Majuto ni mjukuu.

mrregion

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2018
Posts
464
Reaction score
544
Habari za leo wakuu.
Nikiwa sekondari mwaka 2008 kidato cha 4 nilikuwa na rafiki yangu kipenzi na ambae tulikubaliana kuishi wote hapo baadae, Mungu bariki tulifauru wote na kuanza kidato cha tano 2009 na 2011 tulimaliza na 2011 tuliacha masomo ya chuo kikuu.

Vyuo tulisoma tofauti na tulipendana sana kwa kutembeleana lakini mwaka 2014 baada ya masoma ya shahada ya kwanza mwenzangu alipata ajira kabla hata hatujawasilisha andiko hivyo akawa na ajira nami nikawa natafuta ajira.

Bahati mbaya kwangu nilisota mtaani kwa mwaka mzima sina kazi na mwenzangu akawa mbali nami na dharau zikaanza na Mipango yetu ilikuwa 2018 tutafunga pingu za maisha(ndoa).

Nilipopata ajira hakuonyesha kufrahi ila sikupata shida sana kwa kujifariji kuwa maandiko yanasema tuishi nao kwa akili ngoja niwe mvumilivu. Nilianza taratibu za kupeleka posa na mahali mwaka 2017 nikamshirikisha akasema sawa.

Nilipeleka posa na mahali tarehe 27/12/2017 lakini harusi tulipanga tufunge mwezi wa 10 akawa analzimisha iwe mapema zaidi nikasema kuwa harusi ni jambo la baraka why tulikimbize hivyo? Lakini binafsi nafsi yangu iligoma kabisa thanks God nilisikiliza sauti iliyosema subiria.

Tarehe 2.4.2018 nilitumiwa message na mpenzi wangu kuwa ana mtoto sikuamini ila nikampigia mdogo wake akasema kweli. Baadae nikifunga safari kwenda Arusha kushuhudia kama kweli, hakika niliona uhalisia, nilimuuliza L nani baba wa huyu mtoto akasema wewe nikasema mara ya mwisho tulikutana lini akasema nikamwambia kama mtoto wa kwangu nadhani angekuwa chumba cha joto na si vinginevyo akasema kama huamini niache ntamlea mwanangu nikasema OK.

Sikukaa sana nikaondoka kurudi ninakofanyia kazi maana nilivurugwa akili kwa kupotezewa mda.

Najuta why nimepoteza mda wangu kiasi chote hicho? Je wanawake mnamatatizo gani? Leo hii naanza kutafuta msichana wa kuoa mwingine nikiwa stressed.


Funzo kuna haja sasa kutafuta wapenzi zaidi ya 2 ili nikiamua kuoa nichague kwa vigezo na si vinginevyo.

Mwakani afe kipa afe refa nahitaja kuwa na mke wa ndoa.

Wadada karibuni ila uwe unajielewa na mwenye heshima na hofu ya Mungu. Sifa kuu usiwe unatumia pombe na usiwe kabila la Mrangi na uwe mkiristo dhehebu lolote la kusali jumapili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Its good to have options kwa kweli maana, mambo ni mengi mda ni mchache
 
Hata ungetafuta watano uchague wanawake ni wale wale kibaya zaidi umehamia kwa wamtandao ya kijamii utachanganyikiwa zaidi.......vijana mliozaliwa miaka ya 90s maisha ya ndoa yanawasumbua hapa mtaa wa jilani moja alijinyonga kisa kamkuta demu wake na kondom za kiume kwenye mkoba wake wakati wenyewe hawatumiagi hizo kondom siku nyingi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akajinyonga ili kumpa nafasi ya kuzitumia vizuri hizo condom

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Seems to me umemkataa mwanao. How Sad.

You know why? Ulipeleka posa na magari na bado ulikuwa unamkula.

Alitaka harusi iwe mapema ili asitirike na aibu ya kuzaa nje ya ndoa. Sauti uliyosikia sio ya Mungu. No za devil alitaka uvuruge mambo na amefanikiwa.

Mdada amekuwa so disappointed so ameamua atalea mtoto pekee yake.
 
Haaa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hiyo akili huwa ya kijinga sana kujiua bora muachane tu,
mbona 1 akifariki hakuna anayesema tuzikwe wote kwasababu tulikuwa tunapendana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mambo ya ajabu sana

Nianze tu kujitanguliza niache puchi inavonoga bhaaah!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…