Kuna jambo limenishtua hivi karibuni nalo ni utenguaji wa nyadhifa ambazo rais hapo awali aliteua, mkuu wa mkoa wa Mara na wale wakuu wa wilaya wawili Fikiri Avias Said pamoja na Emile Ntakamulenga nimejiuliza iweje rais mwenyewe ateue watu hao baada ya kipindi kifupi tu awatengue, kitu nilichogundua hapa huenda rais anapelekewa taarifa na watu wake na kuzifanyia kazi pasipo kutumia muda kidogo kuzichunguza kitu ambacho ni hatari zaidi maana huenda mleta taarifa anaweza kuwa na chuki binafsi na mteuliwa, kwa lugha nyepesi kabisa rais amekaribisha majungu na umbea katika utawala wake, kitu ambacho ni hatari maana kitafanya watu wasiwe na mamlaka kamili maeneo yao kazi na vile vile kuwa na nidhamu ya uoga.
Kipindi fulani mh rais mstaafu Kikwete aliwahi kusema alipelekewa majungu akamwajibisha mtu kumbe ulikuwa uongo je, ni wangapi watakaowajibishwa serikali hii kwa kuonewa kutokana na kupelekwa taarifa za uongo, majungu na umbea.
Mh rais atambue kuwa ukiruhusu majungu maeneo ya kazi utasababisha watu wasifanye kazi kwa uhuru zaidi lakini pia watu hao watakuwa waoga maana hawajui kesho yao.
Mh rais inampasa kutumia kuchunguza na kujiridhisha na tuhuma kabla ya kumwajibisha mtu na wakati mwingine akigundua tuhuma hizo ni za kweli kama hazihusiani na ubadhirifu atoe onyo kwa kiongozi huyo pasipo kumtumbua au kutengua nafasi yake
Mh rais atambue endapo mtangulizi wake angelifanya kazi kwa majungu leo hii asingelikuwa hapo zile tuhuma zilizokuwa zinamwandama kipindi kile angelitengua uteuzi wake.