Makala kwa wahitimu udom 2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makala kwa wahitimu udom 2011

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by JOMBAAA, Nov 26, 2011.

 1. JOMBAAA

  JOMBAAA Member

  #1
  Nov 26, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MAKALA KWA WAHITIMU UDOM MWAKA
  Ndugu watanzania wenzangu tunayofuraha kubwa kusema kuwa leo tarehe 26/11/2011 chuo kikuu cha Dodoma(UDOM) kimesherekea mahafari ya pili tangu kuanzishwa kwake mwaka 2007 na kutimiza takribani miaka ninne (04).Mimi binafsi ninayo furaha kubwa kwa kuhitimu shahada ya kwanza leo katika chuo hiki.
  Nomamba nitoe rai kwa wanafunzi walio baki chuo kuwa wayaendeleze yale yote mazuri tuliyoyaacha ikiwa ni pamoja na kusoma kwa bidii na kukinda amani ndani na nje ya chuo.Ndugu watanzania wenzangu nimeamua kundika makala hii katika mtandao huu wa kijamii kwa sababu kuu mbili.
  Kwanza;Kumekuwa na lawana nyingi ndani ya jamii kuwa baadhi ya wasomi hawatimizi wajibu wao katika kutumikia jamii na taifa kwa ujumla. Ni kweli , baadhi ya wasomi wamekana taaluma zao na kujiingiza katika siasa.Na siasa wazifanyazo ni siasa za chuki,dhuluma na uporaji wa mali za umma kwa maslahi binafsi.Ngudu wahitimu wenzangu natoa rai kwenu kuwa tumini jipya kwa watanzania wanaosubiri mchango wetu katika jamii.Ni aibu kubwa leo watanzania wanashuhudia kundi la wasomi wachache wakinufaika kwa kujitwalia mali za umma kwa maslahi binafsi.Wewe kama msomi ambae leo hii umehitimu shahada ya kwanza jamii inakusubiri na kukutegemea uwe chachu ya maendeleo ya taifa.Ngudu wasomi wenzangu jamii tunaishi inaelekea kupoteza imani juu ya mazao ya elimu na wasomi kwa ujumla. Inatupasa mimi na wewe turudishe imani hiyo kwa kuwa waadilifu,wapenda haki na usawa ili kurejesha heshima ya msomi katika jamii na kulinda uzalendo wa mtanzania..
  Pili; Naomba wasomi wasifuate siasa. Kwa mustakabali wa taifa hili sasa wasomi wengi wanaamini ati siasa ndio tiba dhidi ya umaskini. Hiz ni fikra potofu kwa msomi..Wewe kamna msomi mwenye taaluma ya juu katika sekta husika(ualimu.udaktari,uinjini​a n.k) nupaswi kuendesha siasa kama huna utashi wa kisiasa. Kufanya hivyo ni kuidhalilisha taaluma yako na kubaka taaluma ya mwenzako.Leo hii utakuta madaktari na mainjinia ndio wanasiasa wakati hawana hata uwezo wa kujenga hoja na kuzitetea.(hiyo sio siasa ni kubaka siasa).
  Nimetoa rai hii ya pili kwa wahitimu kwani leo hii tumehitimu hapa tupo katika fani mbalimbali, si vema kesho kusikia ati muhitimu wa fani ya biashara anafanya siasa tena za chuki,dhuluma na rushwa.Huu ni utumwa katika fani.
  Ngugu wahitimu wenzangu napenda kutoa rai kwa uongozi wa chuo kikuu cha Dodoma.Nimekuwa katika serikali ya wanafunzi kwa takribani miaka miwili, hivyo naufahamu vizuri uongozi wa serikali ya wanafunzi UDOM na menejimenti kwa ujumla.
  Rai yangu kwa uongozi wa chuo ni kwanba ni vema matatizo ya jumuiya ua chuo yatatuliwe na wana jumuiya wenyewe.(kati ya wanafunzi na menejimenti ya chuo). Kufanya hivyo kutaepusha kutoelewqana kati ya wanafunzi na menejinenti ya chuo na pia itajenga heshima ya chuo ndani na nje ya chuo na uongozi kwa ujumla.
  Si vema kutumia vyombo vya dola kama jeshi la polisi kutatua migogoro ya kitaalumal.Chuo kikuu ni mahali pa wasomi ebu tuyatatue matatizo yetu kisomi..
  Napenda kutoa shukrani zangi za dhati kwa aliyekuwa mnkuu wa chuo cha elimu na mwanzilishi wa chuo hicho, Mh.Prof.OSAKI kwa umakini wake pindi alipokuwa mkuu wa chuo hicho kwa busara zake dhidi ya kutatua migogoro baina ya mwanafunzi na menejimenti ya chuo.
  Ndugu wana chuo wenzangu nitakuwa mnafiki wa kutosema ukweli kama sitazungumzia juu ya ushiriki wa siasa chuo kikuu cha Dodoma. Kumekuwa na wmbi la wanasiasa wa nchi hii kufanya mikutano nje kidogo ya eneo la chuo kama makulu, Dodoma hotel na hata ng'ong'ona kijijini.Hili hufanywa na vyama vyote vya kisiasa hata chama tawala. Kwangu naona hii sio sahihi maana kumekuwa na utumiaji mbaya wa wanafunzi katika dimba la kisiasa kwa faida ya wanasiasa.Natoa rai kwa wanasiasa kuacha kuwatumia wanafunzi kwa lengo la kutimiza hazma zao za kisiasa.
  Ebu tuache wanafunzi wasome kisha waaingia katika siasa kwa utashi wao wenyewe na si kwa ushawishi.(HII SIO SIASA SAFI NA YA KWELI KAMWE KWA WATANZANIA).
  Mwisho ndugu wahitimu napenda kuzungumzia juu ya UZALENDO wa wasomi na watanzania kwa ujumla.Leo hii makundi ya watanzania katika rika mbalmabali wamejaa lawama juu ya ugumu wa maisha. Hii ni kwa sababu wale tuliowapa dhamana ya kuedesha taifa hili si wazaledo kamwe.Hivyo basi sis kama wasomi nigelipenda tuwe wazalendo na kutoa elimu juu ya UTAIFA kwa watanzani wote bila kujali wadhifa wa mtu. Nalisema hili kwa uchungu sana maana taifa sana limejaa wanyang'anyi.Hii ni kwa sababu mimi na wewe hatuna uzalendo katika taifa letu."Tanzania yenye kujali haki,usawa na kutokukubali dhuluma dhidi mali ya umma itajengwa na watanzania wazalendo"
  MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA
   
