viongozi wa dini wameishauri na kuikemea Serikali ya CCM. Kwa nini haiwasikilizi na badala yake inawakejeli na mwishowe ni kuwatukana kama ilvyotokea katika Bunge Maalumu la Katiba? Hivi ukiona hayo yanatendeka unaweza kujidanganya kwamba siasa za Tanzania siku moja zitakuwa za kistaarabu, nikiwa mkweli naona hii ni ndoto ya mchana.

Nawaomba viongozi mkae chini na kutafakari kuhusu siasa zetu za mwaka 2015 na sasa mjaribu kupiga picha bila ushabiki mwakani mambo yatakuwaje?

Ukweli utawaweka huru. Nimebaini mwakani hali ya kisiasa nchini itazidi kuwa mbaya zaidi hii ni kwa sababu pia upinzani unazidi kukua kwa kasi na kukomaa na hivi kuongeza hofu kwa Serikali ya CCM.

Tutake tusitake Tanzania ni sehemu ya dunia inayobadilika yaani kiuchumi, kijamii, kitekinolojia na kisiasa pia ukweli huu haukwepeki.

Nazidi kujiuliza hivi siasa za mwaka 2016 zitakuwa za namna gani ukiangalia yale yanayoendelea kutendeka wakati huu. Nawatakieni heri na baraka tele kwa Mwaka Mpya 2016. Mungu ibariki Tanzania.
 
Kwa nini CCM wahofu kama wanafahamu kuwa ushindi wao hauna kama walakini? Nadhan kama siyo hofu ya madudu yao ya uchaguzi kuwekwa wazi, wangeruhusu EDDO awashukuru watanzania kwa kidogo walichompa.ccm+magufuli kuwa washindi hakuwafanyi kuweka utawala wa sheria mfukoni
 
.....omba omba hushukuru kwa chochote anachopewa...lowassa hakuwa akiomba kiasi fulani cha pesa akapewa pungufu ya alichoomba, alikuwa mgombea uraisi na alishindwa...! asitake kutuletea mbwa kachoka na paka chongo zinazojulikana miaka nenda miaka rudi ! washindi wenyewe ambao ndio haswa tukitegemea kuwaona wakipita kutoa shukrani kwa wapiga kura, wengi wao wako kwenye kutekeleza ahadi walizotoa wakakti wa kampeni..
Unatumia nguvu kubwa sana kujibu utumbo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom