Majukumu ya mke na mume ndoani

BM Pesambili

Senior Member
Jul 10, 2016
102
624
Kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kifungu cha 9, kinatoa tafsiri ya ndoa kuwa ni muunganiko wa hiari kati ya mwanaume na mwanamke unaokusudiwa kudumu kwa muda wa maisha yao yote.

Ndoa ni haja ya kawaida kwa kila mwanadamu. Ndoa ndio njia pekee ya kujenga familia, ndoa ndio njia halali ambayo binadamu yeyote anaruhusiwa kutimiza haja zake kimwili tofauti na hapo.... Kwani Mwanaume ameubwa kwa ajili ya mwanamke hali kadhalika mwanamke ameubwa kwa ajili ya mwanaume "Bwana Mungu akasema si vema huyu mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye, Bwana Mungu akamletea Adam usingizi, naye akalala; kisha akatwaa ubavu mmoja, akafunika nyama mahali pake, na ule ubavu alioutwaa katika Adam Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adam; kwa hiyo mwanaume atamwacha baba yake na mama yake ataambatana na mkewe na watakuwa kitu kimoja (Mwanzo 2:18.....24)

Lakini kwa sasa hakuna suala gumu, tata na nyeti linalohusu maisha ya watu kama ndoa. Kumekuwa na migongano mingi na mizozo isiyo kwisha katika maisha ya ndoa. Leo ndoa imeonekana kama utumwa, mzingo au kubebeshwa msalaba, na sasa imekuwa kawaida watu kufunga ndoa saa sita mchana kufika saa 12 jioni ndoa imevunjika. Tena jamii yetu ya sasa iliyomomonyoka maadili na kuingiliwa na utamaduni wa kimagharibi ndio kunachangia zaidi migogoro na mivutano katika ndoa.

Kumekuwa na mada nyingi humu zinazohusu ndoa, wengine kuumizwa katika ndoa, wengine kusalitiwa, kupigana mpaka kutoana manundu, wengine hata kuana na wengine kuachana kabisa. Ndio maana nimeona nilete mada hii mezani tuijadili kwa mapana pamoja.

Kwa kuanza kwangu kuchangia katika mada hii nitajikita kuelezea majukumu ya mke kwa mume wake na majukum ya mume kwa mke wake. Kwa sababu kila mtu anayeingia katika mkataba wa ndoa, anaingia katika mkataba huo akiwa na matatizo yake binafsi na kiasi fulani cha ujinga wake. Ili ndoa iweze kustawi na kudumu lazima kila mwanandoa ajue wajibu na majukum yake. Wahenga wanasema ndoa ni chuo, hivyo wanandoa wanashauriwa kuwa tayari kujifunza, ndoa haiwezi kuimarika endapo wanandoa hao watabaki kung'ang'ania misimamo yao waliyokuwa nayo kabla ya kuona. Na hizi ndio njia pekee za kuimarisha na kustawisha ndoa na kuwa ya furaha wakati wote. naelezea kwa ufupi ili nisimchoshe msomaji.

Nikianza na majukumu ya mke kwa mume wake:

(1) Kazi ya mke ni kumtunza na kumlea mume. Najua hii si kazi rahisi kwa wanawake wengi, jukumu hili linahitaji busara, hekima na mbinu nyingi.

(2) Kumstahi na kumheshimu mume . kumheshimu mume wako haina maana umejidhalilisha, Bali njia ya kuonyesha upendo kwake na unamjali. Unatakiwa uwe mpole na adabu unapozungumza na mume wako, usizungumze nae kwa ukali, usimtukane, uwe msikivu kwake wakati wote. Tena usithubuti kumwita mume wako majina machafu au majina ya utani asiyoyapenda. Mumeo anapokuja nyumbani, jaribu kutabasam na kumsalimia kwa uchangamfu. Sio akifika umefura kama umemeza chura. Hapo unampa nafasi ya kuchepuka tu, akafurahie nyumba ndogo maana akifika mlangoni tu ameishaitwa majina 40 kidogo tena matamu, anapokelewa kwa mabusu na mahaba ya hali juu, kisha anavulishwa kiatu na nguo na kutengewa maji ya moto ya kuoga. Mwisho wa siku anaamia nyumba ndogo we unabaki unalalama tu mme wangu kalishwa libwata wapi kaa hapo.

