Majizzo awashusha Clouds kwenye uandaaji wa Festival, Samia Serengeti Festival jukwaa lake ni la kimataifa

Majizzo awashusha Clouds kwenye uandaaji wa Festival, Samia Serengeti Festival jukwaa lake ni la kimataifa

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,563
Reaction score
7,321
Wote tunakumbuka miaka ya 2000s mwanzoni kuja mpaka miaka ya 2010s na miaka iliyofuatia hapo, Fiesta Festival chini ya CMG (Clouds Media Group) ambayo ndio kampuni inayomiliki Clouds TV na Clouds FM chini ya kichwa cha Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga iliweza kukimbiza kwa show za kufa mtu hapa Tanzania. Watu wengi wa miaka hiyo walikuwa na ufahamu na utambuzi watakuambia Fiesta Festival ilishika nchi nzima kwa umaarufu wake.

CMG waliweza kuendesha Show ya Fiesta kila ukanda wa Tanzania, walijitahidi kupeleka show ya Fiesta kila mkoa, na siku zote walijitahidi mkoa wa kufungia show ukiwa Dar es Salaa. CMG waliweza kuleta Wasanii wakubwa miaka hiyo kama kina Rick Ross, Shaggy, na wengineo kupiga show Dar es Salaam. Na msanii kama Shaggy alitembezwa mikoa mingi, wakati huo mimi nikiwa Mwanza pale, na kipindi icho Mwanza uwaambii kitu kuhusu mziki wa Dancehall, Shaggy kuletwa mwanza kwenye Fiesta ilikuwa ni kama kuwanywesha maji watu wenye kiu kikali.

Clouds kwa kweli walisimika utawala wao kwenye kusambaza burudani nchini Tanzania. Na kwa miaka hiyo waliweza kutamba, na hakuna msanii wa kibongo aliyeweza kukataa kupiga show, kwa sababu ilikuwa ndoto ya kila msanii kutumbuiza kwenye jukwaa kubwa. Na clouds kupitia Fiesta Music Festival kwa ukanda huu wa afrika mashariki na kati ilikuwa ndio jukwaa kubwa la muziki. Show hii baadae ikaja na kupotea kabisa na haikusikika tena baada ya Ruge Mutahaba kuanza kuumwa na badae kufariki. Kifo cha ruge kiliondoka na baadhi ya vitu vilivyoanzishwa kama Fiesta Music Festival, Kipindi cha Fursa, THT (Tanzania House of Talent) na baadhi ya matukio makuu ya CMG.

Baadae akaibuka kijana mdogo aliyeitwa Majizzo akianza kazi kama DJ, na baadae alivyopata mkwanja akatengeneza media yake ya EFM na ETV. Majizzo alikuja kama Messiah kwenye ulimwengu wa burudani wa Tanzania hususani kwa wasanii wadogo kama waimba singeli na kadhalika ambapo walipewa platform ya kutambulisha nyimbo zao. Majizzo hakuishia hapo alianzisha festival zake za muziki, japo haikuwa na muendelezo mzuri kama zile za Fiesta chini ya Clouds. Festival za Majizzo zilikuja kipindi ambacho Media za burudani zimekuwa nyingi, na festival nyinginezo kama wasafi Festival na Nandy Festival zilizokuwa chini ya wasanii wa mziki kuwa kama washindani. Baadae Festival hizo za Majizzo chini ya EFM na ETV zilipotea gafla.

wiki hii sasa, Majizzo kaibuka na Festival nyingine ambayo inaonekana wazi ina ubia kama sio usoda na serikali ya Tanzania, ambapo imepewa jina la Samia Serengeti Music Festival. Festival hii wikiendi hii ya leo imetabulishwa kuwa na kiingilio cha bure kwa watu wote, na wasanii wengi wakitumbuiza. Kilichowashangaza wengi ni jinsi ukubwa wa jukwaa la festival hiyo ulivyo, ambapo jukwaa limetengenezwa kuwa kubwa sana na lenye viwango vya kimataifa. Ujasiri huu wa majizzo umewashitua wengi na wengineo kuuliza kama itakuwa na muendelezo au ni mbwembee za kuelekea uchaguzi mkuu wa nchi.


View: https://www.instagram.com/reel/DI6gUeZskEQ/?igsh=MmdsbWZkaHIzaDU0
 
Jamaa hata afanye kitu kwa ukubwa kiasi gani huwa hakionekani kuwa kikubwa nafirikiri ana shida kwenye promotion
 
Mbona hakuna promotion, jukwaa kubwa hivyo, alafu hakuna matangazo, Majizo bado hajajua power ya kutangaza event, mara nyingi event zake hazisikiki sbb hatangazi
 
Back
Top Bottom