 2. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,146
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  udom mmejaribu mnasonga mbele ila ninashaka kama mmeweza.
   
 3. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,556
  Likes Received: 486
  Trophy Points: 180
  Umeandika mengi mazuri,nami pia nawapongeza sio wa Udom tu bali wote mliohitimu taaluma mbalimbali nchini.Naomba nitofautiane kidogo na wewe kuhusu siasa.Kwa mfumo wa nchi yetu siasa ndo inaamua kila kitu.Siasa inaamua elimu ya aina gani tupate,maisha yetu yaweje,mishahara,bei za bidhaa,nauli za usafiri,tuwe na bunge la namna gani,serikali na hata uongozi kuanzia serikali za mitaa mpaka serikali kuu!Kwa mtazamo wangu kuiacha siasa iende bila wewe au mimi kuwa sehemu yake ni kukubali kuwa wewe si chachu ya mabadiliko ya jamii yako.Mi nafikiri wasomi kazi yenu kubwa ni kuiletea maendeleo jamii yenu.Hayo maendeleo yanakuwa defined na siasa.Hapa kuna mawili,usitegemee mabadiliko kama siasa haipo vizuri.Mwalimu Nyerere alisema ili tuendelee tunahitaji watu,siasa safi na uongozi bora.Tanzania tupo hapa tulipo kwa kukosa siasa safi ambayo ingezaa uongozi bora.Tunawahitaji wasomi mtutoa hapa tupige hatua.Hamuwezi kukaa kando na kuacha kila kitu kiende chenyewe kwa kisingizio cha kutoshiriki siasa.Mtakuwa mmekwepa jukumu lenu la msingi sana.Jukumu la kubadilisha siasa hii chafu ni lenu na ni lazima mshiriki kutuletea siasa safi kama msingi mmoja wa maendeleo.Mambo ya muhimu kama katiba ya nchi yote yapo kwenye mfumo wa kisiasa.Sasa utapataje katiba mpya nzuri bila kuingia kwenye mfumo unaosimamia hiyo katiba?Kwa hiyo mi naona siasa haiepukiki ni lazima kuishiriki kwa namna yoyote ile.Pili kama mnaamua kustay away from siasa basi muwe na uhakika kuwa jamii yenu ambayo inawategemea haiumizwi kwa namna yoyote na jinsi siasa zinavyoenda.Sasa ni kweli kuwa siasa tuliyonayo inamfaidisha mnyonge?Hapana ni lazima kubadili siasa iwe safi something which is impossible without being a part of it...!
   
 4. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #4
  Nov 27, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  ni ngumu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kutohusika kwenye siasa kwa sababu ni watu wenye utashi hivyo hufanya maamuzi bila kulazimishwa. Ukisoma historia za wanamapinduzi wengi duniani kama chavez,castro, che guevara nk,wengi wao walianza wakiwa vyuoni. Pia kuwa che guevara alikuwa dactari lakini akageukia kwenye uanamapinduzi ili kuwakomboa wanyonge wanaonyonywa. Inaumiza sana unapokuwa doc halaf wagonjwa wanakufa kwa kukosa dawa,hakuna vitanda, mshahara mdogo wakati wengine wanalipana allowance 300000 kwa kikao.
   
 5. Ngaliba Dume

  Ngaliba Dume JF-Expert Member

  #5
  Nov 27, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,604
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Siasa ndo kila kitu...Mlacha kawaharibu nyie watoto
   
 6. F

  Fahari MJ JF-Expert Member

  #6
  Nov 27, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 425
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wamehitimu mafunzo ya siasa???????
   
 7. M

  Malyamungu JF-Expert Member

  #7
  Nov 27, 2011
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  basi kama siasa hazifai vyoni msingesoma political sayansi na economy. Infact politics is everythings tukiwa vyuoni twaangalia namna 'sociological imagination' vs 'collective forces' za watu wa jamii ile au wanasiasa the approach are being complied and how are being responded to assist the majority poor issues.
   
Loading...