Majina mengine ya Mungu

jehova ni mungu akiabudiwa na waisrael na el ni mungu akiabudiwa na jamii mbalimbali za caanan.
maandiko ya bible ni mixer ya maandiko ya walioabudu YAHWEH na walioabudu El, ndo maana jina la el limetokea katika baadhi ya aya za bible

EL ni neno lenye maana ya mungu,linatokana na lugha ya wakaanani kama ulivyosema mkuu,isipokuwa kwa muktadha wa matumizi yake,ni more of a title rather than a name.

Kutokana na neno hili as a root,ndipo kiaramaiki kikapata neno Elah,kiebrania kikapata neno Eloah ambayo plural form yake ni Elohim na kiarabu kikapata neno Allah,yote haya yakimaanisha God yaani Mungu.

Tena kuprove kuwa hii ni title zaidi ya jina halisi,kwa kiebrania wingi(plural form) wake ni Elohim,na kuna baadhi ya maandishi ya zamani sana,yanatumia neno Elohim kumaanisha aina fulani ya viumbe wa mbinguni,na hata fallen angels(nephillims) wakiwaita Elohims,kudhihirisha kuwa hawa malaika waasi waliabudiwa kama miungu wakati fulani hapa duniani,na ndio chanzo cha ibada ya masanamu ya kipagani,ikiwa ni mfano wa vile viumbe halisi vya mbinguni vilivyoshuka wakati wa Yaredi na hata baada ya gharika kule Babylon kuja kuitawala na kuichafua dunia.

Katika miungu iliyoabudiwa kanaani alikuwepo mmoja aliyeitwa El Elyon(Mungu aliye juu) ambaye kuna mafungu kwenye biblia ambayo yanaonyesha kuwa huyu ndiye aliyeabudiwa na akina Abraham na Melchizedek wa Salem na hata dini nyingine za kiabrahamu kama uislam na uyahudi zina context inayofanana katika hili(Mungu aliye juu,Muumba wa vyote,aliye pekee,mmoja tu).

Samahani kwa kumjumuisha Mungu katika miungu ya kanaani,nimelazimika kutumia lugha hiyo ili nieleweke kutokana na uhalisia wa imani miaka ile,ambapo watu waliabudu miungu mingi tofauti,ambapo hata Mungu wa kweli walimhesabu kama mojawapo ya miungu.Mimi siamini hivyo,naamini Mungu ni mmoja tu isipokuwa hapa nazungumza kwa namna ya mazingira ya kiimani yaliyokuwa corrupt ya wakati ule,hivyo msinielewe vibaya wadau,msije mkaniwashia moto hapa.

Kwa hiyo historically katika Semitic languages,Mungu,miungu waliitwa kwa majina ambayo root yake ni El,lakini ni lazima uwe mwangalifu kujua particular sect wanamzungumzia El yupi,Abraham yeye El wake ni El Elyon.

Ndipo hapo watu wengi wanachanganya historia na kudhani kwamba huyu El Elyon ni mojawapo ya pagan deities za Canaan na hivyo kudhani Abraham aliabudu masanamu ya kanani,which is not true.

Hivyo since Mungu wa Abraham alikuwa ni El Elyon(Most High),then it is agreed na wachunguzi wa mambo kwamba all Abrahamic religions zinamwabudu Mungu huyu El Elyon,tofauti inakuja tu katika namna ya kumuelezea,tamaduni na athari zilizotokana na njia ambayo wahusika wameitumia kupokea imani toka vizazi vilivyopita(hata hivyo hilo ni muhimu kulizingatia kwa mtazamo wa kiimani).

Kwa hivyo kwa muktadha huo,inasemekana kwamba kimsingi,ukiondoa athari hizo along the way,Allah na Elohim historically ni Mungu mmoja huyo huyo isipokuwa tu baadae kila mtu akaweka nakshi zake kwa mujibu wa tamaduni zilimopitia dini hizo.