(3) Epuka malalamiko na manung'uniko. Ni kweli hakuna mtu asiye kuwa na matatizo na manung'uniko kuhusu maisha. Lakini kuna baadhi ya wanawake wao kutwa malalamiko hasa yanayolenga maisha ya kipato cha mume na watu wengine. Muda wote mbona Mimi unajanunulia hiki, mbona yule ana hiki, tena analalamika bila kujali uwezo wa mume. Inafika mahali mwanaume anakata tamaa, maana tabia ya mwanamke kulalamika, kunung'unika na kudekadeka wakati wote inaudhi wanaume wengi.

(4) Kuwa mvumilivu wa kazi ya mume wako. Kila mtu anayo kazi na kazi zimetofautiana, na kila kazi ina hadha yake. Kama mume wako ni Mwalimu, daktari, dereva, mhandisi, fundi ujenzi, fundi makanika, muokota makopo n.k ipende kazi yake na umshukuru Mungu kwamba mume anajishughulisha. kwa mfano Daktari ukesha hospitalini akiwahudumia wagonjwa, Dereva husafiri sana na kutumia siku kadhaa kuwa mbali na nyumbani kwake. Mwalimu anatumia muda wake mrefu kutayarisha masomo, kusahihisha kazi za wanafunzi. Fundi makanika, kutwa nzima anachezea mafuta machafu na grisi, na wafanyakazi wengine hali kadhalika.

Shida inakuja mwanamke anataka mume awe nyumbani mapema na matatizo kwa wale wanaoishi Dar foleni, basi mume akifika nyumbani tu basi mke anamudandia ulikuwa kwa mahawara wako na maneno mengine ya maudhi. Bahati mbaya sana kuna wengine wanakuwa sio waaminifu kwenye ndoa zao kutokana na kazi ya mume kwa mfano km madereva wa masafa marefu dah! Ngoja niachie hapo lakini huo nimetolea mfano tu madereva msije mkanitoa nyongo bure.

(5) Usiwe na tabia ya kumwazia mume wako vibaya. Tabia ya kumwazia mwenzako vibaya ni tabia mbaya sana tena yenye madhara makubwa. Bahati mbaya wanawake wengi wana ungojwa huu. Si vibaya kumfatilia mume wako lakini tabia hii isivuke mipaka. Ukiona mwanamke mwenzako kamchangamkia mume wako au kumsalimu tu basi ni hawara yake, akitoa msaada wowote kwa mwanamke yeyote hata kama ni mjane, unasema sio bure kuna namna hapa unafura, Akimpa lifti mwanamke yoyote hata kama ni bibi kizee utasikia siku hizi unachukua mpaka vibibi Mimi sikuridhishi?

Mwanamke yoyote akimsifia mume wako jamani ana roho nzuri, mkarimu na mpole basi inakuwa tabu kwa mumeo siku hiyo apakaliki ndani. Ukisikia simu ya mumeo inaita unakimbia kwenda kusikiliza anaongea na nani, meseji ikiingia unataka uwe wa kwanza kusoma. Kila saa mume anakaguliwa. Kwa tabia kama hizi huifanya nyumba kuwa jehanamu kwa mume. Nyumbani panakuwa pachungu kuishi.

(6) Mwanamke unatakiwa kutunza siri za mumeo. Wanaume wengi wanaamini wanawake awawezi kutunza siri. Ni kweli wanawake wengi wanapenda kutoa siri za ndani sana na kupeleka kwa marafiki na majirani. Japo wanawake wengi wanapenda kujua siri za mume wake, lakini wanaume hawako tayari kuwambia siri zao kila kitu. Unapotaka kujua siri za mume wako jifunze kutunza siri.

Sifa nyingine kwa ufupi, kubali uongozi wa mume wako hata kama una PhD 3, una mamlaka makubwa serikalini usije kuyaleta kwa mumeo, hayo mamlaka yako yaishie getini. Uwe safi na Mrembo muda wote huwapo nyumbani sio kujiachia tu, na wengine mawingi kichwani mpaka yanatoa harafu, jumlisha na kikwapa mume lazima akimbie tu.

Unatakiwa umrizishe mume wako na si wazazi wako. Uwe mwelevu na mvumilivu pale kipato kinapoyumba. Epuka kushiriki kupiga umbea. Kuna sifa nyingi lakini ngoja niwaachie wengine muendeleze.

