Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,156
- 13,249
Hii ni tafakuri yangu;
- Awali ilikua dini ya Roma ama Roman baadae ikasambaa duniani kote (catholic) na ikawa Roman Catholic.
- Martin Luther alikua na mapingamizi 95 dhidi ya dini ya Roma wakati akiwa mtumishi na akajitenga kuanzisha kanisa nchini mwake ndilo leo huitwa Lutheran yaani wafuasi wa Luther na ndio vile Wajerumani wengi ni walutheran ila imeenea duniani kote
- neno Anglican linamaanisha England na linashabahiana kidogo na story ya Luther na muasisi wake aliamua kuanzisha kanisa nchini mwake kupingana na urumi na kuitwa Anglican church ama church of england na baadae kusamba duniani kote ila naamibiwa huwezi kuw mtawala england kama wewe si muanglikana
- Baptist ni asili ya watu waliofuata ubatizo wa maji mengi kwenye bibilia na kujitenga na ule wa kunyunyizia
- Methododist ni vijana wasomi waliokuwa hawaridhishwi na mwenendo wa taratibu za kanisa na kanzisha taratibu bora zaidi za kuabudu (methods)
- Seventh Day Adventist lina taathira ya kuweka mkazo katika kuabudu siku ya saba ya juma (seventh) badala ya Jumapili lakini pia utabiri wa majirlo wa William Miller ndio neno Adventists
- ........................ongeza...................................