Majina ya nyongeza usaili utumishi

logan007

Senior Member
Nov 22, 2020
197
200
Habari wakubwa kwa wadogo.
Naona siku hizi utumishi kumekuwa na kawaida ya kuongeza majina ya wasailiwa kwenye interview zao.
Swali je hawa wanaongezwa ndio wenye koneksheni au ndio wale lete MILIONI MBILI upate kazi au ndio watoto na ndugu wa wafanyakazi wa UTUMISHI kule Dodoma?
Weekend njema.
 
Maana utasikia majina ya nyongeza sijui kanzi data sijui nini?
Mi nahisi hapa ndio kuna UPIGAJI
 
Mwenyewe kwenye Suala la majina ya nyongeza sijawahi kuwakubali hata kidogo, nasema hv kwa sababu zifuatazo:-

  • Kwanini hayo majina wasitoe yote kwa pamoja wakati watu wote wamekidhi vigezo..?
  • Kama wamekidhi vigezo kwann wakose kuitwa kwenye batch 1...?
  • kwanini hawatoi sababu ya hao watu wao KUTOKUITWA batch 1 mpaka wanawaitwa kwenye batch probable..?
  • Kwanini wanatoa majina siku moja au masaa machache kabla ya Usaili..?
  • Nimejaribu kufuatilia majina ya nyongeza yote kwenye kazi tofautitofauti huwa wanatangaza leo halafu kesho ndo Usaili unaanza, hv kama Mimi nipo kwetu huku Somalia upande wa Baba nitawahi kweli Usaili unaofanyika Dodoma-Tanzania..? Au hata wale watani wangu(Wasukuma) Kwa upande wa Mama ,wako Mwanza watawahi kweli Usaili unaofanyika kesho yake Dodoma..?

Hapa ndipo tunapoona watu wanachomekwa, yaaan hata yule ambaye hakuomba kazi basi linawekwa jina lake ili aende kusukumwasukumwa Kila hatua na mwisho wa siku apangiwe kazi..

Utumishi kama hamtolei ufafanuzi hili basi Kila kukicha hamtaacha kulalamikiwa na Youth Job seekers
 
Yeah, wanatuletea mambo ya kipa chon dida na mambo ya chupli chupli
 
Kuna wanaoenda kwenye hizo interview bila kujua kwamba nafasi zilizotangazwa tayari watu walishaijaza. Bongo bahati mbaya tuendelee kupambana tuuu..Bao la mkono ni endelevu
 
Nahisi hawa ni wale wanao appeal kutokuonekana kwenye mkeka, so wakishajiridhisha ndo wanawaongeza.
 
Tufanye hivi waliocomplain kuhusu majina yao pengine, najaribu kufanya hiyo assumption
Hii assumption naweza kuifikiria nami.. Ila Kuna jamaa yangu aliwahi kunambia kuwa aliwahi kucomplain kazi fulani ambayo hakuwa shortlisted,,, alitumia Email zao Ila hakujibiwa.. Au Kuna njia zingine tena ni za haraka za kuwaface tofauti na email zao..?
 
IKO HIVI, MFANO UMEOMBA NAFASI ...THEN MKEKA UKATOKA JINA HALIPO NA WAKAWEKA SABABU LABDA HUJAATACH PICHA AU ADDRESS UMEKOSEA....SO WEWE LAKINI HIYO SABABU SIO KWELI ,CZ WALE NI BINADAMU NA HUWA WANAKOSEA SO UNAPIGA SIMU UNAWAELEZEA AU UNAENDA SO WAKIJIRIDHISHA NDIO JINA LAKO LINATOKA KWA NYONGEZA...NI UTARATIBU WA KAWAIDA TUU
 
Hakuna kitu Kama hiki,kwanza hawajawai kupokea simu wale jamaa
 
Habari wakubwa kwa wadogo.
Naona siku hizi utumishi kumekuwa na kawaida ya kuongeza majina ya wasailiwa kwenye interview zao.
Swali je hawa wanaongezwa ndio wenye koneksheni au ndio wale lete MILIONI MBILI upate kazi au ndio watoto na ndugu wa wafanyakazi wa UTUMISHI kule Dodoma?
Weekend njema.
Hayo ndo mambo yanayokatisha tamaa kufanya hizi interview.
 
Back
Top Bottom