Kwa upande wa Mume:

(1) Mume ni mlinzi na mlezi familia. Wajibu mkubwa wa mwanaume katika ndoa ni kulea na kutunza familia(Kichwa cha familia). Kwa ufupi.

(2) Mpende mke wako. Mke wako kabla ya kumuo alikuwa anafaidi mapenzi toka kwa wazazi wake, sasa ameamua kuingia katika mkataba wa ndoa na wewe, kuishi maisha yake yote basi mpende sana. Kumuoa mwanamke sio kumuajiri kama mfanyakazi, bali ni kumchagua mwenza na rafiki ambaye utaishi naye katika maisha yako yaliyosalia.

Sifa zingine kwa ufupi:

Mtumze mke wako, usipomtunza usije kulauumu kutunziwa na wanaume wa mjini. Kuwa mfariji na kumliwaza mke wako kila wakati unapopata nafasi. Epuke kutafuta mapungufu kwa mke wako. Epuka kusikiliza maneno ya pembeni. Usitamani wanawake wengine. Uwe na shukrani kwa mkeo. Na sifa nyingine nyingi.

Lakini sifa kubwa kuliko zote: Kwa imani ya dini zetu mumtanguliza Mungu kila wakati ombeni na mumlilia kwa ajili ya ndoa yenu, hakuna mtu atakayefurahi mkiishi kwa amani na mumeo au mkeo, wataanzisha fitina na kuwaendea hata kwa sagoma muachane. Lakini wanaomwamini Mungu hayatawapata kamwe mtazidi kuimarisha zaidi penzi lenu na kuwa la furaha.

Asante kwa kutoa ushirikiano wa kusoma na Mungu akubariki lakini usipite kimya kimya toa neno kwa wana JF wenzio, na kama unaswali uliza pia utajibiwa humuhumu JF ndio kila kitu.
 
Kabla sijatoa mchango wangu Katikaada naomba kukuuliza maswali matatu.

1. Leo nimeshituka kukuona huku kwenye jukwaa la mapenzi ukizungumzie ndoa, tunakujua wew ni mwanasiasa vipi leo na mada yako unataka kusema umestafu siasa rasmi?
2) Naamini humu JF hakuna mtoto iweje useme watu wazima tu watoto wapishe, je kuna mtoto humu?
3) Je wew unatimiza majukum yako kwa mke wako? Naomba unijibu kwanza alafu tuendelee mada.
 
Nimesoma ujumbe wako nilipomaliza nikascroll up nione nani mwandishi mahiri!
Kweli maswala y mahusiano yanaletwa sana humu jf na sehem zngne mbalimbali tena tunaletewa kila aina ya vionjo vya jinsi ya kuishi ndani y ndoa!zamani wazazi wetu walipooana waliambia maneno machache sana tofauti na sasa lazma mzazi ufanye kazi ya ziada.
Ila ndo hivyo wanawake w sasa ingawa sio wote sijui hizi tabia wameokota wapi ni mapungufu kweli yapo kibinadamu ila mapungufu haya yamekuwa makusudi ndoa haina furaha wala huruma na mapenzi hakuna uvumilivu.wanawake rahisi kulaghaiwa yaani muumba wangu sitakuja kuoa me
 
Haaaaaaaa maswali mengine bwana, basi sawa ngoja nikujibu. Katika jamii kuna mambo mengi sana ya kuzungumzia na sio siasa pekee. Tena ndoa imekuwa ni janga la kijamii na limeleta athari kubwa sana katika familia nyingi. Hivyo halina watu maalum wa kusemea hili, matatizo ya ndoa yanawakabili wanadamu wote wakiwemo wanasiasa wako pia.

Swali lako la pili, Mkuu hii ni lugha ya kisanaa kuvuta hadhira, hujawi kuona gazeti la udaku limeandikwa Wema wamerudiana rasmi Diamond Zari Kabaki mdomo wazi. ukakimbia kununua ili usome nini kimo ndani, sababu ya kurudiana ukifungua unakuta kitu tofauti na kile ulichotarajia, unabaki kofyoza lakini umeisha mchangia shigongo mtaji. Lkn pia mkuu kuna watoto humu mdani we wafutilie hoja zao ni za kipuuzi na matusi tu, mtu mzima atukani. Na hapa watoto utawaona.
Swali lako tatu, nitakujibu pm. Asante na karibu tena
 
