Makaburu wateka Burka Arusha - NNAUYE Jr vipi ongea kwa hili

Ni kweli kabisa, Arusha ina makaburu na watu wa mataifa mengine wengi kuliko mikoa mingine ya Tanzania.....utaona wengine wanazurura mitaani kama waswahili wengine.....
Labda wawe wamemilikishwa ardhi kwa ajili ya uwekezaji kupitia TIC (derivative right) vinginevyo ni kosa kwa mtu ambaye si raia wa nchi hii kumilikishwa ardhi.........

Lakini makaburu wengi wametumia ujanja wa kuoa waswahili......wengi wameoa mabinti wa akina Laizer, Mollel, Sarakikya, Mushi etc.......

Ukiangalia kwa undani.....wengi wamepewa maeneo kwa ajili ya uwekezaji......lakini hawajawekeza kitu......sasa nashangaa hizo certificate of incentive za TIC zinakaguliwa????? maana inatakiwa wawe wameandaa project progress report......kila baada ya miaka 3 na kuipeleka TIC na TIC wana wajibu wa kukagua miradi katika ardhi hizo (za wawekezaji) kama yanaendana na kile kilichoko kwenye miradi hiyo... lakini sidhani kama hicho kinafanyika......
 
KOBA.....Usifanye mchezo whether wananchi hawaelewi au wanaelewa ukweli ni kwamba hawana ardhi, na wanaona ardhi nyingi nzuri inachukuliwa na wazungu. na pia kwa msaada kwa watanzania wenzako weka hizo sheria apa.
ishue ingine watanzania tusing'ang'ane na sehemu moja kuna ardhi ipo tena bei karibu na bure apo apo arusha nje kidogo ya mji. chakarika utapata kwa ajili ya kujihifadhi huku tukiendelea na mapambano.
but muhimu ni kuendelea kupambana kwa ajili ya wanetu.
 
Nimemsikia Kikwete juzi Afrika kusini akisifia ujio wa Makaburu zaidi ya 170 nchini Tanzania na mchango wao katika uwekezaji.
 
Muulizeni Mkulu mtaona majibu yake....mnakumbuka Chiligati kuhusu Kigamboni? nanukuu...tumechoshwa na watu wanaobeba mfuko mmoja wa simenti kwenda kujenga...Tuwape wenye uwezo....Mkulu alisema, wanasema eti nimempa rafiki yangu Bush kigamboni...akatabasam...bongo sold.
 
sio upande wa maua bali halmashauri imeshatangaza kuuza viwanja lakini bei yake hakuna mtanzania wa kawaida ataweza kununua hata wameru wanaozunguka eneo hilo.
hakyanane Wameru hatuna chetu! Mwaka huu cjui tutakata migomba tena au! Mimi naona tuwakate wavamizi na siyo migomba maana tunaonekana majuha!
 

kilimo cha maua, wizi mtupu. Sumu kwa mapafu ya wafanyakazi. Mshahara mdogo. Kodi wanakwepa.

Bora wagawiwe wananchi walime mboga na matunda
 
Kinacho shangaza ni kwamba sheria yetu hairuhusu raia wa kigeni kumiliki ardhi lakini ukweli ni kwamba wageni wanaomiliki ardhi kwa sasa ni wengi kuliko maelezo, sio Burka tu kwa Arusha bali hata Usa River/Maji ya chai.. hivi hii serikali ipo kweli au hua inajionyesha tu kwenye chaguzi kuilinda ccm kwa kuonea wananchi?
 

Umeonaeeeh?
 
Mkuu Nape achana na hawa viwavi wa cdm huna cha kujibu kwenye hii thread
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…