Makala juu ya umoja katika muziki

Makala juu ya umoja katika muziki

isajorsergio

Platinum Member
Joined
Apr 22, 2018
Posts
4,143
Reaction score
6,562
Burudani ya muziki imekuwa chanzo cha kuleta faraja baina ya akili, mwili na roho kwa walio wengi. Muziki ni ajira kwa vijana, watoto na wazee. Muziki unaeleza zetu hisia, taswira, maono na unapaza sauti kupitia mirindimo na a'lra mbalimbali zikibebwa kwa sauti na mashairi yenye ladha.

Muziki amekuwapo enzi na enzi karne kwa karne, muziki umebadirika kwa vipindi tofauti na unazidi kubadirika kutokana na mtindo huru wa utayarishaji, uandishi, uimbaji, usambazaji na mapokeo katika jamii mbalimbali.

Wakongwe watakumbuka Folks, Salsa, Bolingo, Raggae, Bachata, Soul na aina nyingi za muziki huku watu wazima wakiitambua Hip-Hop, Pop, Taarab na Bongofleva. Kwetu vijana tukiwa tumesheheni shehena ya kila aina kama Raggaeton, Trap, Dance, Electro, House, Funk, Techno (EDM), Singeli, Afropop, Afrobongo, Gospel, Dancehall, Rnb na kila aina ya muziki unaoufahamu huku tukizidi kutafakari na kuongeza aina nyingine mpya.

Muziki ni kiunganishi na kielelezo baina ya wengi. Muziki unayo nguvu ya asili, nguvu zenye uzito usiofichika wala pimika iwe kwa mtoto hadi mzee, uzao mpaka kifo. 'Ukisikika mdundo, a'lra na sauti sharti utikise kichwa' haina mfano sote twafahamu fika ni utamu upi hufikia ubongo.

Waimbaji na watayarishaji wenye kuleta bidhaa ya mwisho sokoni iwe wimbo au nyimbo wanastahili pongezi na heshima kila mtu kwa nafasi yake. Uwe mtayarishaji ' Produkte, Composer ', mpiga gitaa ' Guitarist ' mpiga kinanda ' Pianist, Keyboardist ' muimbaji ' Singer ' kati ya wote wenye kuleta matokeo heshima ibaki kwenu. Hata Record labels, Management's, Promoters, Platforms, Publishing houses, Video Directors na Media michango yenu ni yenye thamani na yenye kuleta raha, furaha, kutukumbusha zetu hisia, maono pia na ajira kutupatia.

Katika historia na somo la muzikia tunaambiwa hapo zamani Tanzania record labels na publishing houses zilihesabika huku wengi wakitaja Bongo Records na MJ Records lakini hivi sasa wengi wanashuhudia uwepo wa Combination Sound, WCB, Switch Music, Pluto Music, King's Music, Tongwe Records, Touchez Sound, Looftop na nyingine kadha wa kadha. Kutoka bara Europa, Amerika kaskazini, Asia, Afrika, Australasia, Latin na Amerika kusini wengi unganishwa na Warner Bros Music, Universal Music Group (UMG) na Sony Music Entertainment (SME) wenye umiliki mkubwa wa record labels nyingi duniani.

Huku zikiwepo nyingine nyingi zilizoanzishwa mwanzoni wa miaka ya 2000's baadhi ya record labels, publishing houses na management hizo ni kama Magnus iliyo chini ya Marc Anthony huku ikiwa na shehena za vipaji Kama Gente de Zona!. Hear This Music ni label nyingine inayokuwa kwa kasi aliyoasisiwa na producers nguli DJ Luian na Mambokingz huku ikimtambulisha Bad Bunny katika ulimwengu wa muziki, ikumbukwe Bad Bunny alikuwa akifanya vibarua katika migahawa na garage mbalimbali ndani ya viunga vya San Juan, Puerto Rico. Hivi sasa Bad Bunny ameondokana na ukata na maisha duni na anautafuta ukwasi, hili ni funzo kwetu sote ya kwamba tupambane bila kukata tamaa maana muda wowote mabadiliko yanakuja.

Kwa Afrika Mashariki na kati, Harmonize anavaa ufanano wa Bad Bunny kwa Latin na Amerika ya kusini. Tukimtafuta producer aliyeleta mabadiliko ndani ya miaka minne hutosita kumtaja kijana Sky Rompiendo 'El Bajo' mzaliwa wa jiji la Medellin, Colombia akifanya kazi zake San Juan na Miami. Sky ameanda nyimbo nyingi na asilimia 97 tunaweza kusema ni ' Hit Songs ' Sky (23) anao mkono katika mafanikio ya J Balvin na J Balvin kupitia sauti amemungoza Sky katika safari ya maisha yake, Sky Rompiendo 'El Bajo' amefanya kazi nyingi na baadhi ya kazi hizo ni Kama ifuatavyo:-

