Majengo marefu kama haya.......!!!!

excel

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2011
Posts
22,463
Reaction score
17,956
Habari zenu wadau..

naombeni kufahamishwa juu ya teknolojia inayotumika kuzuia radi... yani kiujumla, inafanya fanya vipi kazi mpaka inazuia radi?

-je, kwanini radi inahusishwa na makundi makubwa ya wanyama? kwamba pale penye kundi kubwa la wanyama, endapo mvua ikiwa inanyesha, kuna uwezekano mkubwa wa kupigwa na radi?


 
Radi au lighting, inatokea endapo mawingu yenye electrostatic charge yanapokutana, yakikutana yanadischarge electricity au umeme kama bolt, ardhi iko neutral kwa hiyo umeme huo unajaribu kutafuta conductor ya kupitia. vitu virefu kama miti na minara ndio vinaathirika kirahisi. ndio maana majengo marefu huwa yanawekwa wire au conductor ndefu ambayo radi ikipiga inakuwa rahisi kufikia. umeme huo ukigusa hicho kitu kirefu unapitishwa kwenye earth ambapo unakuwa hauleti madhara.
Ndio maana ndege za abiria zinawekewa material inayopitisha umeme, radi ikipiga umeme unakuwa conducted kwa hiyo hauleti madhara.
 
na vipi kuhusu radi zinazotengenezwa na wabena wa Lupembe na zile za sumbawanga za wafipa?
 
Nasikia radi haimwezi kondoo hata kidogo!
 
Radi ni miale ya mwanga na volteji ya umeme inayojijenga wakati mawingu angani yenye chaji mbili tofauti (hasi na chanya) yanapokaribiana au pia kati ya mawingu na ardhi (kwenye umbo lililo na ncha chongofu).

Kwa kawaida kutokana na effect ya ionization mawingu ya yenye concentration kubwa ya chaji chanya hukaa juu ya yale yenye concentration kubwa ya chaji hasi.

Sasa ni wakati gani ambapo radi huwa inapiga duniani?
Awali ya yote katika elimu ya static electricity kuna kanuni moja huwa inasema "like charges repel unlike charges attract".

Kwa kuzingatia kanuni hiyo utagundua kuwa kitu chochote huku ardhini ambacho kinahifadhi chaji upande ule unaotizamana na mawingu (kumbuka mawingu yaliyo chini yana chaji hasi) utakuwa na concentration kubwa ya chaji chanya hivyo kupelekea zao la electric field baina ya mawingu na kitu hicho au ardhi.

Vilevile katika elimu ya static electricity kuna nadharia nyingine ambayo inaelezea kuwa vitu vyenye ncha chongofu au vyenye area ndogo na virefu mathalani minara, milima, majengo marefu huwa na concentration kubwa ya chaji.

Kwa kuunganisha nadharia ile ya kwanza na hii ya pili utatambua kuwa vitu hivi virefu wakati wa mawingu yasabishayo radi vyenyewe huwa na concentration kubwa ya chaji chanya.

Sasa jinsi chaji hasi mawinguni inavyoongezeka, huwa inatafuta mahali pa ku-discharge.

Sehemu nzuri za kudischarge ni zile zenye uwepo mkubwa wa chaji chanya ambazo ndio zile chongofu na ndefu (zilizo jitokeza).

Hivyo ndio maana radi ikipiga unaona inakimbilia katika minara, miti, watu au wanyama waliosimama sehemu ya wazi au uwanda wa wazi n.k.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…