Majirani washauri mtoto mlemavu auawe - Ontario Marekani

Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,143
3,196
Waafrika huwa tunaamini kwamba ukimcheka mlemavu, au ukimsema vibaya mama mwenye mtoto mlemavu basi na wewe utapata ulemavu au utazaa mtoto mlemavu. Hii kwetu ni myth na kila mmoja anamheshimu mtu mwenye ulemavu bila kujali usumbufu anaoweza kuwa nao. Tuna familia nyingi za watu wenye ulemavu na tunaishi nazo vizuri, tukiwa wadogo tumecheza na wenzetu waliokuwa walemavu, bila kujali ulemavu wao. Lakini angalia hawa wenzatu; majirani wanalalamikia kelele za mtoto mwenye mtindio wa ubongo ambaye wanaishi naye mtaa mmoja. Wanasema ni bora kusikiliza kelele za watoto wakilia kuliko kusikiliza kelele za huyo mtoto mwenye mtindio wa ubongo, wanamshauri mwenye mtoto ama ahame mtaa au amue tu huyo mtoto maana hana faida yoyote. Hataweza kupata mke mzuri kwakuwa hakuna mwanamke atakayekubali kuolewa naye, hawezi kuwa na msaada wowote katika maisha yake. Na wanamuonya kwamba ajue yeye (huyo mzazi) hataishi milele, kuna siku atakufa na huyo mtoto atakuwa mzigo kwa wengine. Hebu soma hii barua hapa chini; inasikitisha sana.

autistic-letter.jpg

Source: Yahoo! News Canada - Latest News & Headlines
 
Dunia ya sasa watu wenye imani ni wachache sana. Mungu amsaidie!
 
Back
Top Bottom