Majibu mujarabu kwa Mdude Nyagali wa CHADEMA kuhusu tozo ya motor vehicle

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,375
Wadau, amani iwe kwenu.

Jana niliona mjadala wa kitoto ulioanzishwa na Mdude Chadema Nyagali Mwanachama wa CHADEMA. Mjadala huo ulianza kwenye Ukurasa wa Facebook wa Mdude Chadema Nyagali na kusambaa kwenye mitandao mingine. Katika mjadala huo ambao aliuita mazungumzo baina yake na dereva wa Bus linalotoka Dar es Salaam hadi Sumbawanga, alijenga hoja kuwa Tozo ya Motor Vehicle iliyopendekezwa kufutwa na Waziri wa Fedha, Philip Mpango ni nafuu zaidi kuliko inayopendekezwa.

Katika mjadala huo, Mdude alifahamishwa na dereva wake kuwa kwa siku anatumia lita 400 kutoka Dar es Salaam hadi Sumbawanga kwa Bus aina ya Yutong. Tena aliupa uzito mjadala huo kwa kuweka picha ya Bus la Shabiby ambalo sina hakika kama linafanya safari hiyo. Kwa maelezo yake, kwa kuwa gari linatumia lita 400, kwa hali hiyo hadi Sumbawanga Busi hilo litalipa motor vehicle ya shilingi 16,000 kwa maana 400 x 40. Kwa Mwezi atalipa Motor Vehicle ya shilingi 16,000 x 30 = 480,000 na kwa mwaka shilingi 480,000 x 12 = 5,760,000.

Mjadala huo ulivuta hisia za wafuasi wa CHADEMA ambao nao bila kutumia akili ipasavyo, wakaanza kushangilia na kujiona wameshinda. Ni kwa bahati mbaya sana Mdude CHADEMA hajawahi kumiliki hata pilipiki kwa hiyo hajui lolote kuhusu consumption ya mafuta kwenye magari. Binafsi nilijiuliza, je umbali wa kutoka Dar es Salaam hadi Sumbawanga unaweza kutumia lita 400? Kama ni hivyo, je abiria wa huko wanalipa nauli kiasi gani? Twende taratibu.

Mabasi mengi yanatumia wastani wa lita moja Diesel kwa kila kilomita 7 hadi . Na kwenye barabara za Highway, consumption ya mafuta ni tofauti na kwenye maeneo ya mijini. Kwa maana hiyo lita 400 anazotuma huyo dereva ukizidisha mara 7 gari hilo litalazimika kutembea kilomita 2800 ili kumaliza mafuta hayo yaani 7 x 400 = 2,800. Je Umbali wa kutoka Sumbawanga hadi Dar es Salaam unafika kilomita hizo?

Haya tufanye gari hilo ni mkweche kiasi cha kutumia kilomita 5 tu kwa lita moja. Maana yake ni kwamba gari hilo litalazimika kutumia kilomita 2000, hadi kumaliza mafuta yote yaani 5 x 400 = 2000. Je umbali wa kutoka Dar es Salaam hadi Sumbawanga unafikia kilomita 2000?

Basi tuseme Tank la Mafuta la Gari hilo linavuja na kwa hali hiyo hutumia lita moja kwa kila kilomita 3 tu. maana yake ni kwamba 3 x400 ni sawa na kilomita 1,200. Je umbali wa kutoka Sumbawanga hadi Dar unafikia kilomita 1,200?

Baada ya kushirikisha ubongo wangu, nilijiuliza maswali haya? Je Mdude Chadema ana uelewa wa matumizi ya mafuta kwenye magari? Au huyo Dereva anampiga cha juu bosi wake na ndo maana akataja kiasi kikubwa cha mafuta?

Ukweli ni kwamba, Motor Vehicle iliyopendekezwa inapunguza sana gharama na hasa kwa sisi tunaoishi huku mikoani. Mathalan, mimi nikijaza full Tank huku Songea natumia wastani wa siku 18 hafi 25 hadi kwenda tena kituo cha mafuta. Kwa maana gari langu aina ya Toyota Harrier ina CC 2160 na ujazo wa Tank ni lita 65. Na inatumia wastani wa kilomita 8 kwa lita moja. Kwa maana hiyo, kwa lita 65 ili ziishe zote ingawa haijawahi kutokea, nitalazimika kutembea kilomita 520 ambayo kwa mzunguko wa mji wetu wa Songea nitatumia wastani wa siku 18 hadi 25 kumaliza na kama ninazurura sana nitatumia siku zisizopungua 10.

Sasa twende taratibu, lita 65 x 40 = shilingi 2,400. Kwa maana hiyo kila siku 15 nitalipa Motor Vehicle ya shilingi 2,400 tu. kwa Mwezi nitalipa shilingi 4,800 tu na kwa mwaka nitalipa shilingi 4800 x 12 = 57,600 tu. hii ni pungufu ukilinganisha na shilingi 200,000 ninayolipa sasa. Yaani nitaokoa shilingi 142,400. Na hapa chukulia kama gari inatembea siku zote. Kama kwa nyakati kadhaa gari halitumiki maana yake ni kwamba kiasi cha Motor Vehicle nitakacholipa kitapungua.

