Maji yanapungua Bonde la Mto Pangani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maji yanapungua Bonde la Mto Pangani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jun 6, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]Mto Pangani ambao unaelekea kupoteza uhalisia wake kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.  MAJI ya Bonde la Mto Pangani (PBWO) yanategemewa na mikoa ya kaskazini mwa Tanzania na baadhi ya maeneo ya nchi jirani ya Kenya katika shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo kilimo, uvuvi, matumizi mbalimbali ya nyumbani na uhifadhi wa mazingira.

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa PBWO, Hamza Sadiki anasema pamoja na umuhimu huo bonde hilo linaathiriwa na mambo mengi kubwa likiwa ni umaskini. Anasema asilimia 36 ya Watanzania ni maskini ambao unawazuia kuwekeza katika teknolojia yenye ufanisi.

  Anasema maskini vijijini wanategemea moja kwa moja maliasili kama zipatikanazo katika mito ambazo ni rahisi kuathirika kutokana na kushuka kwa ubora wa uhai wa mito husika.

  Ubora wa maji pia unapungua kutokana na matumizi mabaya ya ardhi, uchafuzi utokanao na majitaka na taka ngumu. Hiyo ni mbali ya kuingia kwa maji-chumvi katika lango la mto kutokana na kupungua kwa kiwango cha mtiririko na wingi wa maji mtoni.

  Changamoto nyingine ni ya uhaba wa maji ambao unaziathiri sekta zote za kiuchumi na kusababisha kushuka kwa uzalishaji kiuchumi wakati wa kiangazi.

  Anasema uzalishaji katika kilimo unashuka au haukui kutokana na uhaba wa maji lakini, pamoja na hali hayo, anatoa matumaini mapya akisema mipango zaidi ya kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu za maji inaandaliwa katika uwanda wa juu wa Kaskazini mashariki na maeneo ya chini ya Mto Pangani.

  Lakini anaonya kwamba uhaba wa maji ya matumizi ya nyumbani unaotokea katika Bonde lote la Mto Pangani huenda ukawalazimisha watu kutegemea zaidi maji ya chini ya ardhi na uvunaji wa maji ya mvua.

  Kuhusu ugavi wa maji, anasema bonde hilo linakabiliwa na uhaba mkubwa. Maji yaliyopo yanapungua kutokana na mabadiliko ya tabianchi na kushuka kwa ubora wa eneo-bonde. Mahitaji yanaongezeka kutokana na idadi ya watu, ukuaji wa uchumi na matumizi mapya ya ardhi.

  Kiasi cha maji kilichopo hivi sasa katika mfumo wa mto kimegawiwa kuzidi kiwango na kusababisha migogoro miongoni mwa watumiaji wa maji. Ardhioevu na mito inakauka.

  Bonde la Mto Pangani lina eneo la kilometa za mraba 43, 650 na asilimia tano ya eneo hilo ipo nchi jirani ya Kenya. Sehemu iliyobaki imegawanyika katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Tanga.

  Mto Pangani unatokana na vijito vidogo vinavyoanzia upande wa kusini mwa Mlima Kilimanjaro ambao ndiyo mrefu kuliko yote barani Afrika na milima Meru ambayo kwa pamoja hujikusanya na kuunda Mito ya Kikuletwa na Ruvu.

  Mito hiyo hujiunga na kuunda Mto Pangani, ambao hupita ndani ya mbuga kame za Masai na kupokea mtiririko wa maji kutoka safu ya Milima ya Upare na Usambara (vijito vya Mkomazi na Luengera) kabla ya kufika kwenye lango la mto na hatimaye kuingia Bahari ya Hindi katika Mji Pangani. Mto huo una urefu wa kilomita 500.

  Mabadiliko ya tabianchi katika eneo la Bonde la Mto Pangani yanahusiana na hali ya ‘Topografia.’ Sehemu ya tambarare ya chini katika maeneo ya kusini-mashariki pembezoni mwa mpaka wa bonde, hali ni ya baridi na unyevu.

  Sehemu za miinuko kwenye miteremko iliyopo juu ya maeneo yenye misitu katika Milima Meru na Kilimanjaro, tabianchi ni ya ‘kiafro-alpine’ na hupata mvua zaidi milimita 2,500 kwa mwaka.