• J Balvin - Reggaeton
• Zion y Lennox Ft. J Balvin - No es junto
• De La Ghetto Ft. J Balvin - Caliente
• Nicky Jam Ft. J Balvin - X (Equis)
• Nicky Jam Ft. J Balvin, Ozuna & Maluma - X (Equis)
• Joel & Randy Ft. J Balvin - Bonita
• J Balvin Ft. Pharrell William, BIA & Sky - Safari
• Zion y Lennox Ft. J Balvin - Otra vez
• J Balvin - Bobo
• J Balvin Ft. Daddy Yankee - Pierde los modales

Hiyo inadhihirisha fika kijana anao mchango mkubwa katika muziki na mahadhi ya Reggaeton.
Katika mahojiano na mazungumzo na Sky alinitaarifu ya kuwa tuyaonayo nje sio sawa na ndani, kuna Inner na Outer!
"Nisingelikuwa Sky Rompiendo bila wenzangu, naweza kusema neno moja 'Umoja' na kulikana neno moja 'Umimi' sote tuyakumbuke haya" - Sky

Na kuzidi kuniambia muziki hasa hasa Reggaeton isingelikuwa hivi bila ushirikiano baina ya waimbaji, wasanii na third parties.
Maana usikiapo Maluma - 11:11 au HP, Yandel - Te Amare, Zion y Lennox - Hipnosis, Becky G Ft. Bad Bunny - Mayores, Justin Quiles - Cristina, Daddy Yankee - Dura, Luis Fonsi Ft. Daddy Yankee - Despacito, Natti Natasha - Me gusta! Au Nicky Jam - El ganador na nyingine nyingi.

Basi umoja ndio unaopeleka muziki mbele, sio ajabu kuwakuta Saga Whiteblack, Chris Jeday, Tainy, Sky Rompiendo, Kenedy, J Quiles, Mambokingz, DJ Luian, Gabri Music, Rvssian, A&X na Pharrell wakiwa studio El Orfanato, La Industria Inc., Hear This Music au Dimelo V wakishirikiana kuanda muziki.

"Tuna udhaifu katika mambo baadhi, ili upate kitu bora ni vyema kushirikiana na wengine mfiche yenu madhaifu" - Sky
Jambo limethibitika kwa watayarishaji wengi wa kiafrika hasa ukanda wa mashariki na kati.

Producer, Actor na Muandishi nguli Red One kutoka Morocco, Afrika alinukiliwa na Billboard akisema "Umoja kwa wasanii wa Afrika ni dhaifu na wa kinafiki. Umimi na kutopendana na tusipo badiri hilo hatufiki popote." - Red One

Tukitazama kwa upande Tanzania utaona maana ya umoja ni umimi, wasanii wengi wanacheka usoni katika mioyo yao wakikataa mjumuiko. Katika wasanii, ma-director na watangazaji pamoja na media wanashindana wao kwa wao ilhali ilitakiwa washindane wao na wale wa nje.

Producers wengi wameshindwa kuungana kuleta vitu tofauti, ku nani?! Heshima iende kwako S2Kizzy umejitoa na kuungana na watayarishaji wengine kama Layzer kuleta burudani, usisite wala kukata tamaa endelea mbele kwa mbele na karibuni utafika kuwa Produkte wa kimataifa.

Rejelea wasanii nguli wa kiafrika walio liwakirisha bara nje ya mipaka ya Afrika, wameanza kurejea Afrika na kusaidia makwao. Tutaona Mohombi, Red One na Akon wakirudi Afrika kusaidia na kusupport. Hivyo basi sote tuungane na kushirkiana katika kuendeleza muziki bila kuchoka.

Heshima kwenu mliotangaza vyema bara la Afrika. Heshima ikufikie Nahreel, Diamond Platinumz, Davido, AY, Wizkid Ayo, Black Coffee, Navio, Wyre, Sarkodie, Nasty C, Mr Eazi, Vanessa Mdee, Alikiba, DJ Arafat, Lartiste, Abou Debeing, Justin Campos, iCandi Cam, Hascana, Sauti Sol, Fally Ipupa, C4 Pedro, Masterkraft, DJ Hamida, Awa Imani, Late* Bi Kidude, Peter and Paul Okoye, J Martins, Godfather Production, Sasha Vybe, Clarence Peters, Patoranking, DJ Bucks, Uhuru na wengine wengi.

Unity = Wealthy
-
Enquires na press Kwa uchambuzi na uandaaji wa makala za (Burudani, Michezo, Muziki, Sanaa, Video, Ubunifu na Mitindo) kupitia:-
sajorsergio@we-play.cc
(Europe, Australasia na North America)
sajorsergiosjanic@gmail.com
(Africa, Latin and South America)
isajorsergio@gmail.com
(Asia na Ocenea)
Freelance works/jobs
isajorsergio@gmail.com
 
Tatizo la wanamuziki wa Afrika kutosaidiana ni nini sijui,mbona wenzetu wanaweza?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijaelewa tatizo nini lakini ukifuatilia kwa makini utaona vijana 95 to 20s wanajaribu kushikana kuliko wala miaka ya nyuma.

All in all bado kuna umimi na ubinafsi. Nashangaa watu wasiopenda kusaidia wenzao kwa kigezo watafanikiwa.
 
Back
Top Bottom