Kwa wale wa Dar es Salaam ambao foleni husababisha matumizi makubwa ya mafuta, twende na mfano huu. Kwa wanaoishi Mbagala, ama Vikindu, ama Kibamba, ama Bunju na wanafanya kazi katikati ya Jiji, hutumia wastani wa lita 70 kwa wiki. Maana yake ni kwamba Motor Vehicle atakayolipa mtu huyo ni kama ifuatavyo; Kwa wiki itakuwa 70 x 40 = 2,800. Kwa mwezi itakuwa 2,800 x 4 = 11,200 na kwa mwaka itakuwa shilingi 11,200 x 12 = 134,400 tu. kwa hali hiyo, mtu mwenye gari kama langu ataokoa shilingi 65,600 kila mwaka iwapo tozo mpya ya Motor Vehicle itapitishwa. Hizi ni hesabu za kitaalam na wewe kama unamiliki gari unaweza kufanya hesabu zako ili kujua utalipa kiasi gani kwa wiki, mwezi na mwaka. Uzuri wa tozo pendekezwa ni kwamba inalipwa kulingana na jinsi unavyolitumia gari lako. Kama weekend una kawaida ya kupumzika basi utaokoa kiasi kikubwa sana cha fedha. Na kama una kawaida ya kupanda daladala siku moja moja ili kuchangamana na jamii kama nifanyavyo mimi basi utaokoa fedha nyingi sana.

Niwasihi Watanzania, tusimezeshwe tu kila kitu. Wengine wanaotumezesha hawajui lolote. Tutumie akili alizotupa Mungu ili kuchanganua mambo.

Nawasilisha
 
naona mmeitoa whatsapp na kuileta huku!!

kwa kifupi kodi imepanda kutokana na matumizi yako ya barabara!! very fair

pia hakuna kukwepa kodi, maana sticker mlikuwa mnachongewa na akina mangi na wahuni wengine, hamkwepi tena

tatu hakuna mahali kuna mtu anajua standard road license....so hata kama milioni kumi sawa tu

wanachofurahia hao jamaa ambao unawaona wajinga ni kulipa taratibu!!! hawaumiii, hiyo ya kwa mkupuo sh hata laki 3, inauma!!

this is brilliant idea no matter what!!

unatoka tegeta mpaka kigogo na lita zako nne kwa siku, mwenzako anatoka dar kwenda bukoba!! hlafu mwisho wa mwaka mlipe road license sawa?? seriously??

hii ya sasa imekaa vizuri na mtaumia weee

mkiona mmekasirika sana, tumia baiskeli au guta!!
 
Lizaboni wewe kama hujui kitu kaa kimya mkuu hiyo bus unayoisema wewe inatembea juu ya meza? Hakuna milima?.tena huyo Mdude katoa kwa bus kwa Truck tutaumia zaidi nawatuma vijana wangu Congo natumia litres 2200
 
Muhimu sana kujua uhalisia wa matumizi ya mafuta ktk gari au pikipiki vinginevyo tutalishana matango pori.
 
Nikitoka Dar kwa kagari kangu nitatumia zaidi ya lita 200 kwenda hapo Mbeya tu,sembuse Basi la abiria??Ifike mahali tuwe wakweli.Ninauhakika kwamba basi linatumia kati ya 300-400 ka trip moja,tusiwe wapenda kukosoa bila kujua reality.

Pili yake kwenye hiyo arobaini tukumbuke kila tutakachonunua kinalipa Road licence,ni kweli ilikuwa inaumiza lakini kwa sasa itaumiza zaidi.Tulitakiwa tupate mbadla wa kuifanya kodi hii kutolipiwa kwa magari yakiwa ni scraper,mabovu kwa maana kwamba hayatembei,yameibiwa nk nk.

Lakini kwa hii mh!
 
naomba lizaboni unijibu hili swali Na pia unijibu kwa ufasaha..


"je tozo hii inapandisha au kupunguza nauli kwa mwananchi wa kawaida ambae Hana gari?"
 
..mkuu, siasa zetu za afrika unadhani wanasiasa wanajali utaalamu basi? Ni mwendo wa kutiririka tu ili mradi kusikika na kupata kiki.
NAKUREKEBISHA MKUU KIDOGO HAPO, MATUMIZI YA MAFUTA KWENYE GARI WAKATI MWINGNE HUTEGEMEA NATURE YA BARABARA. BARABARA ALIYOITAJA MHUSIKA HAPO INA SIFA YA MILIMA MINGI INGAWA SINA HAKIKA KAMA INATUMIA LITA 400 SIJUI.
NB: hapo tunaopaswa kulalamika ni wale tutakaolipa hyo license kwenye majenereta, vibatari, mitambo, mashine, n.k
Maana hyo sh. 40 imeingzwa kwenye mafuta ya taa, diesel na petrol
Ila wenye magari watakuwa wamepunguziwa mzgo.
 
Muongo wewe, basi gani linatumia Lita Saba kwa kilometa moja?
Gari ndogo ndio inaweza kutumia Lita Saba kwa kilometa moja.
Katika utafiti uliofanywa, Bus la Volvo ndio linaongoza kwa kutumia mafuta kidogo. Linatumia Lita 26 kwa kila kilometa 100. Hiyo ina maana linatumia chini kidogo ya Lita 4 kwa kila km moja. Mahesabu hayo ni kwa mwendo wa wastani wa 60km/h.

Kumbuka ukiendesha gari kwa speed kubwa linatumia mafuta zaidi. Ukiendesha kwa speed ndogo Sana pia linatumia mafuta zaidi. Speed ambayo inaleta matumizi mazuri ya mafuta no hiyo ya around 60km/h.

Kwa Tanzania mabasi yanaenda wastani wa 100km/h.
Na ubaya huo wa barabara, sitashangaa basi likila Lita moja kwa kila km 2.
 
Naona unapiga hesabu za kimakinikia hapa, badala ya kujibu na kufafanua bajeti unamjibu Mdude, makinikia yanawaharibu sana, kumbe mmekaa watu zaidi ya kumi mmejifungia usiku mzima nilijua mnajadili mambo ya maana kumbe ndo mmetoka na haya mashabo
 
Back
Top Bottom