Kwa ufupi ni kwamba chuo hiki kimekuwa kikituhumiwa kwa muda mrefu kuhusu ufisadi katika maeneo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa ghorofa tatu, kufukuza viongozi wa jumuiya ya kitaaluma (academic staff association), viongozi wa THTU, mkuu wa chuo kuitumia bodi kwa maslahi yake, mwenyekiti wa bodi kukaa muda mrefu pamoja na kwamba hana sifa kuiongoza taasisi kubwa km hii. nafasi za kazi kwa upendeleo wa kikabila. mambo mengi yameandikiwa ofisi mbalimbali za serikali tangia mwaka 2012. wafanyakazi walishabahatika kuandika kupitia gazeti la raia mwema. baadaye tunaambiwa mkuu wa chuo (Dr. Richard Masika) amemnunua mhariri mtendaji wa gazeti hilo na baada ya hapo kweli mhariri alikataa kuandika tuhuma hizo za kifisadi pamoja na kwamba zimejaa ushahidi. wafanyakazi tumekosa pa kupaza sauti zetu. Tunamuomba Mh. Rais kupitia jukwaa hili atume timu yake kufuatilia ukweli hatimaye asaidie kutumbua haya majipu.