Majibu ya mawaziri wetu!!!

mpemba mbishi

JF-Expert Member
Nov 27, 2011
1,132
183
TANZANRA NI NCHI YA MAAJABU SANA! HEBU ANGALIA MFANO MDOGO WA MAJIBU YA WATU TULIOWAPA DHAMANA YA KUTUONGOZA!!

MWANDISHI: Mheshimiwa...ASALAAM ALYKUM?

WAZIRI: Waaleikum salaam!

MWANDISHI: Mheshimiwa hivi punde tumepata habari kuwa jengo maarufu hapa
Mjini Unguja hapo maeneo ya FORODHANI lijulikanalo kama HOUSE OF WONDER limeanguka ukuta wake
mmoja upande wa Kusini ya jengo hilo, vipi habari hizi unazithibitisha vipi Mheshimiwa?

WAZIRI: Hahaha... nyinyi waandishi kwa kuzuwa bwana,!! Sikiliza ndugu
mwandishi hilo jengo ni kubwa sana kwanza napenda uwelewe na
ukawaambie wenzio hivyo, na ukisikia jambo lazima ulipime ndugu yangu, ni kweli kwamba kuna tukio
la kudondoka tu sehemu ya ukuta wa jengo hilo na tena sio kusini ni Kaskazini na ni ukuta mmoja tu sio jengo, SASA NASHANGAA SANA NYINYI
WAANDISHI MNAVYOPENDA KUKUZA MAMBO KAMA HAYA HEHEHE! NAKUMBUKA HATA MMOJA WENU SIKU ZILE ALINIPIGIYA SIMU ETI
AKANIAMBIA MELI YA SKAGET SIJUI WALIOKUFA NI WATOTO 13 NA UKWELI NI 12 TUUU..nashangaaa mie!! .. LAKINI NYINYI NDIO KAZI YENU
KUANDIKA VITU MSIVYOVIJUWA BWANA HEHEHE, AU NA YULE MWANDISHI MWENZAKO MWENGINE ANANIULIZA
KWANINI WANAWAKE WENGI AMBAO NI 36 WALIFARIKI KWENYE AJALI YA SPICE ISLAND? huu ni uwongo
MTUPU... kabisa mwandishi wakati ajali ile wanawake waliofariki ni 20 TU!!!

MWANDISH:I Lakini Mheshimiwa tumesikia kuwa
hata baadhi ya Wawakilishi
walitowa tahadhari juu ya
uwezekano wa majengo hayo kuwa hatarini kwa vile macho ya serikali kwayo hayakuwa makali Muheshimiwa na hili unalitazama vipi?

WAZIRI: hahahahahah,, HAO WANATAFUTA UMAARUFU WA KISIASA TU NDUGU
MWANDISHI!! Sisi tanafanya kazi zetu siku zote kwa umakini mkubwa na tena tulisema macho yetu makali
kuliko wao hao, lakini pia kama hilo halitoshi tukawaahidi kuyashuhulikia maana ndio kazi ya serikali eti au vipi!! ???

MWANDISHI: Kwa hiyo mtachukuwa hatuwa gani
kwa hili na majanga mengine mfano wa hili Mheshimiwa?

WAZIRI: BILA SHAKA SERIKALI INAFANYA KILA LIWEZEKANALO KUHAKIKISHA HAYA
YANATAFUTIWA UFUMBUZI NA TUKO MBIONI KUTAFUTA SULUHISHO YA YOTE

AHSANTE....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom