Majeruhi ajali ya Watoto wa shule Arusha kupelekwa Marekani kwa matibabu zaidi

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,870
Arusha. Jopo la madaktari bingwa wa Shirika la Stemm la Marekani kwa kushirikiana na Serikali, limeamua kuwapeleka Marekani kwa matibabu majeruhi watatu wa ajali ya wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva.

Majeruhi hao ambao wamelazwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru ni Jofrey Tarimo, Doreen Mshana na Sadia Awadh wanatarajiwa kusafirishwa kwenda Marekani wakiambatana na wazazi wao, daktari na muuguzi wa hospitali ya mkoa wa Arusha.

Matibabu hayo yatatolewa kwa ufadhili wa madaktari hao kutoka Marekani ambao walikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuwasidia wanafunzi hao kutoka kwenye gari lililo pata ajali, wakiwa njiani kuelekea Ngorongoro na Serengeti kutalii.

Daktari mkuu wa hospitali Mount Meru, Wonanji Thimos amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na madaktari hao imeshaanza taratibu za kuwasafirisha majeruhi hao kwa ajili ya matibabu zaidi.



Dk Thimos amesema taratibu za safari zikikamilika majeruhi hao watasafirishwa kwenda Marekani wakati wowote kuanzia sasa.

















 
Mungu awasimamie, alipoyasema Mh. Samia kwenye hotuba yake nilijua lazima itakuwa hivi juu ya kutibiwa. Mola awe nao, wapone haraka.

Utakuta Mbunge Lema leo anashangaa kuyasikia, kwa sababu mawazo yake siku hiyo yalikuwa kushika mic tu na kumfikiria Gambo. Eeh
 
Naunga dot tu. Hao wamarekani waliowaokota walikuwa eneo husika kwa mawasiliano. Kwenye ajali hakukuwa nadamu, hiyo shule ni ya private. Leo wanapelekwa marekani kwa matibabu.
Nadhani wanaenda kuchunguzwa kwa nini walishinda jaribu LA wajenzi huru.
Nawaza tu
 
Ngoja wakapate exposure kidogo..japo tuwasahau maana kibongobongo wakitoka hospital tungejaza makwao kwenda kupata ushuhuda..lakini wakienda huko mpaka wakirudi tushasahau..
 
Back
Top Bottom