Jambo la msingi kwetu sisi wa kizazi cha leo,tuliopokea dini baada ya kupita katika mikono mingi,ni kuchunguza kama Allah na Elohim bado ni Mungu yule yule mmoja yaani El Elyon kama ilivyoaminiwa na Abraham descendants wa zamani,au along the road nakshi zilizidi kiasi cha kuharibu (corrupt) mantiki nzima ya imani husika,ukakuta kuwa unaabudu jiwe,jua,malaika etc huku ukiambiwa ndiye El Elyon!

La pili,kwa upande wa Wakristo na Wayahudi,

Katika Biblia,wakati Musa akizungumza na Mungu,Mwenyezi Mungu alijitambulisha na kumwambia Jina lake ni I AM(MIMI NDIYE),na kumuambia amtambulishe hivyo kwa Waisraeli.

Kwa kiebrania Jina hilo linaandikwa YHWH(no vowels).

Halikuwa na vowels katika kuliandika kwa taratibu za lugha yao wakati huo.

Lilikuwa na heshima ya pekee,nilisoma mahali fulani kwamba hata katika kuandika hizo herufi,kila herufi iliandikwa kwa kalamu yake na wino wake(wa kuchovya).



Baadae waisrael wakaona ya kuwa jina hilo ni takatifu mno kulitamka,hivyo wakaamua kutumia neno Adonai(Lord,My Lord) mahala pake.

Miaka ilivyosonga kiebrania kikaanza kutumia vowels hata katika maandishi,ikaonekana kuna umuhimu wa kuweka alama za vowels katika kuliandika(vowels zao waliandika kama alama fulani juu na chini ya neno), wakachukua vowels za Adonai na kuzichanganya na consonants za YHWH na kupata neno YAHOWAH,na hapo ndipo matamshi ya mwanzo ya Jina tulilonalo leo yalipoanza,baadae kilatini kikaingiza J na kwa influence ya kilatini na kigiriki pamoja na hiyo Hebrew hybrid ikapatikana JEHOVAH.

Hii yote ni katika kuhangaikia matamshi ya jina hilo.

Waisrael walichangia kwa kiasi kikubwa kupoteza matamshi ya lile Jina halisi la YHWH,kwa kupiga marufuku matumizi yake kwa miaka mingi sana.

Hivyo again,ukichunguza kwa kina kibiblia,tunatumia a Hybrid name Jehovah,jina halisi ni YHWH,baadhi wakilitamka YAHWEH,ila ukweli unabaki kuwa hizi zote ni makisio tu,kwa leo,nobody knows how to pronounce this Holy Name,zaidi ya kuliandika tu hivyo,YHWH au ukipenda unaweza kuliandika kwa tetragramaton(ndivyo inavyotakiwa haswa).

Na waislamu wao kupitia uarabu,wameamua kubaki na lile jina la zamani sana ambalo kimantiki ni title,yaani Mungu,..Allah(from El).

Kuna story kwamba Allah ilitumika kabla ya uislamu katika imani za wapagani wa Meccah,hii ni kweli ila tu cha msingi ni kwamba maana ya neno hilo ni Mungu/mungu,hivyo ni rahisi kuchanganya Allah yule wa wapagani ukadhani ndio huyu wa Qur'an,hapo ni kazi ya waislamu kuudhihirishia ulimwengu kuwa Allah wao si yule wa waarabu wapagani bali ni yule wa Ibrahim.
 


Soma 2 Wakorintho 4:4 Uone nani mwingine anayeitwa Mungu..... Halafu nitaomba unijibu baada ya kusoma..
 
KIKOSIKAZI@ kwa mwenye kutaka kuelewa ameelewa kwa text yako .big up sannnnnna:thumbup::thumbup:
 

Hakuna Buzi la bura humu.
Nenda Kule Chit chat ukatafute mume!
 
emmanuel = Mungu pamoja na wanadamu = yesu ambaye freemasons wanamuita adonai
 

huyu na JEHOVA watakuwa tofauti kabisa.
 

Ukiisoma vizuri hiyo mistari, utaona ya kuwa kwa mfano apo kwenye kutoka 17:15,musa akapaita mahali pale yehova nisi, so hayo sio majina ya Mungu ni majina ya mahali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…