Makala: Kwanini sasa wanafunzi wanafaulu kuliko zamani?

Makala: Kwanini sasa wanafunzi wanafaulu kuliko zamani?

(Uchambuzi wa Mabadiliko ya Grading – CSEE na ACSEE Tanzania)

Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na mjadala mkubwa kuhusu ongezeko la ufaulu kwa wanafunzi wa Tanzania, hasa katika Form Four (CSEE) na Form Six (ACSEE). Wengi hujiuliza

Je wanafunzi wa sasa wamesoma zaidi kuliko wa zamani, au kuna sababu nyingine?

Ukweli ni huu,mitihani ni ile ile, lakini mfumo wa grading ndio umebadilishwa, na hapo ndipo siri ya ufaulu mkubwa wa sasa ilipo.

1. GRADING YA FORM FOUR (CSEE): ZAMANI VS SASA

Grading ya ZAMANI (Old System kabla ya mabadiliko)
A: 81 – 100
B: 61 – 80
C: 41 – 60
D: 21 – 40
F: 0 – 20

Grading ya SASA (Current System)
A: 75 – 100
B: 65 – 74
C: 45 – 64
D: 30 – 44
F: 0 – 29

2. UCHAMBUZI: KWANINI SASA NI RAHISI KUAFAULU (CSEE)
(a) Kushushwa kwa Kiwango cha A
Zamani: A ilianza 81
Sasa: A inaanzia 75

Hii ina maana mwanafunzi aliyepata 78:
Zamani: B
Sasa: A

Idadi ya A imeongezeka bila mabadiliko ya kiwango cha mitihani.

(b) Kuinuliwa kwa Daraja la C
Zamani: 41–60
Sasa: 45–64

👉 Wanafunzi waliokuwa D ya juu zamani, sasa wanaingia C.

Matokeo yake Ufaulu wa jumla (pass rate) unaonekana umeongezeka.

(c) Pass imepandishwa, lakini Fail pia imepanuliwa
Zamani D (Pass) ilianza 21
Sasa D (Pass) inaanzia 30
Fail sasa ni hadi 29 (badala ya 20)

Hii inafanya matokeo yaonekane yamepangwa vizuri, lakini mgawanyo umebadilishwa kisaikolojia ili ufaulu uonekane mzuri zaidi.

3. GRADING YA FORM SIX (ACSEE): ZAMANI VS SASA

Grading ya ZAMANI (ACSEE – Old System)
A: 80 – 100
B: 70 – 79
C: 60 – 69
D: 50 – 59
E: 40 – 49
F: 0 – 39

Grading ya SASA (ACSEE – Current System)
A: 75 – 100
B: 65 – 74
C: 45 – 64
D: 35 – 44
E: 30 – 34
F: 0 – 29

4. UCHAMBUZI: KWANINI ACSEE YA SASA NI RAHISI KULIKO ZAMANI
(a) A-Level A Imeshushwa
Zamani: A ilianza 80
Sasa: A inaanzia 75

Mwanafunzi wa Physics au Mathematics aliyepata 76
Zamani: B
Sasa: A

Hii inaongeza idadi ya Division One bila kubadilisha ugumu wa mitihani.

(b) C na D Zimepanuliwa Sana
Zamani: C = 60–69
Sasa: C = 45–64

Hii inabeba wanafunzi wengi wa wastani kwenda juu zaidi.

5. MITIHANI NI ILE ILE, KINACHOBADILIKA NI GRADING
Ni muhimu kuelewa jambo hili Silabasi ni ile ile
Aina ya maswali ni ile ile
Kiwango cha ugumu kimebaki kile kile
Kilichobadilishwa ni mipaka ya alama (grading thresholds)
Hivyo, ufaulu wa sasa hauonyeshi moja kwa moja kuwa wanafunzi wa sasa wana akili au maarifa kuliko wa zamani, bali unaonesha mabadiliko ya mfumo wa upimaji.

6. MFANO HALISI: FORM SIX 2013 (TANZANIA NZIMA)
Mwaka 2013, matokeo ya ACSEE yalionesha hali halisi ya ugumu wa mfumo wa zamani:
Tanzania One (Division One ya juu kabisa)
👉 Mwanafunzi mmoja tu alifanikiwa kupata Division One ya pointi chache sana (mfano pointi 5) nchini kote.
Physics
👉 Hakukuwa na A hata moja ya Physics Tanzania nzima.

