Makala nilisiyoisahau kutoka Mwanahalisi ya kumuhusu Lowassa

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
Lowassa hajakomaa kisiasa

Na Malaila Junior - Imechapwa 12 March 2008


MTAALAMU yeyote wa masuala ya siasa, achambue kadri awezavyo, hawezi kukwepa ukweli kwamba siasa ni msingi wa maendeleo kwa watu na taifa lao.

Katu hawezi kukana hoja ya kuwa siasa ni muunganisho wa fikra za watu za kuwajengea umoja na mshikamano wa kitaifa kwa lengo la kuwakomboa kiuchumi, kisiasa, kijamii na kidemokrasia.

Hivyo basi, anayestahili kuitwa mwanasiasa safi, jasiri, mkomavu na bora, ni yule aliyefanikiwa kulitekeleza lengo hili kikamilifu.

Yule aliyefanikiwa kuwafikisha watu wake pale walipokuwa wakitarajia, au katika nukta ambayo dhahiri wao watasadiki kuwa wanaelekea kule wanapopataka.

Wanasiasa waliofaulu katika hili au watakaofaulu, hao ndiyo wanaostahili kupewa sifa na pongezi, lakini si wale wanaosinzia bungeni wakati mijadala makini ikipamba moto.

Si wale waliosaidia kulitumbukiza taifa hili katika hasara kubwa kufuatia mikataba mibovu iliyosainiwa chini ya dhamana zao.

Kwa hakika, ni dhambi kubwa kuwapongeza wanasiasa wa aina hii. Hii ni kwa sababu, wamepoteza hadhi na heshima yao mbele ya wale wanaowaongoza.

Pamoja na kuwepo wa ukweli huu, katika siku za karibuni kumekuwapo na genge la watu linalopita huku na kule na kuwamwagia sifa na pongezi mtu mmoja kwa hoja kwamba kutokana na uamuzi wake wa kujiuzulu.

Huyo si mwingine, bali ni Edward Lowassa, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri.

Hili ni jambo kubwa na la hatari sana kwa mustakabali wa nchi. Maana watu walioshiriki kwa namna moja ama nyingine kuhujumu maslahi ya wananchi na nchi kutokana na mkataba wa kinyonyaji wa Richmond, anawezaje kusafishwa na kuitwa shujaa?

Lowassa si mtu makini, kama wanaomsafisha wanavyotaka tuamini. Angekuwa makini, katu asingethubutu kulitumbukiza taifa lake katika ujinga huu.

Lowassa si mkomavu wa kisiasa kama wanaomtumikia wanavyotaka kutuonyesha.
Kama ingekuwa Lowassa amekomaa, katu asingekurupuka kujiuzulu bila kwanza kujitetea, badala yake anapita mitaani kumwaga porojo.

Lowassa hajawahi na hawezi tena kuwa mtu shupavu na mwenye kuona mbali.
Kama Lowassa, angekuwa shupavu na mwenye kuona mbali, asigeshindwa kutumia nafasi aliyopewa ya kilitumikia taifa, badala yake akashiriki katika kulitafuna taifa lake.

Wala Lowassa hajawa jasiri, kama wanaopita huku na kule kutaka kumuosha wanavyotaka tuamini.

Nasema hivi: kama Lowassa angekuwa jasiri, asingekubali kujiuzulu kwa shingo upande, huku akilalama kwamba "uwaziri mkuu wake."

Jamii ya Watanzania itakuwa inafanya makosa sana iwapo itakubali kuaminishwa kirahisirahisi kwamba kila anayejiuzulu ni mkomavu, ni hodari, ni shupavu na jasiri.
Ni lazima umma utazame historia ya kiongozi huyo. Tathmini ya namna hii ikifanywa katika utendaji wa Lowassa, zinamvua sifa hizo.

Alipokuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Lowassa alikumbwa na kashfa ya ununuaji magari ya serikali.

Alipokwenda wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo Mijini, ni katika kipindi hicho alipoliingiza taifa katika migogoro mingi ya ardhi.

Dosari za namna hii ziliendelea kumuandama Lowassa hata pale alipokuwa Waziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo.

Ni katika kipindi chake, serikali iliimgia mkataba na kampuni ya City Water, ambapo sasa imedhirika kwamba kampuni hiyo ilikuwa Richmond nyingine. Ilivuna ambacho hakikupanda.

Majigambo ya Lowassa kwamba ni yeye aliyevunja mkataba huo hayana msingi. Maana hapa anakwepa jukumu lake jingine. Je, nani aliliingiza taifa katika mkataba huo kama si yeye mwenyewe?

Kwa miaka miwili ambayo amekalia kiti cha waziri mkuu, Lowassa amefanya mambo mengi ya hovyo.

Ni katika kipindi hicho, serikali ilipoteza kabisa mwelekeo wake mbele ya wananchi kutokana na kutawaliwa na maagizo mengi yaliokwenda kinyume na maamuzi ya serikali.

Huyo ndiyo Lowassa ambaye wako wanaodiriki kumwita mkomavu wa kisiasa, jasiri, shujaa wa maamuzi, mtu mwenye ari na aliyetayari kujitoa muhanga kutetea maslahi ya wananchi wake.

Je, hivi ni kweli kwamba mizani anayopimwa Lowassa inastahili?

Mwanahalisi
 
Ushamba mzigo

Tatizo hujui kanuni mbili kuu za siasa ,

Politics is dynamic not static
There are no permanent friends or foes in politics

Tafuta mtu akutafsirie kisha rudi singida Dodoma uwahi kilimo cha mbegu za mafuta
 
Ushamba mzigo

Tatizo hujui kanuni mbili kuu za siasa ,

Politics is dynamic not static
There are no permanent friends or foes in politics

Tafuta mtu akutafsirie kisha rudi singida Dodoma uwahi kilimo cha mbegu za mafuta
Tambala la deki,upo?!
 
Ushamba mzigo

Tatizo hujui kanuni mbili kuu za siasa ,

Politics is dynamic not static
There are no permanent friends or foes in politics

Tafuta mtu akutafsirie kisha rudi singida Dodoma uwahi kilimo cha mbegu za mafuta
Kwa hyo ulitaka kusemaje mkuu
 
Leo mwanahalisi hao hao ni wapangusa viatu vya Lowasa!!!

Njaa Mbaya sana
9d7714742007b37c21624d9d47e6fec3.jpg
Kubenea Construction Co @ work
 
Ushamba mzigo

Tatizo hujui kanuni mbili kuu za siasa ,

Politics is dynamic not static
There are no permanent friends or foes in politics

Tafuta mtu akutafsirie kisha rudi singida Dodoma uwahi kilimo cha mbegu za mafuta

Mbona wengine Mnawaita Wanafiki mfano wakirudi CCM ?
 
Kwa Tanzania upinzani halisi ulishakufa pale walipoingia mkenge kumpokea lowasa......amewapora hoja muhimu ya ufisadi iliyowainua na kuwapa credit
 
acheni zenu,bhana iyo ilikuwa 2008 saw na sasa kwan? au siasa za kipind iko zimekuwa kam za hivi karbun? mi nadhani lowasa kam kwel hakuwa kakomaa,but now amekomaa so msitafute sababu yoyte ktaka kuwapondea cdm.
 
Siasa haina adui wa kudumu kwa nani? kwa wananchi au ni kwa wanasiasa wenyewe?

Haiwezekani fisadi ambaye ni adui wa wananchi ajekuwa rafiki yetu hali ni bado fisadi,huu msemo wa siasa haina adui wala rafiki wa kudumu itabaki kwa wanasiasa wenyewe na si kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom