Majirani zangu wameanza kununa

Yawezekana ni mtazamo wako ndio tatizo.
 
Una point hapa kubwa sana
 
Mkuu napo nawewe bega kwa bega kwa hiki ulichokiandika
Mama angu kaanza kujenga tangia 2011 mwanzo kuna mzee tulimuamini sana na kupelekea kumpa hela zote za material lakini akawa anazifanyia mambo yake

Mama akaamua kuachana naye asa kile kitendo kilimuuma sana kwani mama alishampata fundi mwingine

Yule fundi aliteleza wakat wanapauwa walikutana na mauzauza mengi sana ikiwemo kuumwa kichwa, kuhisi uchovu na hata kunusurika kuanguka lakini walifanikiwa kupauwa

Baada ya hapo ndani kukawa kuajaa matandabui kwenye kona zote ikimaanisha kuifunga nyuma isiendelee

Daaah binadamu binadamu binadamu mbona tupo hivi

Eeeh Mungu shusha gharika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtani mbona kujenga ni kitu cha kawaida tu now days.

Unaniangusha ujue 😀
Kujenga ni kitu cha kawaida? Hebu mwacheni mleta uzi ajidai. Kuna member humu alimkataa member mwenzake kisa hajajenga. Hebu mwacheni mwenye uzi wake afurahie ujenzi
 
Umenena vyema....
Inawezekana kabisa jamaa anatumia maji mpaka wanakosa ya kutumia, na haombi radhi kwa yanaayotokea...
Majirani wanahangaika kutafuta maji siku 2 kabla kisima hakijajaa...
Inawezekana, hivyo vifaa akiweka siku ya kuchukua anasemea pembeni vifaa vyake vingine havioni...

Ajitafakari alipokosea...hakuna kama jirani ndiye ndugu yako wa kwanza..ishi naye vizuri..

Everyday is Saturday..................... 😎
 
Mafundi ni watu wenye ustaarabu hafifu. Usipokuwa makini wanakugombanisha na majirani bure.
 
Mkuu hongera binadamu ndo tulivyo siku zote "mtu anayekufahamu ukimwambia au akiona mafanikio yako roho ya kwanza kumjia ni roho mbaya sasa hapo ndo anahiyari yake kuipokea au kuikataa"

Ila nini mkuu fanya basi hata buku mchana upite vizuri boss [emoji41][emoji41]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe!!nilidhan ni kitaa chetu tu,mpaka nakiitaga kiwanja kilichokuwa kinafanyiwa mikutano Na wachawi

mwongo atofautiani Na mchawi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…