Hii haimaanishi wanafunzi walikuwa wajinga, bali
Grading ilikuwa kali
A ilikuwa ngumu sana
Mfumo ulipima tofauti ndogo sana za uwezo

🔹 Zamani ufaulu ulikuwa mgumu kwa sababu grading ilikuwa kali
🔹 Sasa ufaulu ni rahisi kwa sababu grading imelegezwa
🔹 Mitihani haijabadilika sana mfumo wa alama ndio umebadilika
🔹 Matokeo ya sasa yanaonekana mazuri, lakini hayalingani moja kwa moja na kiwango cha maarifa ya zamani
Vile vile mitihani ni miepesi mfano physics A level ukisoma Chand na ukasolve maswali yake ujue umefaulu lakini enzi zetu kulikuwa na vitabu vingi mno mfano Thom Duncan, Nelcon, ABC modern, Compressor, CHAND, Roger Muncaster na UP. Kiufupi km ningesoma zama hizi ningekua TO. Elimu imekuwa nyepesi plus unemployment rate ni kubwa hata mchikichini na mapambano mwenge watu sio wengi kivilee
 
Mtu toka darasa la kwanza mpaka la tano yupo na kitabu cha kibanga ampiga mkoloni mara sadiki,fikiri unamalizia na sungura sizitaki mbichu hizi haya madudu yalitufanya tudumae sana watoto wa siku hizi biology ya kidato cha tatu na nne wao wanasoma kwenye darasa la tano lazima uwezo utofautiane mtoto darasa la sita anafanya maswali ya resistance wakati wengine mpaka wanaliza kidato cha nne hawajakutana na hizi mambo ndio maana watoto wanafanya vizuri..
 
Mwaka nilio maliza mimi na kumbukumbu zangu Dar nzima kulikwa na one moja ya nane tena demu Naomi (Jangwani-Sasa hivi ni Meneja KMPG), mwengine alipiga one ya Tisa Atupele Kilindu (Forodhani) Advance akapiga tatu(Mzumbe) akawa wa sita kitaifa mara ya mwisho nilimsikia yupo kwenye kampuni ya mafuta ya Wajerumani.Yaani enzi hizo single digiti unatafuta kwa tochi yaani zinahesabika.

Ila sasa shule nzima ina one wa mwisho ana one wa 13,yaani mpaka mnajiuliza may be zamani tulikuwa tunacheza au siku hizi mitihani mepesi,yaani sasa hivi one ya saba sio story kitu cha kawaida.
 
(Uchambuzi wa Mabadiliko ya Grading – CSEE na ACSEE Tanzania)

Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na mjadala mkubwa kuhusu ongezeko la ufaulu kwa wanafunzi wa Tanzania, hasa katika Form Four (CSEE) na Form Six (ACSEE). Wengi hujiuliza

Je wanafunzi wa sasa wamesoma zaidi kuliko wa zamani, au kuna sababu nyingine?

Ukweli ni huu,mitihani ni ile ile, lakini mfumo wa grading ndio umebadilishwa, na hapo ndipo siri ya ufaulu mkubwa wa sasa ilipo.

1. GRADING YA FORM FOUR (CSEE): ZAMANI VS SASA

Grading ya ZAMANI (Old System kabla ya mabadiliko)
A: 81 – 100
B: 61 – 80
C: 41 – 60
D: 21 – 40
F: 0 – 20

Grading ya SASA (Current System)
A: 75 – 100
B: 65 – 74
C: 45 – 64
D: 30 – 44
F: 0 – 29

2. UCHAMBUZI: KWANINI SASA NI RAHISI KUAFAULU (CSEE)
(a) Kushushwa kwa Kiwango cha A
Zamani: A ilianza 81
Sasa: A inaanzia 75

Hii ina maana mwanafunzi aliyepata 78:
Zamani: B
Sasa: A

Idadi ya A imeongezeka bila mabadiliko ya kiwango cha mitihani.

