Tangu kukamilika kwa marekebisho ya mfumo wa umeme, hali imekuwa tete. Karibu kila siku, hasa nyakati za jioni, umeme unakatika, na hali hii imeanza kuathiri huduma nyingine muhimu—hasa maji.
Mwanza ni jiji lenye maeneo mengi ya milima na miinuko. Mfumo wa maji unahitaji umeme wa uhakika ili mitambo iweze kusukuma maji kwa nguvu inayohitajika.
Umeme unapokatika mara kwa mara, kasi ya kusukuma maji hupungua, na hatimaye maji hayafiki katika maeneo mengi.
Nyegezi na mitaa yake ni miongoni mwa maeneo yanayokabiliwa na changamoto hii. Kuna maeneo ambayo yamefikia karibu mwezi mzima bila maji, huku mgao wa maji ukiwa haufuati ratiba kwa uhakika.
Wakati Waziri alipofika na kusimamia suala la maji, hali ilianza kuonekana kuwa nafuu na maji yakapatikana. Lakini baada ya Waziri kuondoka, hali imerejea kuwa mbaya—maji hayapatikani kama inavyotarajiwa.
Kwa watu wa MWAUWASA, swali ni rahisi:
Tatizo liko wapi? Kwa nini huduma ya maji iwe nzuri wakati wa ufuatiliaji wa Waziri, lakini baada ya kuondoka wananchi warudi kwenye hali ya kukosa maji?
Wananchi wa Nyegezi na maeneo mengine wanahitaji maji ya uhakika, si maji yanayopatikana kwa kusubiri ziara au ufuatiliaji wa viongozi.
Maji ni uhai. Mwanza inahitaji suluhisho la kudumu.