MAJESHI YA UKRAINE YAKOMBOA ZAID YA KM 1000 kharkiv

Mrengwa wa kulia

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2022
Posts
1,145
Reaction score
3,765
Vikosi vya jeshi la Ukraine vimepata mafanikio kwenye uwanja wa vita baada ya kuyakomboa maeneo kadhaa yaliyokuwa chini ya udhibiti wa Urusi kwenye mkoa wa mashariki mwa nchi hiyo wa Kharkiv.

Taarifa hizo zimetangazwa na rais Volodymyr Zelenskiy kupitia ujumbe wa video aloutoa jana na kuthibitishwa na kiongozi aliyewekwa madarakani na Urusi kwenye jimbo hilo la Kharkiv, Vitaly Ganchev.

Rais Zelensky amesema kwa jumla wanajeshi wa Ukraine wameyakomboa maeneo kadhaa ya makaazi na kurejesha udhibiti wa eneo la ukubwa wa kiasi kilometa za mraba 1,000 upande wa mashariki na kusini mwa nchi hiyo.

Moja ya maeneo yaliyokombolewa ni mji wa Balakliia, ulio sehemu ya uwanja wa vita kusini mwa jimbo la Kharkiv. Kiongozi wa jimbo hilo anayeungwa mkono na Urusi amekiri hayo ni mafanikio makubwa kwa vikosi vya jeshi la Ukraine.
source

DW,aljazeera

KWANI HIZO HIMARS ZIMEKOMBOA VIJIJI VINGAPI HADI SASA??
 
Jaribu kutumia akili ya kawaida!! Hivi hujui kuwa km 1000 ni umbali wa kutoka kaskazini ya tanzania hadi dare salaam.. ni zaidi ya mikoa 6 unaipita: hivi unataka kuniambia hiyo kharkiv ina ukubwa huo kiasi kwamba wamekomboa hizo km 1000 halafu bado na wanajeshi was urusi wako ndani humohumo?
 
Jaribu kutumia akili ya kawaida!! Hivi hujui kuwa km 1000 ni unbelievable way kutoka kaskazini ya tanzania hadi dare salaam.. ni zaidi ya mikoa 6 unaipita: hivi unataka kuniambia hiyo kharkiv ina ukubwa huo kiasi kwamba wamekomboa hizo km 1000 halafu bado na wanajeshi was urusi wako ndani humohumo?
Zile ni km za mraba 1000, jaribu kutumia akili usikurupuke,
 
Jaribu kutumia akili ya kawaida!! Hivi hujui kuwa km 1000 ni unbelievable way kutoka kaskazini ya tanzania hadi dare salaam.. ni zaidi ya mikoa 6 unaipita: hivi unataka kuniambia hiyo kharkiv ina ukubwa huo kiasi kwamba wamekomboa hizo km 1000 halafu bado na wanajeshi was urusi wako ndani humohumo?
Jaribu kusoma habari kwa makini, na unapopewa ukubwa wa eneo sio lazima iwe urefu tu, yamkini limehesabiwa na kwa mapana pia. Hapo ni km za mraba.
 
Vikosi vya jeshi la Ukraine vimepata mafanikio kwenye uwanja wa vita baada ya kuyakomboa maeneo kadhaa yaliyokuwa chini ya udhibiti wa Urusi kwenye mkoa wa mashariki mwa nchi hiyo wa Kharkiv.

Taarifa hizo zimetangazwa na rais Volodymyr Zelenskiy kupitia ujumbe wa video aloutoa jana na kuthibitishwa na kiongozi aliyewekwa madarakani na Urusi kwenye jimbo hilo la Kharkiv, Vitaly Ganchev.

Rais Zelensky amesema kwa jumla wanajeshi wa Ukraine wameyakomboa maeneo kadhaa ya makaazi na kurejesha udhibiti wa eneo la ukubwa wa kiasi kilometa za mraba 1,000 upande wa mashariki na kusini mwa nchi hiyo.

Moja ya maeneo yaliyokombolewa ni mji wa Balakliia, ulio sehemu ya uwanja wa vita kusini mwa jimbo la Kharkiv. Kiongozi wa jimbo hilo anayeungwa mkono na Urusi amekiri hayo ni mafanikio makubwa kwa vikosi vya jeshi la Ukraine.
source

DW,aljazeera

KWANI HIZO HIMARS ZIMEKOMBOA VIJIJI VINGAPI HADI SASA??
1000 KM^2 ni eneo kama kariakoo - mbezi;, pugu- mbagala.....

Ni sawa kusema wamekomboa vijiji kumi!
 
Kwan KHARKIV yote si ilikimbolewa au kuna KHARKIV mbili
Isije ikawa mie mkaazi wa king'amboni siijui UKRAINE
RUSSIA nilazima SMO ikamilike

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom