Makala: Miaka 20 ya Putin ulingoni

Rubawa

JF-Expert Member
Dec 25, 2015
2,055
3,238
Miongo miwili ulingoni, Putin na mkakati wa kubakia madarakani.

NA MOHAMMED ABDULRAHMAN

Jina la Vladimir Putin ni maarufu sana miongoni mwa viongozi wa dunia kama lilivyo la Donald Trump. Rais huyu wa taifa kubwa la Urusi aliyekuwa afisa wa Shirika la ujasusi KGB kwa miaka 16 akiwa na cheo cha Luteni Kanali alianza kugonga vichwa vya habari alipojimwaga kwenye ulingo wa kisiasa Saint Petersburg 1991 alipojiuzulu kazi hiyo ya ukachero.

Saint Petersburg, ulirudishiwa jina lake hilo la zamani uliposambaratika Muungano wa Jamhuri za Kisovieti 1991, lilipofutwa baada mapinduzi ya 1917 na kuitwa Leningrad, kumuenzi muasisi wa mapinduzi hayo, wajina wake Vladimir Lenin.

Agosti 1999 kwa mshangao wa wengi, Putin aliteuliwa na rais Boris Yeltsin kuwa Waziri mkuu na kusema ndiye anayemtaka awe mrithi wake.
Katika tukio lisilotarajiwa mkesha wa mwaka mpya Desemba 1999 Yelstin akalitangazia taifa anajiuzulu na kwa mujibu wa katiba Putin akawa kaimu Rais na kuanza kujiimarisha akijitokeza kugombea uchaguzi uliofanyika miezi mitatu baada ya Yeltsin kujiuzulu.

Sababu za mwanasiasa huyo mkongwe Yeltsin kuamua kuacha madaraka ilikuwa ni pamoja na hali yake ya afya iliochangiwa na unywaji pombe kupita kiasi. Alishindwa kuongoza na kuonekana dhaifu katika utoaji maamuzi, huku akikosolewa vikali kwa upendeleo. Rushwa ilikithiri na jamii kuanza kujiuuliza kama hayo ndiyo matunda ya Demokrasia ambayo Yeltsin aliyemuangusha madarakani Michail Gorbachev akiinadi .

Warusi wengi na hasa wafuasi wa chama tawala cha zamani cha Kikoministi wanashutumu Gorbachov kuwa chanzo cha kusambaratika dola lao kubwa, Muungano wa Jamhuri za Kisovieti na vile vile ndiye sababu ya kuzuka hatari ya kuporomoka kwa nguvu ya Urusi katika kukabiliana na Marekani, kuweka wizani wa kisiasa na kijeshi duniani.

Udhaifu wa Yeltsin ambaye alionekana dhahiri kutokuwa na dira, uliifungulia mlango Marekani kuwa dola pekee lenye usemi na lililofanikiwa katika kupambana na ukoministi. Yote hayo yalijiri baada ya Gorbachov kuanza kutekeleza sera yake ya Perestroika na Glasnost ( Mageuzi na Uwazi). Wakosoaji wake wanaamini alifungua milango wazi ya Uhuru, ambao haukuwa na mipaka na hatimaye akashindwa kuudhibiti.

Kwa upande wake Yelstin aliyetambua madaraka ni mazito na yamemshinda akatafuta muokozi na ndipo alipomuona Putin .

Mara tu baada ya Putin kushika hatamu za kuliongoza taifa hilo kubwa aliposhinda uchaguzi mwaka 2000, akaanza kujenga nguzo za Urusi iliokuwa ikiporomoka na zaidi katika sekta yakiuchumi na kijeshi. Lengo lake lilikuwa kurudisha hadhi ya Urusi kama taifa lenye nguvu. Ni dhahiri hatari ya hali hiyo akiiona kutokana na maarifa yake kama afisa wa ngazi ya juu wa zamani wa Shirika la ujasusi KGB. Alifahamu enzi za chama cha kikoministi ilikuwa imeanza kuzikwa, lakini aliutumia mfumo ule ule wa kuongoza na kudhibiti, akiibuka kuwa kiongozi mwenye ujasiri.

Ninaporudi nyuma na kuidurusu historia ya kisiasa ya Urusi baada ya vita vya pili vya dunia, nina mfananisha na Leonid Brezhnev aliyechukua nafasi ya Nikita Krushchev kama Katibu mkuu wa Chama na Kiongozi mkuu 1964 na kutawala miaka 18. Brezhnev ni mmoja wa viongozi wakuu shupavu wa uliokuwa Muungano wa Jamhuri za Kisovieti (Urusi ya zamani).

