Makaburu wateka Burka Arusha - NNAUYE Jr vipi ongea kwa hili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makaburu wateka Burka Arusha - NNAUYE Jr vipi ongea kwa hili

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MPadmire, Jul 16, 2011.

 1. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,636
  Likes Received: 906
  Trophy Points: 280
  Vile viwanja kule burka vilivyoleta Mushkeri, maeneo hayo hayo Makaburu wameanzisha kijiji chao.

  Kuna eneo kubwa sana kama vijiji viwili hivi, makaburu wamepewa viwanja na wamejenga. Hebu mswahili sogelea ardhi uone.

  Hivi ni kwa nini Mtanzania akitaka ardhi hawezi kupewa??

  Kwani Zamani wazee wetu walipataje Ardhi??

  Kuna utaratibu gani kwa watanzania wasio na ardhi kupata ardhi ya kuishi (residential) au kulima.

  Kama vijana wanazurura mijini kama wamachinga, watapata wapi ardhi ya kulima au makazi.

  Dawa ni kuwaunganisha wamachinga na kuvamia wageni waliopewa maana viongozi wanawauza wananchi ndani ya nchi yao.
   
 2. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mkuu! Ingewezeka hilo zoezi la Uvamizi lingeanza mapema iwezekanavyo,Mi cjui ni lini Watanzania wataenda pale South Africa wakapate kumiliki ardhi kirahisi hivyo. Mpadmire thread yako ni nzuri na ngoja 2wasubirie washikaji.
   
 3. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  pesa mbele utu nyuma
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
 5. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,636
  Likes Received: 906
  Trophy Points: 280
  Asante Bwana Saint Ivuga na MTN.

  Kweli nchi SOLD na watanzania bado tunateseka na bidhaa zetu mkononi tunatembeza (machingas).

  Amini huwezi kwenda Kenya au Africa kusini ukamiliki Ardhi kwa dola 10000 tu, very cheap. They got big land for only 10,000 US $ only. Hata kupata kazi tu Africa kusini au kenya sembuse ardhi !!! Huu mchezo mchafu umechezwa na madiwani wa ccm, maafisa ardhi na hata wakuu wa wilaya na mkoa. Usalama wa taifa uko wapi.
  Usalama wa taifa unajua kuwa hawa vijana wasio na kazi watahatarisha usalama??? Unajua mtu aliye na njaa yupo tayari kufanya lolote?

  Usalama wa taifa mnajua kuwa vijana wako tayari?

  Hivi wazee wa zamani yaani baba zetu na babu zetu walinunua ardhi au walipewa? Mie najua kila kijana aliyetaka kulima au kufuga aligaiwa ardhi na akaaza kulima. Ndo maana tunawakulima wadogo wadogo huko vijijini. Na ndio watu wengi walikulia huko, wakasoma ndo tukaja mjini. siku hizi kijana anamaliza shule, kama hajabahatika kupelekwa secondari anakuwa hana kazi. Anakuja mjini kupiga umachinga, kwa sababu hana ardhi ya kulima.

  Na ndo hizo ardhi tunagombea kati ya koo na koo wakati ardhi zenye rutuba wanapewa wadekezwaji (WAWEKEZAJI).

  Hizo taasisi kama Kituo cha sheria na haki za binadamu au Haki ardhi wanafanya nini.

  Kwanini hatujiulizi wamachinga wanatokea wapi?? Hapo mwaka 1994 ndo mara yangu ya kwanza kwenda mjini,, mbona kulikuwa hakuna machinga? labda Dar kidogo ila kulikuwa na maduka tu. Sasa hivi kila mji una wamachinga
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Hii k itu inahitajika kufanyika mapema sana ama laa soon ardhi yetu itakuwa kama sauzi, ardhi yetu ni urithi wetu na si wa hawa viongozi wachache walafi, tuiinde nchi yetu jamani
   
 7. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Sio burka tu subiri na tengeru!
   
 8. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #8
  Jul 16, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Dahh! Hapo Tengeru wameshafinya tena? Ama unasemeya upande wa maua.
   
