Makada 13 wa CCM Arusha kumrithi Sanare uenyekiti wa CCM Mkoa

jembejembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
572
1,000
Makada wapatao 13 wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Arusha,wamejitosa kuchukua fomu kwa ajili ya kuwania nafasi ya mwenyekiti wa ccm mkoa iliyoachwa wazi na aliyekuwa mwenyekiti wake Loota Sanare ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Morogoro.

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Katibu wa CCM mkoani humo, Musa Matoroka amesema zoezi hilo la uchukuaji wa fomu limeanza rasimi jana Novemba 25 mwaka huu na linatarajia kumalizika kesho Novemba 27 saa kumi jioni.

Amesema hadi kufikia leo Novemba 26 majira ya saa sita mchana wanachama wapatao 13 walikuwa wamejitokeza kuchukua fomu kuwania nafasi hiyo ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha.

Aidha Matoroka amebainisha kuwa utaratibu wa chama hicho baada ya zoezi hilo la uchukuaji wa fomu kukamilika watafanya upembuzi yakinifu majina hayo na kisha kuyatuma makao makuu ya CCM na kwamba majina matatu pekee ndio yatarejea kwa ajili ya kupigiwa kura siku itakayopangwa.

Hivyo aliwataka wanachama na wakereketwa wa CCM kukaa mkao wa kula wakati mchakato wa kupata Mwenyekiti wa CCM mkoa ukifanyika.

images%20(2).jpeg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom