?Nakubaliana Mgambo ndio jeshi lilo karibu na jamii wanajua chocho na wahusika kuliko hawa wamagorofani ndio maana siku hizi wanavaa model na viduku kwenye mustach
Mnakasha maridhawa huu. Na ushauri wangu ni kuwa tuchangie bila ya kuweka hisa za kisiasa.Hebu tupitie kwa ufupi aina ya majeshi yetu na majukumu yake ya kila siku
-JWTZ- hili ndio kama jeshi kuu linalihusika na ulinzi na usalama wa mipaka yetu....naweza kusema ndio jeshi mama na mara chache kuonekana mitaani na linapoonekana mitaani kwenye mavazi yao rasmi ujue hali sio shwari sana... (kuna haja ya kuwa na mjadala kwenye jina)
-JPT/TPDF/TP- Hili ni jeshi la polisi Tanzania, ndio jeshi lililozoeleka zaidi kwa wananchi ndio jeshi linalihusika na kushughulika na maisha ya kawaida ya kila siku ya mwananchi! Kuanzia usalama wa ndani, nyaraka mbalimbali, kesi , hukumu vifungo hata misamaha na madawati ya jinsia na kwa sehemu msaada wa kisheria...! Tungeruhusu mijadala ya wazi hili ndio lilipaswa kuitwa Jeshi la wananchi
-JKT- Jeshi la kujenga Taifa , hili ni jeshi la damu changa madhumuni yake ni kuwafundisha vijana wote wanapomaliza elimu ya kidato cha sita nk uzalendo ukakamavu na stadi anuwai kabla ya kuendelea na elimu ya juu....hapa kuna nguvu kazi kubwa sana inapotea bure nguvu kazi ya kujenga taifa katika nyanja mbalimbali kuanzia kilimo ufundi ufugaji mpaka biashara na sayansi na teknolojia... kile kitengo cha SUMA-JKT kama kungekuwa na uhuru wa majadiliano kingepaswa kipelekwe JKT na wanajeshi waachiwe jukumu lao la msingi
-JLMT- Jeshi la mgambo Tanzania, hili ni jeshi ambalo sio rasmi sana likiwa haitofautiani sana na polisi jamii (kitengo kinachoelekea kufutwa awamu hii)haya ni majeshi ya msingi lakini yasiyopewa kipaumbele sana...haya ndio yanajua kila kitu nyumba kwa nyumba mtu kwa mtu na mtaa kwa mtaa...tungekuwa na mijadala huru hili tungelijadili kitaifa ili iwe ndio msingi rasmi wa majeshi yote na kuwe na program maalum zinazohusika na kutambulika kisheria
-Tuna majeshi mengine kama ya zimamoto nk lakini haya hayawezi kuwa sehemu ya mjadala kwakuwa ni vitengo ndani ya jeshi la polisi
Je katiba yetu inatuambia nini kwenye dhima na utayari wa kuwa na mijadala kama hii?
Nawasilisha....!!!
Sahihi kabisa ila nimeona ni kama auxiliary kwenye jeshi la polisi...ila kwakuwa ni mjadala nakubaliana naweMnakasha maridhawa huu. Na ushauri wangu ni kuwa tuchangie bila ya kuweka hisa za kisiasa.
Nirudi kwenye mada, Mshana Jr Mimi naongezea na jeshi la Magereza (MT) jeshi hili linahusika na utekelezaji wa vifungo kwa watu ambao wamehukumiwa vifungo (magerezeni na nje [kwa kushirikiana na idara ya ustawi wa jamii]).
NB:
Wanasheria watuwekee na sheria zilizoanzisha majeshi haya
Shukran.
Kaka ...
Nimeona ila mkuu ingekua vizuri kama majeshi hayo ungeweka juu, hao mgambo ndipo ukawaweka kwenye nk.Angalia para ya mwisho nimesema zimamoto nk
Huhitajiki kutoa lugha za kukera huu ni mjadala huru usio na mtazamo wa kisiasa..kumbuka kila tutakachoandika hapa kitakuwa na faida kwa wengi hivyo nashauri tu tuache mihemko tuelimishaneKwa hapa wewe ni ****** kwa taarifa tu suma jkt ni shirika lipo chini ya jkt na wasimamizi ni jkt, na hakuna jeshi la mgambo bali mgambo ni tawi ndani ya jwtz na mkuu wa tawi la mgambo ni meja jeneral japo sasa anakaimu brigedia hata wakuu wa mgambo mikoani ni ma colnel
Sasa ****** ndio nini? Hivi lazima mfumue makucha yenu kwenye kila mnakasha? Kwenye hii mijadala pia tunapimana kiwango chetu cha ustaarabu!Kwa hapa wewe ni ****** kwa taarifa tu suma jkt ni shirika lipo chini ya jkt na wasimamizi ni jkt, na hakuna jeshi la mgambo bali mgambo ni tawi ndani ya jwtz na mkuu wa tawi la mgambo ni meja jeneral japo sasa anakaimu brigedia hata wakuu wa mgambo mikoani ni ma colnel
Na kama uko sahihi kuhusu mgambo inabidi waondolewe kwenye usimamizi wa JWTZ kwakuwa majukumu hayafananiKwa hapa wewe ni ****** kwa taarifa tu suma jkt ni shirika lipo chini ya jkt na wasimamizi ni jkt, na hakuna jeshi la mgambo bali mgambo ni tawi ndani ya jwtz na mkuu wa tawi la mgambo ni meja jeneral japo sasa anakaimu brigedia hata wakuu wa mgambo mikoani ni ma colnel
Mmh hapana japo kwa tafsiri ya kiswahili ni mlinda usalama wa Mali na RAIAMkuu Mshana Jr.
Labda tu utueleweshe kama unafahamu kirefu cha POLICE kama ambavyo umetafsiri JWTZ (Jeshi la Wananchi wa Tanzania).
Nini kirefu neno kwa neno tunaposema POLICE, pengine labda tunapotumia kiswahili kwa maana ya Polisi tunapoteza maana.?
Sijaona jeshi la magereza, jeshi la zimamoto, na uhamiaji. Mshana Jr?