singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
WIKI hii, Rais John Magufuli anatimiza siku 100 akiwa madarakani. Katika muda huo mfupi, amefanikiwa kufanya mambo ambayo wengi walitaraji kuwa angeyafanya.
Lakini, ni wazi kuwa Magufuli mwenyewe asingeweza kufanya kila kitu. Katika makala hii, tunatazama watu sita ambao walikuwa na mchango mkubwa katika siku hizi 100 za kwanza za Serikali ya Awamu ya Tano.
Hawa ndiyo walikuwa watekelezaji wa maagizo yake; kwa kumshauri, kutenda na kutengeneza mazingira ya kufanikishwa kwa kile ambacho Rais Magufuli alikuwa ameahidi kufanya wakati kampeni.
1. Dk. Servacius Beda Likwelile
Imesahaulika mapema kwamba Rais Magufuli alikaa madakani kwa takribani mwezi mmoja kabla ya kuteua mawaziri na watendaji wengine kumsaidia katika utekelezaji wa majukumu yake.
Ni katika kipindi hicho ndipo Magufuli alipojipambanua kama ‘mtumbua majipu namba moja’. Ni wakati huo ndipo Rais alipoanza kazi ya kufumua Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Bandari (TPA).
Vyanzo vya gazeti hili vinaeleza kuwa nyuma ya matukio haya muhimu yaliyoweza kuupa taswira uongozi wa Magufuli alikuwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile.
Likwelile ni msomi wa shahada ya uzamivu (PhD) katika uchumi na katika kipindi cha miaka 25 iliyopita, amefanya kazi kama mhadhiri katika vyuo vikuu mbalimbali vya ndani na nje ya nchi, Benki ya Maendeleo ya Afrika na vyombo vingine vya kiserikali na visivyo vya kiserikali.
Raia Mwema limeambiwa kwamba katika siku za kwanza za utawala wake, Magufuli alikuwa akisikiliza ushauri wa Likwelile kwenye maamuzi mengi yaliyohusu kuongeza mapato na kisera katika eneo la uchumi.
Kama ilivyo kwa Magufuli, Likwelile pia ni zao la Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, ambaye alimtoa Likwelile kwenye shughuli za kitaaluma na kumfanya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa uliokuwa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Inawezekana hakupata vichwa vingi vya habari kwenye siku hizi 100 za kwanza za utawala wa Magufuli lakini Likwelile alikuwa na msaada mkubwa kwa serikali kwenye kipindi hicho.
2. Lawrence Nyasebwa Mafuru
Wakati wa kampeni za kuwania urais, mojawapo ya ahadi kubwa za Rais Magufuli ilikuwa ni namna alivyopania kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda na pia kurejesha ardhi na mashamba yaliyotelekezwa.
Katika kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda, mojawapo ya mambo ambayo ilibidi serikali iyafanye haraka ilikuwa ni kuhakikisha kuwa viwanda vilivyobinafsishwa na serikali lakini vikatelekezwa au kutumika ndivyo-sivyo, vinarejeshwa haraka.
Ndani ya siku 100 za utawala wa Magufuli, Mafuru kwa wadhifa wake kama Msajili wa Hazina, ameanza kazi kwa kasi kutekeleza ahadi hizo za rais katika namna ambayo imewavutia wengi ndani ya serikali.
Wiki mbili zilizopita, Mafuru aliagiza kuvunjwa kwa mkataba baina ya serikali na mwekezaji wa kiwanda cha chai cha Mponde mkoani Tanga; akiamuru kitwaliwe na kuanza kazi mara moja.
Mgogoro wa kiwanda hicho ulikuwa umedumu pasipo suluhisho la maana katika kipindi cha miaka kumi iliyopita na wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, aliyekuwa mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, aliahidi kuwa kama angeshinda urais, angetatua mgogoro huo.
Lakini Mafuru amefanya hilo ndani ya muda mfupi pamoja na kutoa agizo la kurejesha mashamba na viwanda vilivyotelekezwa; akitoa tangazo hilo ndani ya wiki mbili tangu Magufuli aapishwe.
