Maji Hufuata Mkondo

Maji Hufuata Mkondo

Dr am 4 real PhD

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2016
Posts
18,356
Reaction score
37,171
Leo tu share story mbali mbali za maji hufuata mkondo..........

Kuna rafiki yangu mmoja alikua anachukizwa sana na kitendo Cha baba yake kupiga ulabu....

Tulipo kua tunakua alituapia kua yeye hato kuja kupiga ulabu duu!! Alipo pata kazi akaanza kupiga ulabu mpk kuitwa Chapombe.....MAJI HUFUATA MKONDO.

Kuna rafiki yangu mmoja baba Ake alikua askari, baada ya kumaliza masomo mtoto Ake akaenda CCP Kwa Sasa ana cheo kikubwa jeshini, mzee alistaafu ila dogo ana cheo kikubwa kuliko mzee....MAJI HUFUATA MKONDO.

Familia Moja mabinti wa hapo huzalia nyumbani.....MAJI HUFUATA MKONDO

Kuna familia ni walaghai, wezi, matapeli, wababaishaji....MAJI HUFUATA MKONDO

Kuna familia Moja baba alikua kiongozi mkubwa wa Dini, mtoto nae akamfuata mzee...MAJI HUFUATA MKONDO.

Je? Una kisa chochote kinacho weza kuelezea maana ya maji kufuata MKONDO?

Karibuni wadau tujadili.
 
Watoto subconsciously wapo wired kufanya kile alichomkuta baba yake anayemlea anafanya.
 
Baba yangu alikuwa daktari nyumbani kwetu dada zangu watatu wote ni madaktari MAJI HUFUATA MKONDO.

Mimi nimesoma masomo ya sayansi enzi za high school masomo ya Art yalinishinda hata daftari nilikuwa sina ajabu watoto wangu wawili wote wamesoma combination niliyosoma mimi high school ya sayansi.Cha ajabu zaidi second born wangu anafanya taaluma niliyoanza nayo kazi hadi sasa MAJI HUFUATA MKONDO.

Baba yangu alikuwa anapiga kilaji kwa ujumla ukoo wetu na kabila letu kilaji ni sehemu ya mila na mimi nakitumia hadi sasa MAJI HUFUATA MKONDO.
 
Mama yangu aliolewa ndoa mbili, ndoa yake ya Kwanza ilivunjika
....napambana huu mkondo usinibebe.
 
Mama yangu aliolewa ndoa mbili, ndoa yake ya Kwanza ilivunjika
....napambana huu mkondo usinibebe.
Pambana kwa ajili yako na kizazi chako. Ukiweza wewe basi umefuta agano hilo vizazi vyako vyote
 
Maisha ya waafrika wengi yapo connect na mizimu, mizimu ndio ucontrol familia kwa kuleta mfanano. Unaweza ukavunja laana yoyote kwa kutojiconnect
 
Unapotaka kuoa au kuolewa angalia bloodline asili ya tabia za wazazi wake zipoje Ili zisikuvae
 
Pambana kwa ajili yako na kizazi chako. Ukiweza wewe basi umefuta agano hilo vizazi vyako vyote
Ni ngumu sana Yani...Namuomba sana Mungu....Imagine ndoa yake ya pili tumezaliwa Sisi watoto ambao Yuko so proud with, mpaka Leo anamlilia Mzee(now marehemu) kuwa waliishi vizuri....Yule mume wa Kwanza Yuko hai Ila hataki hata kumuona.
It's like grass is greener on the other side.
 
Dah mtihani lakini Mungu yupo
 
Maisha ya waafrika wengi yapo connect na mizimu, mizimu ndio ucontrol familia kwa kuleta mfanano. Unaweza ukavunja laana yoyote kwa kutojiconnect
Kiafrika unaconnectiwa kinguvu utake usitake, unazaliwa tu sijui kitovu kinatupwa wapi, nywele zinafukiwa huko....unafungwa mikamba mikamba....Hadi unakua ni you are successful connected.
 
Kiafrika unaconnectiwa kinguvu utake usitake, unazaliwa tu sijui kitovu kinatupwa wapi, nywele zinafukiwa huko....unafungwa mikamba mikamba....Hadi unakua ni you are successful connected.
Thus ni muhimu kujidisconnet Ili usonge
 
Back
Top Bottom