Kuna watu wana roho mbaya mpaka ukiwaona unawaza labda wanatokea sayari ya tofauti mana kiuhalisia mambo wanayoyafanya ni yatofauti kabisaUnazuiwa unamwaga mbali na kuanza kusomba kwa kichwa chezea waswahili mie sina hamu, ulipofikia wewe komaa tu wasalimie tu pita zako wataona aibu tu wao wenyewe.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu napo nawewe bega kwa bega kwa hiki ulichokiandika
Mama angu kaanza kujenga tangia 2011 mwanzo kuna mzee tulimuamini sana na kupelekea kumpa hela zote za material lakini akawa anazifanyia mambo yake
Mama akaamua kuachana naye asa kile kitendo kilimuuma sana kwani mama alishampata fundi mwingine
Yule fundi aliteleza wakat wanapauwa walikutana na mauzauza mengi sana ikiwemo kuumwa kichwa, kuhisi uchovu na hata kunusurika kuanguka lakini walifanikiwa kupauwa
Baada ya hapo ndani kukawa kuajaa matandabui kwenye kona zote ikimaanisha kuifunga nyuma isiendelee
Daaah binadamu binadamu binadamu mbona tupo hivi
Eeeh Mungu shusha gharika
Sent using Jamii Forums mobile app
Hebu tuma picha ya mke wa jirani akiwa ameangalia chini kwa aibu wakati unamuulizia ishu za salamu...
Umenena vyema....
Inawezekana kabisa jamaa anatumia maji mpaka wanakosa ya kutumia, na haombi radhi kwa yanaayotokea...
Majirani wanahangaika kutafuta maji siku 2 kabla kisima hakijajaa...
Inawezekana, hivyo vifaa akiweka siku ya kuchukua anasemea pembeni vifaa vyake vingine havioni...
Ajitafakari alipokosea...hakuna kama jirani ndiye ndugu yako wa kwanza..ishi naye vizuri..
Everyday is Saturday..................... 😎
Mafundi ni watu wenye ustaarabu hafifu. Usipokuwa makini wanakugombanisha na majirani bure.
Mkuu hongera binadamu ndo tulivyo siku zote "mtu anayekufahamu ukimwambia au akiona mafanikio yako roho ya kwanza kumjia ni roho mbaya sasa hapo ndo anahiyari yake kuipokea au kuikataa"
Ila nini mkuu fanya basi hata buku mchana upite vizuri boss [emoji41][emoji41]
Sent using Jamii Forums mobile app
ila tuseme ukweli mkuu..kwa jinsi tu ulivyoandika hii mada, inaonyesha una vimajivuno flani.
Binadamu Ni shida sana na wwe pia jaribu kujichunguza tabia yako hujawabadilikia majirani zako
Sent using Jamii Forums mobile app
Ni mimi jirani yako, umeamua kuja kunianika eti! Nakuheshimu wewe kijana naomba tusifike mbali,,,
Ukiwafahamu wanadamu hutapata shida zaidi ya kuchukua tahadhari tu
Sent using Jamii Forums mobile app
Mtoa Uzi tupia picha basi hapa tupate uhalisia wa unachosema!
Ila hata humu jamvini wako wengi wenye wivu! Utawagundua tu kwa comments zao!!
Mkuu mbona kawaida sana hiyo? Mimi nilifukuzwa na mwenye nyumba kisa mlo wangu uko vizuri!? Leo kuku ndizi/wali kesho rost maini kesho kutwa natoka out na shemeji yako yeye dagaa wanapishana daily.no outings Yaan Ni shida
Hiyo Hali ni ya mtu na mtu, umempata jirani mbaya.katika maisha wapo watu wa aina hiyo wengi tu.Kiukweli siku ya Jana nimedhihirisha ule usemi, kuwa majiran watakupenda wakiona mafanikio yako yapo chini,..na maisha yako Ni duni kuliko wao, ila ukiwazid kidogo Basi usitegemee ushirikiano wait Tena..
Mimi Ni kijana tu wa miaka,ya makamo..nlijichanga nikanunua mahali kiwanja..mwaka 2018.kwenye maeneo Hayo Kuna jirani ZANGU ambao nliwakuta tayari wameshajenga na wanaishi na familia zao..tulikuwa tunasalimiana vizuri mnoo..Tena walikuwa wakinikaribisha Kila wakati nnapokwenda saiti kuangalia kiwanja changu na kulimia limia sehemu penye nyasi..
Baada ya mwaka mmoja nikaanza kumwaga mawe,.kwa ajili ya kujengea msingi..ushirikiano ulikuwa Bado Ni mzuri na majirani ZANGU...nnaopakana nao..Basi mwaka huo huo 2019 nikaamua kujenga msingi..na jirani akaniambia usiwe na Shaka maji utatumia tu haya haya..Mana yeye ana kisima kikubwa Sana..na huwa kinajaa maji Kila baada ya siku mbili..
