Habari zenu wanaChitchat....
Ni miaka mingi imepita tangu nilipoondoka kijijini kwetu, na sababu ya kufanya hivyo ilikuwa ni baada ya mkasa wa kifamilia ulionitukia nyumbani.
Hii ilikuwa ni mara tu baada ya Vita ya Kagera kuisha, maisha ya wakati huo yalikuwa ni magumu haswa kwa sisi vijana tuliotoka vitani.
Nakumbuka mara tu baada ya kumalizika kwa vita, nami nikiwa mkoani Kagera nilikutana na binti mrembo mwenye asili ya Kinyarwanda ambaye tulipatana tuoane na nikarudi naye kwetu.
Wazazi wangu na dada zangu walipinga sana lakini msimamo wangu usiotetereka na mapenzi ya dhati kwa binti huyo ndivyo vilikua nguzo muhimu ya mimi kuendelea kuishi naye kama mke.
Wakati narudi kijijini na mpenzi wangu tayari alikuwa ni mjamzito wa kama miezi miwili hivi, na ulikuwa ni ujauzito wa watoto mapacha(Hili sikulijua wakati huo).
Baada ya miezi tisa mke wangu alipatwa na uchungu, kwa bahati mbaya siku hiyo ilikuwa ni siku ya gulio kijiji cha jirani hivyo mimi sikuwepo.
Msaada pekee alioupata mke wangu ni kutoka kwa wifi zake na mama mkwe ambaye ndiye mama yangu wa kunizaa. Alitafutwa kungwi na shughuli ya kumzalisha mke wangu ikaendelea.
Mungu ni mwema, mke wangu alijifungua mabinti mapacha wakiwa na siha njema kabisa tena wenye kufanana kweli na baba yao ambaye ndio mimi.
Hapo awali nilidokeza kuwa mke wangu hakuwa amekubalika sana kwenye familia yetu, hivyo mara baada tu ya kujifungua na kupata nguvu familia ikamdanganya kuwa pacha mmoja amefariki na mmoja yupo hai.
Kumbe haikuwa hivyo, mama yangu kwa kushirikiana na dada zangu walimchukua pacha mmoja na kwenda kumficha nia ikiwa ni kumpatia binamu yetu mmoja ambaye alikuwa hajajaliwa mtoto.
Miaka imepita sasa na binti amekuwa mkubwa wa kuweza hata kuposwa. Kabla mama yake hajafariki(ambaye ndiye binamu yangu), aliacha barua yenye kumueleza mkasa mzima na kumuelekeza wapi kwa kumpata baba yake.
Binti huyu jina lake anaitwa
Passion Lady na ndiye pacha wa
WiseLady, dada wa
charminglady na
sweetlady.
Mpenzi
measkron, njoo tumpokee mwanetu amerudi nyumbani baada ya kumpoteza kwa miaka yote hii.
NB:
Nimeweza kuthibitisha hilo kutokana na majibu ya Mkemia mkuu wa Serikali na majibu yalikuwa POSITIVE.
Passion Lady karibu nyumbani kipenzi,
measkron ni mama yako wa kukuzaa na wala sio mama mdogo.