(b) Kuinuliwa kwa Daraja la C
Zamani: 41–60
Sasa: 45–64

👉 Wanafunzi waliokuwa D ya juu zamani, sasa wanaingia C.

Matokeo yake Ufaulu wa jumla (pass rate) unaonekana umeongezeka.

(c) Pass imepandishwa, lakini Fail pia imepanuliwa
Zamani D (Pass) ilianza 21
Sasa D (Pass) inaanzia 30
Fail sasa ni hadi 29 (badala ya 20)

Hii inafanya matokeo yaonekane yamepangwa vizuri, lakini mgawanyo umebadilishwa kisaikolojia ili ufaulu uonekane mzuri zaidi.

3. GRADING YA FORM SIX (ACSEE): ZAMANI VS SASA

Grading ya ZAMANI (ACSEE – Old System)
A: 80 – 100
B: 70 – 79
C: 60 – 69
D: 50 – 59
E: 40 – 49
F: 0 – 39

Grading ya SASA (ACSEE – Current System)
A: 75 – 100
B: 65 – 74
C: 45 – 64
D: 35 – 44
E: 30 – 34
F: 0 – 29

4. UCHAMBUZI: KWANINI ACSEE YA SASA NI RAHISI KULIKO ZAMANI
(a) A-Level A Imeshushwa
Zamani: A ilianza 80
Sasa: A inaanzia 75

Mwanafunzi wa Physics au Mathematics aliyepata 76
Zamani: B
Sasa: A

Hii inaongeza idadi ya Division One bila kubadilisha ugumu wa mitihani.

(b) C na D Zimepanuliwa Sana
Zamani: C = 60–69
Sasa: C = 45–64

Hii inabeba wanafunzi wengi wa wastani kwenda juu zaidi.

5. MITIHANI NI ILE ILE, KINACHOBADILIKA NI GRADING
Ni muhimu kuelewa jambo hili Silabasi ni ile ile
Aina ya maswali ni ile ile
Kiwango cha ugumu kimebaki kile kile
Kilichobadilishwa ni mipaka ya alama (grading thresholds)
Hivyo, ufaulu wa sasa hauonyeshi moja kwa moja kuwa wanafunzi wa sasa wana akili au maarifa kuliko wa zamani, bali unaonesha mabadiliko ya mfumo wa upimaji.

6. MFANO HALISI: FORM SIX 2013 (TANZANIA NZIMA)
Mwaka 2013, matokeo ya ACSEE yalionesha hali halisi ya ugumu wa mfumo wa zamani:
Tanzania One (Division One ya juu kabisa)
👉 Mwanafunzi mmoja tu alifanikiwa kupata Division One ya pointi chache sana (mfano pointi 5) nchini kote.
Physics
👉 Hakukuwa na A hata moja ya Physics Tanzania nzima.

Hii haimaanishi wanafunzi walikuwa wajinga, bali
Grading ilikuwa kali
A ilikuwa ngumu sana
Mfumo ulipima tofauti ndogo sana za uwezo

🔹 Zamani ufaulu ulikuwa mgumu kwa sababu grading ilikuwa kali
🔹 Sasa ufaulu ni rahisi kwa sababu grading imelegezwa
🔹 Mitihani haijabadilika sana mfumo wa alama ndio umebadilika
🔹 Matokeo ya sasa yanaonekana mazuri, lakini hayalingani moja kwa moja na kiwango cha maarifa ya zamani
Kuhusu ACSEE Grading system umetuingiza chaka wembe ni ule ule A 100-80
 
Ambayo kwasasa ni A hiyo
Ufaulu kuongezeka kuna mambo mengi zaidi ya grading… miundombinu ya ujifunzaji imekuwa sana learning materials ziko kila mahali, idadi ya walimu imeimarika maradufu na idadi uelewa wa wazazi umekuwa mambo yanaenda mbele hayarudi nyuma kamwe
 
Basi kumbe ..mana Kuna binti mtaani mienendo yake kapiga div 1 , ila ndio mtaani anawaendesha mibaba, anakanyagwa na maboda, yan tunazuzuka na huyo binti , hela yako tu..ila ndio kapiga liwani
😄😄😄
 
Back
Top Bottom