Maji ya bahari kubadilishiwa matumizi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maji ya bahari kubadilishiwa matumizi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Nov 20, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 20, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  MAJI ya bahari nchini yanaweza kubadilishwa na kuanza kutumiwa kwa shughuli zingine zikiwamo za kunywa na kufanyia usafi, imebainishwa.

  Hayo yalisemwa jana na Kaimu Balozi wa Hispania nchini, Carolina de Manuels Alvares, alipokutana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Abedi Karume.

  Balozi Alvares na Balozi Staffan Herrstrom wa Sweden walikutana na Karume na kwa niaba ya Jumuiya ya Ulaya (EU) walimweleza kufurahishwa kwao na mazungumzo kati yake na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad na kufungua ukurasa mpya wa kisiasa Visiwani.

  Kwa upande wake Alvares alisema nchi yake iko tayari kufanya utafiti wa kuyabadilisha maji ya chumvi na kutumika katika shughuli nyingine kutokana na wao kufanikiwa katika utaalamu huo.

  Herrston ambaye aliongoza ujumbe wa mabalozi hao wa EU alisema hatua ya viongozi hao wa CCM na CUF kukutana ni mwanga mzuri wa maendeleo ya Zanzibar na wananchi wake.

  “EU tumefurahishwa na hatua hiyo itakayoendeleza ushirikiano na uhusiano mwema wa wananchi wa Zanzibar na kusukuma mbele juhudi zao katika kujiletea maendeleo,” alisema.

  Alisema Sweden imekuwa ikishuhudia uendelezaji wa miradi inayofadhiliwa na nchi hiyo ambayo wananchi wa Unguja na Pemba wamekuwa wakiitekeleza kwa pamoja kwa ufanisi bila kujali itikadi za kisiasa.

  Pia alimpongeza Rais Karume kwa kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki cha Dar-es-Salaam.

  Rais Karume aliueleza ujumbe huo kuwa mazungumzo yaliyofanywa kati yake na Katibu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, ni juhudi za kuzidisha maelewano kwa wananchi na vyama vyao vya siasa na kuweka mustakabali mwema wa nchi.

  Alisema Zanzibar ina historia ndefu katika kuimarisha amani, utulivu na kuwaweka watu wake kuwa wamoja hali ambayo imeifanya kupiga hatua kubwa ya kimaendeleo.

  Alisema wananchi wa Zanzibar wana utamaduni wa ushirikiano ambao umewawezesha kuishi pamoja, kushirikiana, kusaidiana na kufanya kazi mbalimbali za maendeleo Unguja na Pemba bila kujali itikadi, na washirika wa maendeleo wanalielewa hilo.

  Kuhusu Daftari la Kudumu la Kupiga Kura, Rais Karume alisisitiza kauli yake kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itahakikisha kila mwenye sifa ya kujiandikisha anafanya hivyo.

  Alieleza kuwa azma ya EU kufanya utafiti juu ya mabadiliko ya hali ya hewa visiwani hapa itaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kutokana na hali hiyo kuathiri juhudi za wananchi katika kilimo.
  http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=4468
   
 2. A

  AM_07 Member

  #2
  Nov 20, 2009
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 74
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ni gharama sana, haitakuwa na faida kwetu, elewa tatizo la bongo sio chanzo cha maji, tatio ni usambazaji, (distribution and sanitation), tuna maji masafi ya kutosha sana, desalinization ni project ya hela nyingi mno
   
Loading...