Majipu kwenye mwili wa Waziri Mkuu Majaliwa

Suleomary

Member
Jul 4, 2015
12
12
Serikali ya awamu ya tano imekuwa ikijinasibu kwa kutumbua majipu, lakini wakati huo huo katika wizara inayoongozwa na waziri mkuu nako kuna majipu ambayo muda si mrefu yanaweza kusababisha saratani.

Majipu hayo yapo katika wizara ya bunge, kazi, walemavu na vijana hasa katika idara inayohusu vijana na idara inayohusika na utoaji wa vibali vya kazi.

MAJIPU KATIKA IDARA YA KAZI.
Mchakato wa utaoji wa vibali vya kufanya kazi hapa nchini kwa wageni ambao sio watanzania umetawaliwa sana na rushwa kiasi cha kushindwa kuzingatia vigezo ama kuwanyima haki wale wasioweza kutoa rushwa.

Pia kuna watu wanapewa vibali vya kufanya kazi nchini kwa taaluma ambazo watanzania wakutosha wenye taaluma hiyo wapo. Hili unaweza kulithibitisha hasa kwenye sekta ya mawasiliano, nenda NOKIA angalia hao waliopewa vibali kama expatriate utachoka, maana hawana tofauti na vijana wengi walioko mtaani bila kazi.

MAJIPU KATIKA IDARA YA KUSAIDIA VIJANA
Urasimu katika idara hii umetawala katika maeneo makubwa matatu ambayo ni mfuko wa kusaidia vijana, mwenge na mambo yanayohusiana na utawala.

Mkurugenzi wa idara hii akishirikiana na mhasibu mkuu wa wizara ya habari wamekuwa vinara wa kutafuna fedha hizi wanavyotaka kupitia migongo ya watumishi ambao hawajui kinachoendelea.

Fedha za mfuko zinatumika kwa matumizi ya tofauti na malengo ya uanzishwaji wa mfuko huo, na hapa ukifuatilia miamala iliyofanywa katika akaunti inayoweka fedha hizo utagundua ufujaji unaofanyika chini ya mkurugenzi na mhasibu wake.

Wakati vijana wakiwa na shida nyingi lakini mkurugenzi amelalia Zaidi ya bilioni moja yenye muda mrefu sasa bila kutoka lakini anaendelea kutafuna hela hizo kidogo kidogo kwa kisingizio cha kuzikopa kwa matumizi mengine.

Mkurugenzi alivyokuwa mjanja mwaka jana alijifanya kuomba ukaguzi wa mfuko huo lakini hata mkaguzi aliyeletwa aliandaliwa fungu la fedha na baadae kupewa safari za hapa na pale kwa hiyo hapa ilikuwa ni iini macho tu, majaliwa fanya ukaguzi maalum kwenye mfuko huo.

Mkoa wa Kagera ndio mkoa unaoongoza kwa kuwa na vikundi vingi vilivyonufaika na mfuko huo ikifuatiwa na wilaya ya Mvomero, hii ni sababu Mkurugenzi ni Mhaya, Fenera Mkangala alikuwa waziri na Mvomero ni sababu ya Amos Makala alikuwa naibu waziri.

Uhamasishaji wa vijana juu ya namna ya kupata mkopo hufanywa kwa zima moto ili ionekane wamefanya watumie na fungu la kazi hiyo vizuri lakini pia ufuatiliaji wa matumizi ya fedha kwa vikundi vilivyokopeshwa haufanyiki huku fedha zilizotengwa kwa kazi hiyo zikitumika.

Kula fedha za mwenge zilizotengwa na serikali huku wakisingizia zimejenga mabanda mikoani wakati mikoa hujigharamia wenyewe kwa kila kitu
Kula fedha za mwenge zinazotolewa na washikadau sababu fedha hizi hazifanyiwi ukaguzi.

Mkurugenzi wa vijana anasemekana anaendekeza sana ukabila hasa kwenye kupendezekeza watu katika nafasi za uteuzi hata kama hawana sifa yuko tayari kuwaacha walio na sifa.

Kutopenda watu wabunifu, wanaofahamu kazi zilivyo na wanaojua kuhoji kwenye vikao wanaofanya hivyo wamekuwa wakihamishwa kama mwaka jana kuna maafisa walikuwa wanatusaidia sana sisi vijana lakini wakahamishiwa Tabora, Bukoba na Kigoma kwenye halmashauri ili afanye anachotaka bila kuhojiwa.

Tafadhali sana Kassim Majaliwa tumbua jipu hili lililopo kwenye mwili wako kabla ya kutumbua ya wengine, idara ya vijana ilivyo kwasasa haiendani kabisa na mahitaji ya vijana wa Tanzania. Viongozi wanawasilisha ripoti za uongo na kutumia muda mwingi kujipendekeza kwa wakubwa badal ya kufanya kazi zinazoonekana.

SALIM MOHAMED, KWA NIABA YA ASASI ZA VIJANA DAR ES SALAAM
 
hay

o wamazo yako tuu yaliyojawa na chuki binafsi juu ya serikali, na hii yote nikutokana na kuona mmeishiwa hoja chadema hamna jipya tena sasa, Jipangeni upya mtapotea kabisa
Baado Mnaweweseka kwa kuchakachua alafu unasema tutapotea baadala ya nyie kupotea miezi mitatu hakuna mnachofanya zaidi ya kuandamana na wandishi wa habari
 
Mtaisoma namba CHAGA -DEMA . Nyie fanyeni majungu kwa magu huku wezenu ACT wanakuja kimya kimya kama moto wa pumba za randa za mbao. CHAGA - DEMA badilikeni mwaka 2020 karibu sana shauli yenu ACT watakupotezeni kama mlivyo wapoteza CUF na ndoa yenu isiyokuwa na Shekhe wala askofu
 
Naona tangu nilipoweka hii habari majipu yanahaha kutaka kurekebisha mambo, sasa nakuja kivingine
 
Back
Top Bottom