Nimepima DNA (kwa mkemia mkuu) ya mtoto mara 3 ili kuwa na uhakika zaidi na mara zote majibu yameleta kuwa mimi ni baba halisi wa mtoto kwa asilimia zote mia.
Baada ya miaka 7 kumetokea mwanaume anasema yule ni mtoto wake na tumejaribu kulizungumza suala hili kwa ushahidi wa vipimo vya awali vya DNA bila mafanikio na yeye analazimisha kufanya kipimo cha DNA tena upya. Inavyoonekana ana uhakika mkubwa wa suala hili kiasi cha kunipa mawazo mengi.
Maswali ninayojiuliza ni kwamba,
1. Je ikitokea kipimo cha mara hii kikaonyesha mtoto ni wake, naweza kudai fidia kwa mkemia mkuu kwa kunipa majibu ya uongo mara zote tatu za mwanzo?
2. Je ikionekana mtoto sio wangu naweza kudai fidia kwa mke wangu aliyesaliti ndoa bila kunieleza ukweli kuhusu mtoto?
3. Ikioneka mtoto sio wangu naweza kuachana na majibu ya sasa na kuendelea kuamini majibu yale ya mara zote za mwanzo yaliyosema mimi ni baba halisi?
4. Je naweza kumfungulia mashitaka huyu mwanaume kwa kutembea na mke wangu na kumpa ujauzito kama ni kweli ni mtoto wake?