oi Mkuu Umenikumbusha zamani sana hii Bar Chini ya Muti nilishakula Nyama Choma Bomba sana miaka ya 1994/5 bro wangu ni Guide basi kila akirejea huznguka sana kutafuta marafiki zake siku ikatokea Rafiki zake wapo hapo Chini ya Muti...
Hii sehemu nilikuwa kila nikitoka USA Lazima nilisome hilo Jina la CHINI YA MUTI hivi bado ipo hiyo Bar hadi miaka hii?
Bila Kusahau Barracuda bar hii yule Mwizi maarufu Arusha alikuwa hakosi humo Bob Sambeke....
Pindi hicho kulikuwa na zile bia feki za Safari zikiuzwa humo bila wasiwasi ila si feki kabisa kwani yule mtaalamu wa TBL alikuwa na kiwanda chake binafsi anachanganya ngano kama yupo tbl vile kisha zinauzwa kama safari beer bila mnywaji kujua kitu... japo mwishowe ikagundulika
hii naifahamu kuna wadada ni warangi wapo hapo yani akiwa anaingia ndani mwili ushapotea wote ila inatumia kama sekunde kumi hivi kwa hizo sehemu za nyuma kupotea pia.