Alhamisi iliopita Machi 26, Putin alitimiza miaka 20, mihula miwili kamili tokea aakabidhiwe hatamu za kuiongoza Urusi. Warusi wanaamini kwa namna moja au nyengine ameliokoa taifa lao na wafuasi wake hawakubaliani na hoja kwamba utawala wake ni sawa na uimla. Wanaamini chini ya utawala wa Yeltsin nchi yao ikielekea katika janga kubwa la kisiasa na kiuchumi.

Mahasimu wake wakiwemo wakoministi walimkosoa na kushangazwa kuwa alijitenga na falsafa iliomlea ya ukoministi na kufuata sera ya soko huru. Wadadisi wengine lakini, walimsifu kwa kuuona na kuutambua ukweli wa mambo. Putin akaanza kuchukua hatua za mabadiliko, kujenga uchumi na kurejesha hadhi ya taifa hilo.

Kufanikisha malengo yake, katika jukwaa la Kimataifa alirejesha uhusiano mwema na China, ambao uliharibika kwa miaka mingi , wakati ndugu hao wawili katika ukoministi walipofarakana 1962 kutokana na tafauti za kifalsafa. Urusi iliiunga mkono China na kuisaidia, baada ya wakoministi kushinda vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuunda Jamhuri ya Umma wa China 1949.
Putin aliuita uhusiano mpya na China kuwa ni “ushirika” na maka jana alikuwa miongoni mwa viongozi waalikwa katika sherehe ya miaka 70 ya kuundwa kwa Jamhuri hiyo.

Akijua ana mshirika wa uhakika kijiografia , mwenye nguvu na ushawishi katika siasa za kimataifa, Putin akaanza kukabiliana na Jumuiya ya kujihami ya NATO yenye wanachama 29 na inayoongozwa na Marekani. Mvutano wa pande hizo mbili ukatuwama zaidi kutokana na hatua ya Urusi kulitwaa eneo la Crimea la Ukraine , kuingia vitani na Jamhuri hiyo ya zamani ya Kisovieti na kulitia msukosuko eneo lake la mashariki kukiibuka hisia za kutaka kujitenga na Ukraine. Pia suala la Syria likawa eneo jengine la kupimana nguvu. Putin akajiunga na Iran kuunga mkono utawala wa Rais Bashar al-Assad .

Tangu matukio ya kuangushwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi 2011, Urusi imekuwa ikijiweka upande wa pili unaokinzana na Marekani katika migogoro yote . Hali hii inafuatia kutoaminiana kulikozuka na NATO baada ya azimio la Umoja wa Mataifa kuzuwia ndege Gaddafi kuwashambulia raia wanaompinga katika mji wa Benghazi kuliko anzia uasi dhidi yake. Urusi ilioliunga mkono azimio hilo inaamini lilikiukwa na Marekani, Uingereza na Ufaransa, wanachama wenzake katika Baraza la Usalama na zikalitafsiri vyengine na kumshambulia Gaddafi kwa kuwaunga mkono waasi, hadi alipoangushwa na kuuwawa.

Katika vita vya kuwania madaraka vinavyoendelea nchini Libya, Urusi inamuunga mkono Jemedari Khalifa Haftar dhidi ya serikali inayotambuliwa kimataifa mjini Tripoli ya waziri mkuu Fayez al-Saraj, kukiwa na taarifa za kuwepo kwa askari wa kukodiwa kutoka Urusi wanaomsaidia Haftar.
Lakini pembezoni Putin amekuwa akiuma na kupuliza ili yatakapogeuka aendelea kuwa na ushawishi hasa panapohusika na masilahi ya kiuchumi ambayo ni utajiri mkubwa wa mafuta nchini Libya. Hilo lilidhihirika alipoitisha mkutano wa upatanishi mjini Moscow Januari mwaka huu kwa akishirikiana na Rais Recep Tayep Erdogan wa Uturuki na kuwaalika Haftar na Saraj kujaribu kuleta suluhisho la mgogoro huo. Mkutano huo lakini haukua na mafanikio na wala mahasimu hao wawili nchini Libya hawakukutana ana kwa ana .

