Majina ya majimbo mapya haya hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majina ya majimbo mapya haya hapa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MziziMkavu, May 22, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Tume ya Uchaguzi pia yatangaza kata zake

  Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Lewis Makame.

  Hatmaye Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetaja majimbo mapya ya uchaguzi ‘yaliyozaliwa', baada ya majimbo saba ya zamani kila moja kugawanywa na kuwa majimbo mawili, huku kata zote za kila jimbo zikiwekwa bayana.

  Majimbo ambayo NEC imeyagawa ni Tunduru (Ruvuma), Nkasi (Rukwa), Maswa (Shinyanga), Bukombe (Shinyanga), Singida Kusini (Singida), Kasulu Mashariki (Kigoma) na Ukonga (Dar es Salaam).

  Hata hiyo, kwa mujibu wa Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Lewis Makame, Jimbo la Singida Kusini, bado linafanyiwa kazi na kwamba ikikamilika, umma utajulishwa kuhusu majina ya majimbo hayo na mipaka yake.

  Uamuzi wa kugawa majimbo hayo umefikiwa na NEC baada ya kujadiliana na wadau wa majimbo husika ambao walipendekeza majina na mipaka ya majimbo hayo na hatimaye kufikia makubaliano ya kuyagawa.

  "Baada ya majadiliano na makubaliano na wadau katika majimbo husika, majimbo hayo yaligawanywa kama ilivyopendekezwa," ilieleza sehemu ya hotuba ya Mwenyekiti wa NEC, Jaji Makame iliyosomwa kwa viongozi wa vyama vya siasa ngazi ya taifa.
  Katika makubaliano hayo, Jimbo la Nkasi limegawanywa na kuwa Nkasi Kaskazini na Nkasi Kusini.

  Aidha, katika mgawanyo huo, Jimbo la Nkasi Kaskazini lina kata nane; ambazo ni Kabwe, Korongwe, Kirando, Kipili, Mtenga, Nkomolo, Namanyele na Mkwamba, wakati Jimbo la Nkasi Kusini lina kata tisa. Kata hizo ni Ninde, Isale, Chala, Nkandasi, Kate, Wampembe, Kipande, Kala na Sintali.

  Jimbo la Maswa limetoa majimbo ya Maswa Mashariki na Maswa Magharibi.

  Kata zinazounda Maswa Mashariki ni 12; Sukuma, Ng'wigwa, Mpindo, Senani, Nguliguli, Mwamanenge, Ipililo, Lalago, Dakama, Busilili, Budekwa na Nyalikungu.

  Maswa Magharibi lina kata 13 ambazo ni Buchambi, Zanzui, Mwamashimba, Masela, Seneng'wa, Nyabubinza, Mwangh'onoli, Shishiyu, Kadoto, Badi, Kulimi, Malampaka na Isanga.

  Nalo jimbo la Bukombe limegawanywa kuwa Bukombe na Mbogwe. Bukombe lina kata 13, ambazo ni Ushirombo, Ng'anzo, Igulwa, Butinzya, Bukombe, Lyambamgongo, Iyogelo, Bugelenga, Runzewe Mashariki, Runzewe Magharibi, Uyovu, Namonge na Busonzo.

  Mbogwe lina kata 16 ambazo ni Mbogwe, Nanda, Ushirika, Ngemo, Ilolangulu, Ikobe, Isebya, Masumbwe, Nyakafuru, Bukandwe, Nhomolwa, Ikunguigazi, Lulembela, Nyasato, Lugunga na Iponya.

  Nalo jimbo la Kasulu Mashariki limegawanywa kuwa Kasulu Mjini na Kasulu Vijijini.

  Kasulu Mjini litakuwa na kata 14; ambazo ni Murubona, Kumsenga, Kunyika, Murusi, Mwilamvya, Kigondo, Murufiti, Nyansha, Msambara, Muhunga, Heru Juu, Ruhita, Nyumbigwa na Mganza.

  Jimbo la Kasulu Vijijini lina kata 13, ambazo ni Rusesa, Kwaga, Muzye, Rungwe Mpya, Nyamnyusi, Kitagata, Nyamidaho, Herushingo, Buhoro, Kitanga, Titye, Kagera Nkanda na Nyakitonto.

  Katika makubaliano hayo, Jimbo la Ukonga limeganwanywa na kuwa na majimbo ya Ukonga na Segerea.

  Jimbo la Ukonga linakuwa na kata nane; ambazo ni Chanika, Majohe, Gongo la Mboto, Ukonga, Pugu, Kitunda, Kivule na Msongola.

  Wakati Segerea nalo linakuwa na kata nane, ambazo ni Buguruni, Tabata, Vingunguti, Segerea, Kinyerezi, Kimanga, Kipawa na Kiwalani.

  Tunduru limegawanywa kuwa Tunduru Kaskazini na Tunduru Kusini. Tunduru Kaskazini lina kata 13; ambazo ni Kalulu, Ligunga, Matemanga, Namwinyu, Kidodoma, Nandembo, Nampungu, Milingoti Mashariki, Milingoti Magharibi, Mindu, Muhuweshi, Nakapanya na Ngapa.

  Tunduru Kusini lina kata 11, ambazo ni Mtina, Mchesi, Lukumbule, Mbesa, Nalasi, Mchoteka, Marumba, Tuwemacho, Ligoma, Namasakata na Misechela.

  Uamuzi kuhusu mapendekezo ya kugawa majimbo ya uchaguzi, ulifikiwa na NEC baada ya kufanya uchambuzi.

  Mapendekezo hayo yaliwasilishwa NEC na Kamati za Ushauri wa Mkoa (RCC) baada ya halmashauri 45 kupeleka maombi 47 zikitaka kugawanywa kwa majimbo yao.

  NEC ilitangaza majimbo yaliyogawanywa Aprili 16, mwaka huu sambamba na ratiba ya mchakato mzima wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu kuanzia uandikishaji, uteuzi wa wagombea, kampeni na siku ya kupiga kura.

  Kuzaliwa kwa majimbo hayo mapya, kunafanya jumla ya majimbo ya uchaguzi nchini kufikia 239 kutoka 232 ya awali.

  CHANZO:
  NIPASHE
   
Loading...