 9. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  sio upande wa maua bali halmashauri imeshatangaza kuuza viwanja lakini bei yake hakuna mtanzania wa kawaida ataweza kununua hata wameru wanaozunguka eneo hilo.
   
 10. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Swali zuri na zito; naamini hata Raisi wetu hawezi kulijibu. Wengi wetu tumekatiwa vipande vya Ardhi na Wazazi wetu lakini hakuna anayefahamu yeye aliipataje. Nikichukulia uchagani (ukanda wa chini) yale mashamba yalikuwa ni ya katani, vingozi wa jadi (wachili waliokuwa wasaidizi wa mangi) walikabidhiwa na kusimamia ugawaji wake. Kwa wakati ule wengi wa wachaga hawakutaka kuja kuishi ukanda wa chini (kasa) hivyo ugawaji haukuwa wa kugombania kama ilivyo sasa. Bahati mbaya sana wale waliokataa kuchukua/kuhamia ukanda wa chini leo hii ndio maskini wa kutupwa ukilinganisha na wachaga wenye mashamba ukanda wa chini (kasa). Hata hivyo, kutokana na uhaba wa ardhi ukanda wa juu, leo hii wachaga wanaishi kila kona (wamisionari wa kitanzania) ya Tanzania na wamekuwa waleta maendeleo kila walipohamia.
   
 11. s

  seniorita JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  watumwa ndani ya nchi yetu=jsmsni tukubali kweli kutawaliwa? Wakati mwingine I salute Mugabe- Serikali yetu imetuuza kwenye utumwa
   
 12. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #12
  Jul 17, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,636
  Likes Received: 906
  Trophy Points: 280
  Enheeee,

  Ardhi ipo hapo kwa ajili ya vizazi vya watanzania.

  Tengeru ni millioni 8 mpaka kumi na ukubwa wa shamba ni mdogo. Hakuna mtu anaweza kulima hapo na kupata faida. Ila cha kushangaza akija muwekezaji anapewa heka 500 bure. Eti analipa kodi ya shs 1000 kila mwaka.

  Sasa kwa nini mtanzania mzawa asipewe kiasi ambacho anaweza kulima kama heka 5 hadi kumi na akalipa elfu kumi kwa mwaka?

  Mwekezaji atalima mibono au maua na atauza nje na faida itaenda nchini mwake. Ila mtanzania akilima mboga mboga, matunda na maharage atauzia mahoteli na uchumi utabaki Tanzania. Pia utakuwa umeondoa wamachinga mjini na vijana watakuwa na ajira.

  Eti utasikia kiongozi anasema hajui kwa nini Tanzania ni masikini??? Eee eti nini Nguvu kazi inapotelea mjini (vijana wanakuwa wamachinga na wapiga debe) wakati tunanunua mboga na matunda kutoka South Africa na Egypt. Tunapoteza pesa za kigeni na shilingi inaporomoka.

  Hawa vijana wangepewa ardhi wakalima mboga na matunda na tungeuza kwenye migodi, mahoteli, na ku export.

  Nape NNAUYE yeye hata siku moja hawezi kuongelea hili, akawaokoa vijana wenzake. Yeye Nape kazi yake kushambulia wazalendo tu wanaoelimisha watanzania. Nape kemea basi hata madawa ya kulevya basi kama Marehemu Amina CHifupa. Nape wewe ni fisadi kwa sababu hukemei mafisadi au wauza madawa, bali unapambana na wazalendo wanapigana na ufisadi.

  Jamani tuseme basi, tuanzishe 'movement' au campaign ya kupinga ardhi kuchezewa. Tupige keleke kwenye magazeti na bungeni ili liwe janga la kitaifa.

  Jamani wamachinga ni janga la kitaifa, amani ya nchi itatoweka kama ufisadi wa ardhi utaendelea hivi. Mfano wamachinga Mwanza wananyanyaswa sana, wakati madini yanachukuliwa. Wamachinga hawa wangewezeshwa, wakalima mazao na wakatautiwa masoko.

