Majibu Kura ya Maoni isiyo Mizengwe

Majibu Kura ya Maoni isiyo Mizengwe

Nyambala

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2007
Posts
4,465
Reaction score
1,172
Wiki iliyokwisha tulishuhudia tafiti mbalimbali kuhusu kura za maoni, nyingine zikisema Magufuli kidedea na nyingine Lowassa kidedea. Zote zilipingwa na kuungwa mkono kwa hoja mbalimbali.

Lakini kuna namna tunaweza kuondoa ubishani huu kwa kupiga kura ya maoni isiyo na mizengwe hata kidogo, haina gharama na unaipiga popote pale kazini, hospitali, nje ya nchi na hata jela. Unaipiga ukiwa unaendelea na kazi yako yoyote ile uwe unapiga debe muda huo, unalima, unasubiri basi kituoni, upo kanisani, msikitini, hekaluni hata ukiwa chini ya mti ukiabudu miungu ya jadi.

Kupiga kura hii hatuhitaji ruhusa, na wala zile sheria za kipuuzi kuhusu masuala ya takwimu hazikugusi. Ni kura ambayo wale waliozoea kushawishi kwa kununua hawataweza kuimudu maana inabidi ununue wananchi nchi nzima. Kura hii haina mambo ya sampuli na kuna uwezekano ikapigwa na watu wengi kuliko hata ile ya tarehe 25 Oktoba. Ni kura inayopigwa mjini na vijijini, vitongojini, milimani, visiwani n.k. Uzuri wa kura hii inaweza kuandaliwa na kuratibiwa na CCM au UKAWA na matokeo yake bado yakakubalika, "amazing eeh?"

Kura hii inapigwaje???? Na inapigiwa wapi??

Ni hivi basi viongozi wa UKAWA watutangazie siku, nzuri zaidi tarehe 22 au 23 Oktoba ili tupate muda wa kujadili matokeo kabla ya tar. 25, au hata wiki kabla. Mtu yeyote kuanzia pemba mpaka Nkasi, Tandahimba mpaka Nansio, Katavi mpaka Handeni anayesapoti ukawa na EL. avae vazi la rangi fulani (Nyekundu, au Bluu, Nyeupe etc), au hata kofia, au scarf, leso, chochote kile kitakachoonyesha uungaji mkono wa harakati hizi. Nimesema UKAWA nikijua CCM kamwe hawawezi kujaribu kura hii.

Kwa kufanya hivyo basi tutakuwa tumepiga kura ya maoni kwa sauti moja itakayowafanya hata wale wanaooandaa bao la mkono wafikiri mara mbili mbili. Wanaojiliwaza majukwaani na mitusi waione hali halisi lakini pia kuondoa hali ya unyonge wa hisia kwa baadhi ya wanaharakati. Kura hii itasaidia kutupa picha halisi ya mwenendo wa kampeni ambazo kila mgombea anadai ni mshindi.

Hivyo basi tujiandae tupige kura ya maoni isiyotumia sauti, peni wala mihuri na matokeo tutayaona.

Je uko tayari?? Muulize na mwenzio, pia jirani yako.
 
Kaka, nikupongeze kwa wazo zuri sana. Familia yangu yote imeafiki na tuko tayari wa kura hii. napendekeza tuvae nguo nyeupe siku hiyo!!!
 
Back
Top Bottom