Katika tangazo lake hilo, Mafuru aliagiza; “Ninawaagiza wawekezaji wote walionunua viwanda na mashamba yaliyokuwa yanamilikiwa na Serikali kwa ajili ya uwekezaji wawasilishe taarifa zao za sasa ndani ya siku 30, kinyume na hapo Serikali itachukua hatua stahiki ikiwamo kurejesha viwanda na mashamba hayo kwenye miliki yake,”
Agizo hili la Mafuru Magufuli tayari limeanza kuzaa matunda kwa kurejeshwa kwa baadhi ya mashamba na viwanda vilivyotelekezwa kwenye siku za nyuma na kuna dalili kuwa kama ataendelea na kasi hii, kutakuwa na mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka mitano ya kwanza ya Magufuli.
Hata hivyo, agizo linalotajwa kuwa la aina yake kutoka kwa Mafuru ni lile la kutaka mashirika na taasisi za kiserikali zilizoweka fedha zao katika mabenki ya kibiashara, yazihamishe na kuzipeleka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Msajili wa Hazina ndiye msimamizi wa mashirika yote ya serikali na kwa uamuzi wake huu; ingawa unapingwa na kupongezwa na pande tofauti, unamaanisha kuwa serikali sasa itakuwa na udhibiti wa fedha zake; ikiwamo kuzipangia mipango na matumizi kwa ajili ya shughuli zake.
Kabla ya kuteuliwa kwake kushika wadhifa huu Novemba, 2014, Mafuru aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC na wakati benki ya FBME ilipowekwa chini ya usimamizi wa serikali, Mafuru pia ndiye aliyeteuliwa kuisimamia.
Ndani ya siku 100 za Magufuli, Mafuru amejitambulisha kama mtu anayetekeleza ahadi za bosi wake huyo kwa kasi kubwa.
3. George Mcheche Masaju
Huyu ndiye Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) ambaye alikuwa mtu wa kwanza kuteuliwa na Magufuli. Kimsingi, Masaju aliyeuliwa kushika wadhifa huo saa chache tu baada ya Magufuli kuapishwa kuwa Rais.
Masaju ni mwanasheria ambaye anaonekana kupata taabu kuishi kisiasa. Kwa wanaomfahamu kupitia vikao vya Bunge, wanapata picha tofauti na mwanasheria ambaye wanaokwenda mahakamani wanamuona.
Mwanasheria huyu alipata umaarufu mkubwa wakati alipokuwa wakili wa serikali kwenye kesi iliyofunguliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kupinga kauli iliyowahi kutolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuwa watu wanaofanya vurugu “wapigwe tu, maana hakuna namna nyingine”.
Masaju aliiokoa serikali katika suala hilo baada ya kutoa hoja kwamba walioshitaki walikosea taratibu kwani kwenye suala kama hilo wanaotakiwa kufungua kesi ni wananchi walioathirika na kauli hiyo na si taasisi kama LHRC na Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS).
Kwenye siku 100 za Magufuli, Raia Mwema limeambiwa kwamba Masaju ndiye aliyekuwa mshauri mkuu wa waziri huyo wa zamani wa Ujenzi katika masuala ya kisheria na kwamba umuhimu wake ni kuwa serikali haijaingia katika matatizo ya sheria kupitia maamuzi mazito yaliyofanyika kwenye siku hizi 100 za kwanza.
Kwenye siku hizi 100, Magufuli ametengua teuzi na kusimamisha watendaji kazi, amefungua kesi za wahujumu uchumi , amebomoa nyumba zilizojengwa maeneo yaliyokatazwa, kuamuru kupelekwa kwa fedha za mashirika ya umma BoT, kuvunja mikataba na kurejesha mashamba; mambo yote hayo yakiwa na athari za kisheria.
Kuliko mtu mwingine yeyote kwenye serikali ya Magufuli, Masaju ndiye ambaye alihakikisha serikali haivunji sheria ua kwenda kinyume na Katiba kupitia maamuzi yote makubwa yaliyofanyika katika wakati huo.
Ni siku 100 za kwanza lakini inaonekana Masaju atakuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha serikali haipati hasara kwa kulipa watu au taasisi zitakazoipeleka serikali endapo sheria hazitafuatwa.