  Hata ukilima mahindi tu yanasoko Kenya, Uganda, Somalia, Sudani

  Ardhi yetu Tanzania????

  Ardhi ya makaburu au wakulima wa maua??
   
 13. Ghost

  Ghost JF-Expert Member

  #13
  Jul 17, 2011
  Joined: Apr 20, 2010
  Messages: 429
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Aisee mkuu inaonekana unaumia kweli....
   
 14. Makoye Matale

  Makoye Matale JF-Expert Member

  #14
  Jul 17, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 6,480
  Likes Received: 450
  Trophy Points: 180
  Wakuu, suala la ardhi ni nyeti ajabu. Hivi sasa tuna eneo linalofaa kwa kilimo hekta milioni 44 (source: Ministry of Agriculture), Watanzania tuko kama milioni 44 hivyo kwa uwiano sawa hakuna Mtanzania atakaye kuwa na ardhi zaidi ya hekta 1 sawa na ekari 2.5 tu! Kila mmoja ajiulize anamiliki ekari ngapi? Kama una zaidi ya ekari 2.5 uko upande salama. Tafakari, chukua hatua!
   
 15. pisces

  pisces JF-Expert Member

  #15
  Jul 18, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 225
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  next time tutumie kura zetu wisely.... Siasa sio soccer.
   
 16. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #16
  Jul 19, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,636
  Likes Received: 906
  Trophy Points: 280
  Heeeee Wanajivua magamba ili 2015 watuchakachue tena. Wanaanza propaganda zao za kuwalaghai watanzania.

  Kwa kweli hili la ardhi ni nyeti mno na kuwaacha vijana kuwa wamachinga, changudoa na wapiga debe ni JANGA LA TAIFA. Ni bomu linalosuri kulipuka.

  Kwa kweli wana JF point tulizojadili hapa zinatakiwa ziingizwe na zijadiliwe na Wizara kivuli ya Ardhi na Makazi (Mh. Halima Mdee) na Wizara ya Kilimo na Chakula, pia Wizara ya Kazi, Ajira na Vijana.

  Pia wanaharakati wapige kelele kwenye hili.

  Nashauri siku ya Budget wizara ya ardhi tuandae vipeperushi au maandamano kwa jambo la ardhi
   
 17. Sijali

  Sijali JF-Expert Member

  #17
  Jul 20, 2011
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 2,062
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Tatizo siyo ardhi inauzwa kwa wageni, inauzwa bei ndogo sana! Ulimbukeni, mazeuzeu ya macho na upumbavu. Kweli wajinga ndio waliwao.
  Ikishauzwa tu, sahau kuwa mnaweza kuipata bila ya kutoa damu. kwanza kanuni za sasa za utandawazi zinamdhamini mwekezaji na hata anaweza kufungua mashataka kwenye mahakam za Kimataifa!
   
 18. K

  Koba JF-Expert Member

  #18
  Jul 20, 2011
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  yaani ukisoma mawazo ya wengi humu unasikitika sana,sijui hata kama mnaelewa utaratibu wa ardhi au ni ushabiki tuu? pls pls kabla ya kuja kutoa moshi wenu humu jaribuni kufanya research kidogo tuu mjue utaratibu na sheria zilizotumika kuwauzia ardhi hao watu,acheni fearmongering zenu as if nchi kama ndio imeshauzwa vile,yaani debate nzima imejaa story za mtaani tuu zisizo na ukweli wowote...sick sick sick!!!
   
 19. k

  keinyo Member

  #19
  Jul 20, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  koba mbona unataka kutetea uozo unaofanywa viongozi wako.kama vimeuzww kwq utaratibu kwa nn wtnzania wabaniwe or ndo couz of small captal but remember that one of da policy of our country is t adress equality and eqity
   
 20. M

  Mzee2000 JF-Expert Member

  #20
  Jul 21, 2011
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 491
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Tanzania ya kikwete imeoza sijui mtu uanzie wapi.lakini ndio hivyo labda upole wetu unatuponza huu ndio wakati wa kuchukua sheria mkononi.
   
Loading...