Maji yaliyotwama huchafua watu

Maji yaliyotwama huchafua watu

pambe samanini

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2015
Posts
430
Reaction score
224
Mvua zinaponyesha mahali mbalimbali maji yake mengine hunywea chini ya ardhi, mengine hutelemka kuelekea bondeni kama mito, maziwa na bahari lakini yaliyo mengi pia hutwama.

Maji yaliyotwama yakikaa muda mrefu hutengeneze uchafu, pengine matumizi yake huwa machache sana, na pengine kutotumika kabisa, haishangazi kuona wazazi wakikataza watoto wao kuongelea katika maji yaliyotwama kwa sababu ya uchafu wake na kutokuwa mazuri kwa afya ya binadamu. Wakati huo watu wakubwa huvaa hata gumboots pamoja na gloves ili wasiguse maji hayo.

Kwa sasa inashamgaza kuona watu wazima wasomi/ taaluma na vyeo vyao na utu wao wanapita kwenye maji hayo peku peku huku gumboots zao zikiwa mikononi na gloves ndani ya gumboots kwa kigezo kuwa viatu(gumboots )navyo huchakaa na kushuka uchafu, hivyo bora kutunza viatu( gumboots )kwa afya yake na mtumiaji wake.

Watu hao watumiao na kuvuka maji machafu peku peku yakiwapata ya kuwapata wanatumika gharama kubwa kujitibisha afya zao, maneno kwao ya kulogwa ni mengi kuliko kujilinga wenyewe. Ni nani awezaye kukaa na watu wa namna hii?

Wakitengwa na watu wao hulalamika kuwa watu Wana wivu tu, wakiugua magonjwa haya ya tumbo tumbo nk husema wamelongwa.

Kwa.nini watu Hawa wapite katika maji yaliyotwama siku nyingi huku viatu (gumboots) zao wakiwa nazo mikononi?. Wakiitwa wachafu nao huwashangaa wawaitao, wakitengwa na watu wao hulazimisha kuwa sehemu ya jamii kwa nguvu zao zote, watatumia watu wenye sifa ili wapewe sifa, watumia pesa kujikosha na kukoga watu kuwa wanawapenda na kujali jamii Yao lakini hakika Yao hawa watu hawafai kujumuika na watu maana wamepita na kutumia maji yaliyotwama siku nyingi, wamepoteza sifa za kuwa sehemu ya jamii maana walionywa athari za maji hao kuyatumia lakini wakaona Bora wayatumie waone kama hayafai, sasa wanahitaji msaada wa jamii wa nini?
 
Back
Top Bottom