Mzee23
JF-Expert Member
- Oct 9, 2014
- 1,742
- 3,673
Habari wana jF!
Jambo moja ni hakika, MAJI ndilo hitaji kubwa zaidi la wananchi wanaoitwa 'wanyonge' hasa wa vijijini baada ya mazao ya Chakula. Nimeishi kijijini nimeshuhudia hili. Wakati wa Kiangazi ni mateso yasiyoelezeka! Kukesha kwenye chemchemi za maji, kwenda umbali mrefu hata kijiji cha sita kutafuta maji! N.k n.k
Kwa miongo mingi,toka uhuru hadi leo hadithi za wanasiasa wetu ni zilezile, awamu hii watasema ufinyu wa bajeti, awamu nyingine watawalaumu wazabuni wa miundombinu ya maji vijijini na awamu nyingine itasema upembuzi yakinifu umekamilika n.k n.k huku 'wanyonge' wakiendelea kutaabika!
Maoni
Kutokana na umuhimu na unyeti wa MAJI, Uchaguliwe mwaka mmoja wa fedha ambao Taifa litatangaza ukosefu wa maji kuwa hali ya dharura(National emergency) ambapo bajeti nzima ya maendeleo ya mwaka huo itaelekezwa kwenye maji.
Kwamba ibaki tu pesa ya kulipia mishahara ya watumishi na dharura zingine huku pesa za maendeleo za wizara zingine zote ipewe wizara ya maji, mipango mingine yote isimame.
Hizi trilioni zitakazopatikana, penye uwezekano wa kuvutwa maji toka vyanzo vikuu kama maziwa, yavutwe, penye maji ardhi visima vichimbwe n.k lengo kuhakikisha kila mita 100 toka kaya ina maji.
Barabara za rami,changarawe, umeme vinavyohangaikiwa na watawala sasa ni ANASA kwa wananchi 'wanyonge' wa vijijini. Wao wakipata MAJI huku mazao yao ya chakula yamekubali basi.