4. Samia Suluhu Hassan
Katika orodha hii ya majemedari wa Magufuli, yeye ndiye mwanamke pekee na pia mwanasiasa kutoka Zanzibar. Jina lake halimo katika orodha hii kwa sababu ya kujenga uwiano. Kuna ushahidi wa wazi kuwa mwanamama huyu ameonyesha uwezo mkubwa.
Kihistoria, nafasi ya Makamu wa Rais, imekuwa ikionekana ni nafasi iliyopo kikatiba tu na isiyo na maana sana. Miaka michache iliyopita, kulikuwa na utani kwamba kifaa muhimu cha kazi kwa Makamu wa Rais wa Tanzania ni mkasi. Kwamba kazi yake kubwa ni kukata utepe wakati wa uzinduzi wa miradi.
Hata hivyo, si kweli kwamba nafasi hii haina hata sababu ya kuwepo. Mwanasiasa maarufu wa Marekani, John Adams, aliyepata kuwa Makamu wa Rais wa nchi hiyo aliwahi kunukuliwa akisema; “Kwa sasa, kwenye wadhifa wangu huu, mimi si chochote, lakini naweza kuja kuwa kila kitu”.
Uchunguzi wa Raia Mwema umeonyesha kwamba taratibu, na kwa staili ya kipekee, Samia ameonyesha uwezo mkubwa hususani katika kushughulika na mgogoro wa kisiasa uliopo Zanzibar na kuhakikisha kuwa ofisi yake inakuwa na msaada kwa Magufuli.
“ Nilichobaini kwa Samia ni kwamba ni mwanasiasa mwenye uwezo mkubwa na msimamo. Ana sura ya upole lakini anaijua siasa ya nchi yetu na msimamo thabiti. Leo hii Zanzibar kumetulia pamoja na matatizo yote yaliyopo.
“Si kwamba kule wananchi wote wanafurahia kila kitu au wameridhika na kinachoendelea, la, lakini kuna mambo yanafanyika kuleta utulivu huo na Samia ni sehemu ya watu wanaofanya utulivu huo uendelee kuwepo,” alisema mmoja wa wanasiasa walio karibu na Samia ambaye hata hivyo hakutaka kutajwa jina lake kwenye habari hii.
Katika kipindi cha siku 100 za Magufuli, Samia ameshiriki katika mazungumzo baina ya Magufuli na wagombea urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu uliofutwa; Dk. Ali Mohamed Shein na Seif Shariff Hamad, kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika (AU) uliofanyika Addis Ababa na pia mkutano baina ya viongozi wa Afrika na China uliofanyika Afrika Kusini.
Katika uongozi ambao Rais wake hajatoka nje ya nchi hata mara moja tangu awe Rais na Waziri Mkuu akiwa amesafiri mara moja tu; maana yake ni kuwa Samia ndiye kiongozi wa juu (miongoni mwa watatu wa juu zaidi kiserikali) aliyesafiri zaidi nje ya nchi (mara mbili!) katika siku 100 za Magufuli kuliko mwingine yeyote.
5. Ombeni Yohana Sefue
Kulikuwa na maswali kuhusu ni namna gani Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, angeweza kufanya kazi kwa karibu na Rais John Magufuli. Sefue ni mwanadiplomasia kutoka unyayoni hadi utosini. Uanadiplomasia ni sifa ya mwisho ambayo mtu anaweza kumpa Magufuli.
Wengi walidhani kwamba ilikuwa rahisi kwa Sefue kufanya kazi na mtangulizi wa Magufuli, Jakaya Kikwete, kwa sababu wote ni wanadiplomasia wenye baadhi ya mambo yanayofanana.
Lakini, katika siku hizi 100 za Magufuli, hususani siku zile 30 za kwanza, Magufuli na Sefue walikuja kuonekana kama pipa na mfuniko. Kuna wakati, kulikuwa na maneno kwamba hakukuwa na haja ya kuteua mawaziri kwa vile Sefue, Magufuli na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, walionekana kwenda vizuri.