Putin ana usuhuba wa kimkakati na Rais Recep Tayep Erdogan wa Uturuki licha ya kuwa ni mwanachama wa NATO na pamoja na kwamba wanatafautiana juu ya kuendelea kuweko madarakani Bashar al-Assad nchini Syria. Uhusiano wao hata hivyo hauifurahishi Marekani hata kidogo huku kuelewana kwa Rais wake Donald Trump na mwenzake wa Urusi kukiwa sawa na maji kujaa na maji kukupwa. Hupongezekana na kushutumiana ikitegemea kila mmoja anafaidika vipi na hali na hali iliojitokeza tukio husika.

Ili kutanua ushawishi wake katika mashariki ya kati Putin ana mahusiano mazuri na Iran na Saudi Arabia mataifa mawili yenye utajiri mkubwa wa mafuta na ushawishi wa kisiasa katika eneo la ghuba na mashariki ya kati kwa jumla. Wakati akiwa ametimiza mihula miwili ya kuliongoza taifa hilo kubwa la Urusi, inaelekea bado Putin hana mpango wowote wa kun´gatuka mapema.

Mbinu zake zilianza 2008 alipomaliza mhula wake wa pili kama Rais na kuzuilika kikatiba kugombea kipindi cha tatu . Alibadilishana wadhifa na Waziri mkuu Dmirty Medvedev aliyechukua kiti cha Urais na Putin kuwa Waziri mkuu hadi 2012, wakati Putin aliporudi tena.
Mwezi Januari mwaka huu Medvedev alijiuzulu pamoja na baraza zima la mawaziri na Putin kumteuwa Waziri mkuu mpya. Lakini hakumtupa sahibu yake wa chanda na pete aliyekuwa awali kabisa meneja wa kampeni yake ya uchaguzi , bali alimteuwa Medvedev kuwa Makamu mwenyekiti wa baraza la usalama la taifa.

Ukiwa muendelezo wa mbinu za kubakia madarakani, Putin amependekeza mabadiliko ya katiba ambayo yalikuwa yapigiwe kura ya maoni na umma mwezi ujao, lakini imeahirishwa kwasababu ya janga la Corona. Mabadiliko hayo yanaweza kumfungulia nafasi ya kubakia madarakani hadi 2036 baada ya muhula wake kumalizika 2024. Putin ana umri wa miaka 67 na wakati huo atakuwa miaka 83. Katika siasa hakuna anayeweza kutabiri matukio, lakini kwa sasa bado Urusi ni Putin na Putin ndiyo Urusi .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Russia ya leo kiukweli pasipo Putin isingeweza kufika hapo

Makala yenyewe hii nkitulia ntaipitia kwa umakini kabsa kwa uwezo Wa Muumba

Sent using My COVID-19
 
Kwa alivyo jijenga na kuweza kuwadhibiti wapinzani wake naaamini lazima ameshaanza kuandaa mrithi wake kwa muda mrefu kam walivyo muandaa yeye, tunashukuru sana kwa makala nzuri. Je na sasa uwezo wake wa kijeshi ukoje?.
 
Kagame ni rwanda na rwanda ni kagame

Una taka kusema ivi pia au

Sent from my SM-A105G using Tapatalk
 
Urusi kwa hivi karibuni imekuwa ikiunga mkono wanaofeli. Akina Madulo, kipindi cha mwisho cha Zuma na huyo Haftar mwenyewe aliwahi kuwa Marekani na alikuwa mmojawapo ya waliomuasi Ghaddafi.
Sera za Urusi kibiashara na uwekezaji bado hazijatosha maana wanategemea sana kuuza rasilimali kama mafuta na gesi.
Putin kakuza sana uchumi wa Urusi kutoka kwa Yeltsin aliyekuwa mjingamjinga tu.

Sasahivi Putin hana mpinzani mkubwa kwani Boris Nemtsov aliyekuwa mpinzani wake wa nguvu na ndiye aliyetakiwa kuwa mrithi wa Yeltsin aliuwawa kwa risasi mwaka 2015.
Ikumbukwe Yeltsin alitafuta mtu atakayelinda maslahi yake na ya rafiki zake ma-oligarch na aliyekuwa na uwezo huo ni Putin, simply kwa kuwa alikuwa katokea KGB na ni inner circle ya Politburo. Nemtsov alikuwa na uwezo mkubwa wa kufanya mageuzi lakini alikuwa hana upendeleo, amenyooka na ndo maana alimsumbua sana Putin kwenye masuala ya demokrasia, rushwa na ubadhilifu wa waandamizi wake. Pia Nemtsov alionekana legelege hivi, kuongoza nchi kama Urusi bila ubabe ni kazi sana maana wamezoea ubabe.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom