Majambazi yavunja ATM Tabata Segerea

Majambazi yavunja ATM Tabata Segerea

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,685
“Wakati wakivunja mashine, baadhi ya madereva wa bodaboda walikuwa wameanza kurejea katika eneo hilo, ndipo walipobaini na kuanza kukusanyika, lakini majambazi hao baada ya kuona wananchi na madereva wa bodaboda wakikusanyika kwa kasi, walikimbia kabla ya polisi hawajafika kwenye tukio. Hawakuchukua kitu.”

“Mmoja wa wakazi wa eneo hilo alisema uvamizi huo ulifanyika saa nane kasoro usiku ‘WAKATI HUO UMEME ULIKUWA UMEKATIKA TANGU SAA TANO USIKU’ “

Source: MWANANCHI
 
Wanachekewa sana, kama wanavamia kituo na kuchukua silaha watashindwa ATM???!!!!

Inakera sana!!!
 
Wale polisi waliofukuzwa kazi kwa kosa la kula "denda" wakiwa kwenye uniforms muda wa kazi, watakwenda kufanya shughuli ipi?
 
Wale polisi waliofukuzwa kazi kwa kosa la kula "denda" wakiwa kwenye uniforms muda wa kazi, watakwenda kufanya shughuli ipi?

Ndiyo shida ya kutelekeza elimu nchini, kama elimu inayotolewa nchini ingekuwa bora na yenye kumuandaa raia kujiajiri hao wasinge risk kwa kwenda kuvunja ATM, lakini elimu bora imeelekezwa kwa watoto wa vigogo huku watoto wa masikini wakipata elimu duni ambayo inawalazimisha ajira za ujambazi, all in all haya yanayotokea ipo siku yatawakuta waliotufikisha hapa tulipo
 
kaburi tunajichimbia wenyew na hii serikali yetu.. Wale vijana wa jkt wanaomaliza mkataba na kurud nyumban bila kuajiliwa wanafanya kaz gan?
Polis waliofukuzwa mwaka jana wako na kaz gan?
Hizo ni nyepes zilizo chini ya kapet sijui kama mkulu analijua hilo....

Kuna baya zaidi linakuja.
Tuombe Mungu Tz isiingie vitan vya wenyew kwa wenyew havitaisha kamwe kuna jeshi kubwa liko mitaan ila limekosa ufadhili wa silaha tu
 
Hii muvi sjui inaisha lini???,bahati mbaya haina wa kuitafsiri.haieleweki.
 
kaburi tunajichimbia wenyew na hii serikali yetu.. Wale vijana wa jkt wanaomaliza mkataba na kurud nyumban bila kuajiliwa wanafanya kaz gan?
Polis waliofukuzwa mwaka jana wako na kaz gan?
Hizo ni nyepes zilizo chini ya kapet sijui kama mkulu analijua hilo....

Kuna baya zaidi linakuja.
Tuombe Mungu Tz isiingie vitan vya wenyew kwa wenyew havitaisha kamwe kuna jeshi kubwa liko mitaan ila limekosa ufadhili wa silaha tu

Ni uzembe tu mkuu watu wasio na silaha hawawezi kiwa tishio kwa "armed forces" kisa walipitia mafunzo, ni potential danger lakini isiwe kiasi cha vituo kuvamiwa na silaha kuporwa au kama hivi watu wanavunja ATM!!!!

Tukubali kuna weakness kubwa leo kwanza kabla ya kuanza kuogopa vita ya kesho!!!
 
!
!
raia wanoko tu........baada ya kuendelea na mishe zao mnafafata watu. Hongera majambazi, mmethubutu angalau. ATM ukiweka geto,alhamdulilah
 
makusanyo ya mwisho wa mwakaaaa......aaaa Mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyeweeee
 
Ni ngumu sana kuvunja Atm uchukue pesa. Si ajabu ukatumia nguvu kubwa kudrill kiasi kwamba ukifanikiwa kufungua unakuta hela zimeungua
 
Nchi za wenzetu ATM hata hazina walinzi..na hata husikii majambazi yamezivunja. Huku kwetu pamoja na walinzi, sungusungu lakini bado hali si shwari.
 
Wale polisi waliofukuzwa kazi kwa kosa la kula "denda" wakiwa kwenye uniforms muda wa kazi, watakwenda kufanya shughuli ipi?
Watakwenda kulana denda kwa nafasi now!!
 
Ndo ile milio kama mabomu juzi usiku?! Niliisikia Mara tatu
 
Shida ya nchi hii ni kuanzisha projects ambazo hakuna mfuatiliaji wa kuhakiki matokeo ya mwisho na impacts zake za muda mfupi na mrefu.
Mifano ipo wazi kama hii ya kustaafisha au kufukuza watu wenye mafunzo ya kijeshi na kuwaacha mitaani bila kuwa na chombo cha kuwafuatilia walipo na wanafanya nini. Kwa nchi hii hili haliwasumbui kwani hatari na athari zake haziwahusu. Wao na chadema tu. Au yote yanangoja msaada wa watu wa marekani?
 
Back
Top Bottom