Katika mambo ambayo Magufuli anaonekana kutaka kuyatilia mkazo kwenye utawala, ni suala la kurejesha nidhamu na uadilifu kwa watumishi wa umma ambao kiongozi wao, kwa mujibu wa sheria zilizopo, ni Sefue.
Mahojiano na baadhi ya viongozi wa serikali yamemtaja Sefue kuwa ndiye mtu aliyemfanya Magufuli aingie na kuuvaa urais “ kama samaki kwenye maji”. Kwamba Magufuli alianza kuchapa kazi kwenye siku yake ya kwanza ofisini kwa sababu Sefue alimuandalia maisha.
Sefue ana uzoefu na Ikulu. Aliingia Ikulu kwa mara ya kwanza mwaka 1993 wakati alipoteuliwa kuwa Mwandishi wa hotuba wa Rais Ali Hassan Mwinyi. Rais Mkapa alipoingia madarakani mwaka 1995, aliendelea na Sefue kwenye wadhifa, ingawa alimuongezea majumuku mengine.
Sefue amewahi pia kuwa Balozi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa (UN) –ikimaanisha kuwa Rais Magufuli ana mtu wa karibu ambaye anamsaidia kupunguza nakisi yake kwenye masuala ya uhusiano wa kimataifa.
Sefue ametumika kama “mdomo” wa Magufuli kwenye siku hizi 100 za kwanza na kuna kipindi alikuwa akionekana kama sura ya utawala huu. Inasaidia pia kwamba yeye, kama ilivyo kwa Magufuli, ni watu walio karibu na Mkapa ambaye anatajwa kuwa na ushawishi mkubwa kwenye serikali ya sasa.
6. Majaliwa Kassim Majaliwa
Wakati alipotangazwa na Rais Magufuli kuwa Waziri Mkuu, Watanzania wengi walikuwa hawamfahamu mwalimu na mwanamichezo huyu. Miezi mitatu baadaye, jina la Majaliwa limekuwa maarufu kwenye medani ya kisiasa hapa nchini.
Kuna mchapo mmoja maarufu ulioenea hapa nchini kuhusu namna Majaliwa alivyo na hamu ya ‘kutumbua majipu’. Kwamba siku moja katika mojawapo ya ziara zake za kiserikali mikoani, alishuka kwenye ndege na kulakiwa na viongozi wa mkoa.
Baada ya salama za awali, mchapo unaendelea, Majaliwa aliuliza swali kwa viongozi hao ambalo ndilo lililosambaa “ Kuna jipu gani hapa linalohitaji kutumbuliwa?” aliuliza kwa namna ya utani lakini uso ukionyesha kuwa alilolizungumza halikuwa na chembe ya utani kwa waliomsikia akizungumza siku hiyo.
Umuhimu wa Majaliwa kwenye siku hizi 100 za kwanza ulitokana na namna alivyokuwa makini katika kuhakikisha maagizo ya Rais Magufuli yanatekelezwa na yeye pia kuhakikisha kwamba si kikwazo kwenye kasi ya Rais.
Mwanasiasa huyu alijisimika kama Waziri Mkuu wakati aliposhughulika na suala la ukwepaji wa mapato kupitia TRA. Baadhi ya watumishi wa TRA na TPA bado wanakumbuka namna alivyotembelea kwenye maeneo yao ya kazi akiwa na rundo la nyaraka zilizoonyesha mapungufu yote yaliyokuwepo.
Majaliwa alikuwa na taarifa kuhusu makontena yaliyopitishwa bandarini, yaliyolipiwa stahili zote, ambayo hayakulipiwa na yale ambayo yalipitishwa bila kulipiwa. Kila swali alilokuwa akiuliza, aliuliza huku akiwa na majibu tayari.
Ni ziara hiyo ndiyo hatimaye ilisababishwa kung’olewa kwa aliyekuwa Kamishina Mkuu wa TRA, Rished Bade, na baadhi ya maofisa wa ngazi za juu wa mamlaka ambao sasa wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za uhujumu uchumi.
Katika kipindi cha siku 100 zilizopita, Majaliwa hajawaangusha wale waliodhani kwamba ingawa ni mchanga katika siasa za kitaifa za Tanzania, amepewa viatu ambavyo amemudu kuvivaa.
Raia Mwema