Majuto ni mjukuu, gharama za kupima

Majuto ni mjukuu, gharama za kupima

Charliemic

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2019
Posts
604
Reaction score
979
Wakubwa na wadogo nawasalimuni nyote.

Nijikite kwenye mada.

Nimeona nyuzi zimejitokeza hapa jukwaani kuhusiana na HIV/ AIDS. Tusiwahukumu wala kuwanyanyapaa walioupata!! Ni gonjwa linaloweza kumpata mtu yeyote, usione kuwa walioupata ni wadhambi saaana.

Wanajamvi, huu ugonjwa upo na unasambaa kwa kasi. Kimasihara unaweza ukaukwaa. Hakuna formula maana wapo walioukwaa kwa tendo moja tu!

Gharama za kupima kabla ya sex ni ndogo kuliko kutokupima. Ni bora kupima maana usipopima utaishia kuwa mwenye mawazo mengi mnooo! Siku hizi vipimo vipo kila mahala hata kwenye vituo vidogo vya afya.

Mwaka 2016 kuna manzi nilimla asubuhi yake washkaji wakanitonya ana moto, nikaenda naye kupima, kweli ana umeme! Pona yangu nilipewa PEP, nikatumia baada ya miezi 6 ndio nilipima nikawa negative. Niliacha umalaya rasmi tokea hapo!!
 
Acheni kuleta thread za kutishatisha, huyu Priscallia ndio wa kulaumiwa hapa
Hakuna kutishana mkuu,ni bora utishwe itasaidia wengi kuliko wachache walioamua kujilipua,usifikirie wewe tu fikiria na kaka zako,dada zako,mama zako,shangazi zako,mabinamu,ndugu,marafiki,watoto wako n.k.ugonjwa upo na takwimu tutakazopewa tarehe 1 December zitakuwa ni za kutisha kwani maambukizi yanongezeka kwa kasi hasa kwa vijana ambao ni taifa la kesho.Ukumbuke pia kuwa serikali inabeba mzigo mkubwa sana kwa hizi dawa kwani inazitoa bure kwa waathirika.Kifupi ni kubadili tabia,dawa ni kuachana na ngono zembe,tumrudie Mungu wetu,hata hizo tamaa za zinaa unazofikiri huwezi kuziepuka anaweza kukuepusha nazo kama utakuwa serious kuhitaji msaada wake...
 
Vijana tuwe makini na tujilinde, ukipima unakua huru na makini zaidi. Starehe ya mda mfupi inaweza katisha ndoto za maisha yako yote japo kupata ukimwi sio mwisho wa maisha kama ukifata utaratibu sahihi
 
inabidi tuwe makini sana na nyie kina kaka muache kutufata PM
 
Back
Top Bottom