Mungu akajalia msingi wa vyumba vitatu vya kulala kimoja Ni master yangu.jiko sitting room,dinning stoo,na public toilet..ukaisha wote na kuupiga lipu.(Kuufuta kwa juu)..jirani yangu baada ya kuona huo msingi akaanza kunipiga stop kutumia kisima chake,.nikamuomba niweke maji yangu kwenye kisima hicho pia akakataa,..akaanza kuninunia yeye pamoja na mkewe
Basi nikaomba sehemu mapipa nikayajaza maji ujenzi ukaendelea..nikaleta tofali za block Basi jirani ndo akazid kuonyesha makucha yake ya chuki bila sababu..kuna mtu akaniambia ungejenga chumba kimoja angekupa maji..Hadi mwisho..ila kwa vile umejenga nyumba kubwa kuliko yeye ..hapo anahisi utampiku ndo Mana anakufanyia visa ili ushindwe kujenga nyumba hiyo.
Cha ajabu Zaidi, nlikuwa natumia chumba chake Cha nje ambayo Ni stoo yake kuwekea vifaa vyangu vya ujenzi, siku ya Jana nlipopeleka mifuko yangu ya cement kwa ajili ya kumalizia over lenta akawaambia wale watu wa gari kuwa iwekeni nje msiingize ndani Mana jirani hanisalimii vizuri, na Cha ajabu Hali ya hewa kulikuwa na mvua..wale vijana waliponipigia simu ikabidi nipande kwa haraka, nikamuuliza jirani mbona Kila siku tunasalimiana,.unasemaje sikusalimii vizuri akawa mpole akainamia chini..huyu Ni mke wa jirani yangu Mana mumewe hakuwepo hapo nyumbani.
Basi baada ya kuona hanijibu nikahamisha mifuko yangu kwa mzee mmoja ambae amejenga nyumba yake ila yeye haishi hapo
Aisee hata rafiki zako watakupenda ukiwa unalingana nao kipato,.na maisha au upo chini yao...Ila ukiwazidi tu Basi subiria kunyanyapaliwa...huku uswazi kweli shida aisee...
Sent using Jamii Forums mobile app
Hata na wewe utajengaje kimasikini kwa kutegemea msaada na fadhila za wenyeji bila kuwapa chochote? Maji upewe bure! Mahali pa kuweka na kutunzia cementi upewe bure! Alafu hata kujiongeza angalau ukaenda na kilo mbili za nyama au hata 20,000 ya kushukuru hapana? Weee ndo mswahili! Alikuwa akikufadhili ulipokuwa unaonyesha bado hujajipanga! Sasa unajenga vifaaa vya mamilioni vinapita unaishia kumlisha vumbi? Weee ndo hujapevuka!
Mimi niliwahi kujenga lakini kila fadhila niliyokuwa napewa na wenyeji nilikuwa natoa mkono wa asante! Kuna siku mama mmoja nilichota maji yake yakaisha tena ya kisima cha kuchimba lakini baada ya kuyatumia nikampa 5,000 akashukuru mahusiano yakaendelea! Mimi nakuona wewe ndo mswahili unashindwa kusoma jamii unayohamia na kusema heti wanakuonea wivu! Winu gani sasa!
Hapo ndiyo utajua wewe ni mtu wa mataifa...Mafundi Ni wasabato wenzie..na huwa wanakutana Sana kwenye ziara za makanisa..sidhani Kama wananifanyia hivyo kwasababu ya mafund
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu una busara ambayo vijana wengi hawana leo hii.
Kuishi na waswahili tunahitaji busara na akili ya kujiongeza sio mbwembwe za kitoto.
Kuna wakati fulani nanmie nilikuwa na ujenzi maeneo fulani ya mamwinyi ma alwatani . Mmoja wa mzee mmoja jirani yangu inasadikika aliogopeka sana kwa uchawi.
Baada ya kufahamu hilo kabla ya kujenga nikajotambulisha kwake, nikajifanya lofa. Nikamwambia mi ni mgeni wakuja sina wazazi hivyo naomba anisimamie kama baba.
Nikaongea uongo mwingi na kumletea vizawadi kila nikija site. Vifaa vyangu nikawa nahifadhi kwake, akawa ndo baba.
Mtihani ukaja pale nimemaliza kujenga akaniambia aje kuzindika nyumba yangu. Mi si muumini wa mazindiko, nikamwambia kwa upole kuwa mi sihitaji mazindiko kwa sababu we baba upo hakuna wa kunigusa mtaa huu, na kama nitahisi kuonewa utaniona kwako .
Mzee akaona ninaimani naye sana , akacheka, akaondoka kwa kuridhika na tukaishi vizuri yeye na familia yangu. Nikisafiri nampigia simu, nikipata cha kumbebea nambebea nikirudi ananipatia mrejesho wa usalama wa familia yangu.
Mwisho alikuwa na eneo/kiwanja kizuri kimepakana na mimi mzee akagoma kukiuza kwa mtu yeyote akaniuliza kama mi nakihitaji tuandikishane nikichukue pesa nimpatie kidogokidogo.
Tukaishi vizuri japo alikuwa anasifika kwa uchawi hatari , nikawa msaada kwa wanae kuwatafutia connection maisha yakaendelea vizur
Sent using Jamii Forums mobile app