Hivi unategemea kitatoka kitu gani kwenye kinywa cha mtu ambaye mara baada ya kumaliza darasa la saba, muda wake wote aliwekeza kwenye upigaji ramri na kafara? Anyway ndio Tanzania yetu hiyo tena, kila kitu kinawezekana tu!
Lakini pia nalazimika kutokua na imani na hayo maneno kama kweli yanatoka ndani ya moyo wake, kumbukumbu zangu zinaonesha, wakati wa kampeni za ubunge wa kule Arumeru zilizomuweka ndogo janja madarakani, huyu bwana alitumwa kwa kazi moja tu ya Kuroga, alipoona uchawi wake unaelekea kushindwa, yeye na yule masai Ole Sendeka walionesha nia ya kumchangia dogo Tsh 500,000/= na walimthibitishia dogo kwamba yeye tayari ni Mbunge bado kuapishwa tu, hii ni kwa mujibu wa gazeti moja enzi hizo, uzi huu, hata humu jamvini pia ulibandikwa, kwa tabia hiyo inaonesha magamba wengi huwa wanazungumza vitu wasivyo viamini wawapo majukwaani!