Sawa nimekusoma mkuu, swali lilobali ungejibu humu kwa faida ya wote. Hata hivyo naona moderator wamebadili kichwa cha mada . Ila ujumbe umefika ngoja kwanza nitimize majukum yangu ya ndoa nitarudi baadae
 
Jando na Unyago virud
Katika enzi zile sifa zilizomfanya mwanamke aolewe hazikuwa uzuri wa maumbile, wala elimu ya darasani, isipokuwa mwanamke alichaguliwa kwanza kwa sifa uhodari wa kufanya kazi, uzazi alionao, tabia aliyonayo n.k mwanamke mvivu alikuwa hapendwi na wanaume wengi. Pia wazazi walikuwa. Wanawajibika kumchagulia mtoto mke au mke wa kuishi nae au kijana alipotaka kuoa wàlichagua ukoo wenye heshima. mfumo huu ulifanya mwanamke kuwa chini ya himaya ya mwanaume, na kukubali kutawaliwa. Lakini siku hizi hali ya uchumi imebadilika, mitindo ya maisha imebadilika pia, wanawake wengi wamehelimishwa mashuleni na wanaharakati. Imefikia hatua tumeache utamaduni wetu wa nyuma, kijana ana Uhuru wa kuchagua ampendae, kijana anatogaza Facebook binti ajui hata historia yake basi anao mwisho wa siku ndoa haidumu.
 
Sijaisoma bado

Ila nimecheka huyo post ya pili anakushangaa kukuona MMU wakati wote wageni...eeeeh
Andika yako basi, wajiuliza wajijibu hahahaaaa
 
Nimesoma ujumbe wako nilipomaliza nikascroll up nione nani mwandishi mahiri!
Kweli maswala y mahusiano yanaletwa sana humu jf na sehem zngne mbalimbali tena tunaletewa kila aina ya vionjo vya jinsi ya kuishi ndani y ndoa!zamani wazazi wetu walipooana waliambia maneno machache sana tofauti na sasa lazma mzazi ufanye kazi ya ziada.
Ila ndo hivyo wanawake w sasa ingawa sio wote sijui hizi tabia wameokota wapi ni mapungufu kweli yapo kibinadamu ila mapungufu haya yamekuwa makusudi ndoa haina furaha wala huruma na mapenzi hakuna uvumilivu.wanawake rahisi kulaghaiwa yaani muumba wangu sitakuja kuoa me
Ndugu Adden usivunjike moyo kuoa, wanazuoni na wataalamu wengi wa masuala ya ndoa bila kujali dini zao au itikadi zao wote wanakubaliana kwamba ndoa ni jambo muhimu sana kwa binadamu na ina faida nyingi sana. Na kwa dini zote wanaamini ndoa ni baraka ya mwenyezi Mungu kwa mfano katika uislamu wanaamini ndoa ni mkataba ambao kila muislamu awe mwanaume au mwanamke lazima aingie katika mkataba huo labda kuwe kuna sababu maalum za msingi za kumzuia kuingia katika mkataba huo.
Sawa nimekusoma mkuu, swali lilobali ungejibu humu kwa faida ya wote. Hata hivyo naona moderator wamebadili kichwa cha mada . Ila ujumbe umefika ngoja kwanza nitimize majukum yangu ya ndoa nitarudi baadae
Katimize kisha urudi tuendelee.
 
Nimezitaja kwa ufupi ili kufupisha mada isichocheshe msomaji, najua sisi watanzania ni wavivu wa kusoma, labda kama ni habari nyepesi kama hadithi, stori au umbea fulani wanasoma hata kama ni ndefu kiasi gani.

Mkuu mbona za wanawake hukutaja kwa ufupi?
 
Ndoa ni furaha ndoa ni amani ndoa ni tunu!
Ila kwanini 70% ya ndoa zina mgogoro?!ingawa migogoro inatufautiana ila kikubwa naona wanandoa kutoridhika na mienendo na misingi ya ndoa ambayo iko wazi na huwezi kuniambia hadi mnaoana hamjui kwann mmeoana au hamjui ndoa inapaswa kuwa vipi?!au wengine tunajaribu ndoa?!bila kuwa tayari kwa suala husika!taendelea kuwa na imani kwamba ndoa hizi za majaribio ndo zenye mgogoro na misunderstanding.
Ila kama ni ndoa ya commitment toka both sides haiwezi kufikia migogoro ya ndoa za majaribio.
 
Expectations ndugu..
 
Back
Top Bottom