Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Fedha hizo ni makusanyo ya mpaka tarehe 19 Mei, 2025 wakitarajiwa kuvuka lengo la fedha walilopangiwa la Shilingi Bilioni 33.15.
Akizungumza na wanahabari wa Tume ya Madini, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Alphonce Bikulamchi amesema, hadi mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu Mkoa huo utakuwa umevuka lengo la zaidi ya asilimia 100 ya ukusanyaji mapato.
Aidha, amesema pia Mkoa huo mbali na makaa ya mawe pia umebarikiwa kuwa na aina nyingi za madini ikiwemo Dhahabu, Shaba, Chuma, Urani, Madini ya Ujenzi na Madini ya Vito.
Amesema pia kuna masoko mawili ya madini ambayo ni Soko la Madini Songea na Soko la Madini Tunduru ambayo yalianzishwa na Serikali kupitia Tume ya Madini ili kuongeza uwazi, usawa, ulinzi wa haki halali na maslahi ya watu wanaofanya biashara hiyo huku akiwataka watanzania kuchangamkia fursa mbalimbali zilizopo mkoani humo kama usambazaji wa teknolojia zinazotumika migodini, usambazaji wa bidhaa za vyakula, uchimbaji, uchenjuaji na biashara ya madini.