Majambazi wateka mji wa Bunda usiku

mende 2014

JF-Expert Member
Apr 13, 2014
763
131
Majambazi wamevamia duka la Muuza simu usiku wa saa tisa na kupora Simu zote na pesa katika eneo la genge la jioni.
Kabla ya tukio hilo wakawa wamepiga risasi Nyasura mbugani mwendo wa saa nne usiku.
Baada ya tukio walipiga risasi zaidi ya 10 na Polisi hawakuweza kujitokeza kujibu mashambuzi hayo.
Pamoja na hayo yote hapa Bunda matukio ya Bunduki yamezidi kila Leo na wananchi hawana amani.
 
Polenin sana,nadhan ni vyema baraza la usalama wilaya ijaribu kutafuta nn chanzo cha hayo yote.
Vp mende bdo zile shughuli zetu pale stand unaziendeleza pamoja na akina nyerere.
 
Kamanda peter ouma ndiye aliweza kudhibiti hii hali lakini alipopandishwa cheo na kuhamishwa tatizo limerudi kwa kasi sana na hata OCD ambaye yupo kwa sasa tunaona hawezi.
 
Last edited by a moderator:
Poleni sana, ila Bunda vijana wengi wana wanashinda vijiweni. hawajitumi kutafuta kazi zaidi kamali, bange, gongo, umalaya, wizi, nk.
 
Majambazi wamevamia duka la Muuza simu usiku wa saa tisa na kupora Simu zote na pesa katika eneo la genge la jioni.
Kabla ya tukio hilo wakawa wamepiga risasi Nyasura mbugani mwendo wa saa nne usiku.
Baada ya tukio walipiga risasi zaidi ya 10 na Polisi hawakuweza kujitokeza kujibu mashambuzi hayo.
Pamoja na hayo yote hapa Bunda matukio ya Bunduki yamezidi kila Leo na wananchi hawana amani.

Mkuu wenu wa jesh la polisi anaitwa nani?
 
Back
Top Bottom