D Metakelfin
JF-Expert Member
- Mar 23, 2017
- 3,193
- 3,325
Watu wanaosadikiwa kuwa majambazi wamevamia machimbo ya dhahabu yaliyopo katika kijiji cha Nyakavangara tarafa ya Isimani ktk halmashauri ya wilaya ya Iringa mkoani Iringa na kuwapora wachimbaji wadogo katika machimbo hayo zaidi ya shilingi milioni 100 pamoja na dhahabu yenye uzito wa gramu 840.
Katika tukio hilo la uvamizi wa kutumia silaha za moto wachimbaji 12 wamejeruhiwa na na kulazwa ktk hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa kwa matibabu huku mmoja kati yao akielezewa kuwa ktk hali ya umahututi.
Akizungumza na waandishi wa habari asubuhi ya leo Mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela amesema watu hao wanaozaniwa kuwa majambazi walivamia machimbo hayo usiku wa jana majira ya saa mbili na kupora wachimbaji wadogo ktk eneo hilo kiasi kikubwa cha pesa.
Bw Kasesela ambaye pia ni M/Kiti wa kamati ya ulinzi wa wilaya hiyo amesema hali ya usalama ktk eneo hilo sio ya kuridhisha sana kufuatia wimbi kubwa la wachimbaji toka mikoa mingine nchini kuingia ktk kijiji hicho huku akiyaomba makambuni ya simu za mkononi nchini kuwekeza ktk miundombinu ya mawasiliano ktk mgodi huo ili kurahisisha mfumo wa malipo kwa njia ya simu.