Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
KUPIGWA, kubakwa na msururu wa wanaume bila kupata chochote ni baadhi tu ya madhila yanayowakumba wasichana na wanawake wanaofanya biashara ya ukahaba katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, ambako kelele nyingi zimepigwa kuhakikisha biashara hiyo inakomeshwa.
Kutokana na kelele hizo, tayari Serikali imetangaza kampeni ya kuwakamata makahaba wote pamoja na wateja wao, zoezi ambalo baadhi ya wadadisi wamesema halitafanikiwa kwa sababu mnyororo wake ni mrefu.
Uchunguzi wa FikraPevu umebaini kuwa ukahaba ambao umekuwepo kwa miaka mingi duniani, siyo suala la kukamata watu mara moja na kuwaweka ndani, bali unatakiwa kutafuta kiini chake na kutafuta ufumbuzi badala ya kutumia nguvu.
SOMA ZAIDI...