  Wastani wa mvua kwa mwaka huongezeka kuelekea kusini kufuata safu ya milima na viwango hutofautiana kati ya milimita 650 kwa mwaka katika Milima ya Pare Kaskazini na Kusini hadi milimita 800 kwa mwaka katika Milima ya Usambara Magharibi na milimita 2,000 kwa mwaka katika Milima ya Usambara Mashariki.

  Kuna takriban zoni nane za kijamii na kiuchumi za aina moja ambazo zimewekwa katika vikundi kwa kuzingatia matumizi ya ardhi na uhusiano wa mifumo ikolojia ya majini.

  Zoni hizo ni Uwanda wa Juu wa Kaskazini, Uwanda wa Juu wa Mashariki, Kinamasi na Maziwa, Kinamasi ya Kirua, Ukanda kame wa upande wa magharibi, Ukanda kame wa upande wa kusini magharibi, Nyanda za chini na Pwani zenye unyevu mwingi.

  Mito katika Bonde la Mto Pangani inaweza kugawanywa katika zoni tisa zenye mfumo wa ikolojia unaofanana. Hizo ni mlima wenye mbubujiko mkubwa wa nguvu za maji, mlima wenye vijito, safu za milima zilizokarabatiwa, Kinamasi na Maziwa, Kinamasi ya Kirua, safu za chini ya mlima na mto uliokomaa bondeni.

  Watu wa jamii ya Wachagga wamekuwa wakiishi kwenye miteremko ya Mlima Kilimanjaro kwa takriban miaka kati ya 300 na 450.

  Mnamo miaka ya 1940 wingi wa shughuli za kilimo za Wachagga ziliongezeka kwa kasi kubwa kiasi kwamba inasemekana, (Johnston 1946) kulikuwa na sehemu ndogo ya ardhi iliyobaki kwa matumizi ya malisho. Mifugo mingi ilibidi ilishwe majumbani.

  Wachagga hawakuweza kuendeleza shughuli zao za ukulima maeneo ya juu mlimani kwa sababu yalikuwa yametengwa kwa ajili ya hifadhi ya misitu na hawakuweza kwenda katikati ya mlima kwa vile maeneo hayo nayo yalitengwa kwa ajili ya wazungu walowezi.

  Kutokana na sababu hizo za kuongezeka kwa kasi kubwa ya kilimo, Wachagga walibuni utaratibu wa kutumia mfumo wa mfereji wa kuchukua maji kutoka kwenye vyanzo vya asili na kuyaleta kwenye mimea yao.

  Utaratibu huo ambao unasemekana ulianzishwa karne ya 18 (Gillingham 1999), unadhaniwa kuwa mfumo wa zamani na mkubwa wa umwagiliaji katika Afrika. Usimamizi na utawala wa kijamii na mfumo mzima umesaidia kuimarisha miundombinu ya maji; wajumbe wa bodi za mifereji walitegemewa kusaidia kuidumisha, wasiokuwa wajumbe walilipa ada ya kuchepusha maji (ICUN 2003).

  Hivi sasa Bonde la Mto Pangani lina zaidi ya mifereji ya asili 2,000 ambayo inahusisha sehemu kubwa katika shughuli za umwagiliaji ndani ya bonde.

  Mifereji mingi ya asili haijabadilishwa kwa zaidi ya karne na mingine haifanyi kazi kwa ufanisi. Inakisiriwa kwamba kiasi cha asilimia 85 ya maji yanayochepushwa kwa ajili ya umwagiliaji huenda yanapotea.

  Kutokana na kuongezeka kwa ushindani wa matumizi ya rasilimali za maji, kuongeza ufanisi katika umwagiliaji kunapewa kipaumbele cha hali ya juu kwenye juhudi za kuanzisha miradi mipya, kama vile Mradi wa Benki ya Dunia uliogharamia Mradi wa Uboreshaji wa Kilimo cha Umwagiliaji cha Wakulima-wadogowadogo na Shirika la Umwagiliaji wa Asili na Mpango wa kuboresha mazingira (TIP).Maji yanapungua Bonde la Mto Pangani

  NaulizaWizara inayohusika na Maji inalichukulia Vipi Tatizo hili la kukauka Kwa Maji? Tanzania inaelekea kwenye jangwa baada ya mika kumi ijayo Tanzania kutakuwa kama Uarabuni hakuna maji ni Ukame Mtupu Tuwe Macho Wananchi jamani.
   
Loading...