Majambazi wapora gari kwa waziri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majambazi wapora gari kwa waziri

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Jun 16, 2010.

  1. Bujibuji

    Bujibuji JF-Expert Member

    #1
    Jun 16, 2010
    Joined: Feb 4, 2009
    Messages: 29,609
    Likes Received: 10,106
    Trophy Points: 280
    WATU wanaoaminika kuwa majambazi wamevamia nyumbani kwa Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Omary Yusuf Mzee na kupora gari la mwanae lenye thamani ya Sh12 milioni.

    Mbali na kupora gari hilo, watu hao pia walimpiga na kumjeruhi na mtoto huyo wa kiume anayeishi na baba yake kwenye nyumba za viongozi wa serikali zilizoko Kijitonyama jijini Dar es Salaam.


    Kamanda wa polisi mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa watu hao walifanya uhalifu huo juzi jioni wakati kijana huyo akiwa anatoka kazini.


    Alisema kijana huyo alivamiwa akiwa nje ya geti la nyumbani kwao na kuporwa gari hilo alilokuwa anaendesha.


    Kwa mujibu wa kamanda huyo wa polisi kutokana na hali hiyo polisi inaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha tukio hilo na kuwatafuta waliohusika.


    "Polisi bado tunaendelea na uchunguzi wa tukio hilo, tukikamilisha tutatoa taarifa pamoja na kueleza hatua nyingine za kisheria tulizochukua," alisema.

    Awali Waziri Mzee aliliambia gazeti hili kuwa kijana wake alivamiwa akiwa nje ya mlango mkubwa wa kuingia nyumbani kwake alipokuwa anarudi kutoka kazini.


    “Ni kweli kijana wangu amevamiwa na majambazi jana (juzi) wakati anatoka kazini. Tukio hilo lilitokea nje ya geti la nyumbani kwangu," alisema Mzee na kuongeza:

    "Wamemwumiza na kumsababishia majeraha mwilini."


    Tukio hilo pia lilivuta hisia za bunge mjini Dodoma ambako naibu spika, Anne Makinda aliwatangazia wabunge kuwa Mzee amevamiwa na majambani nyumbani kwake.

    "Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi Omary Yusuf Mzee amepata matatizo nyumbani kwake baada ya kijana wake wa kiume kuporwa gari na kujeruhiwa nyumbani kwake," alisema.


    Alisema kutokana na tatizo hilo naibu waziri huyo ameomba ruhusa na kuruhusiwa kwenda Dar es Salaam kumwangalia mtoto wake huyo.


    Makinda alisema alilazimika kutoa taarifa ya kukosekana kwa naibu waziri huyo baada ya Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo kubaki pekee yake bungeni bila hata naibu mmoja.


    Manaibu waziri katika wizara hiyo nyeti kwa uchumi wa taifa ni Jeremiah Sumari na Omary Yusuf Mzee.


    Sumary bado yuko nchini India ambako alienda miezi kadhaa iliyopita kwa ajili ya matibabu
     
  2. Askofu

    Askofu JF-Expert Member

    #2
    Jun 16, 2010
    Joined: Feb 14, 2009
    Messages: 1,668
    Likes Received: 2
    Trophy Points: 133
    Eeeh, makubwa...

    Hivi hawa mawaziri si wanalindwa na FFU?
     
  3. N-handsome

    N-handsome JF-Expert Member

    #3
    Jun 16, 2010
    Joined: Jan 23, 2008
    Messages: 2,297
    Likes Received: 110
    Trophy Points: 160
    :embarrassed:
     
  4. PakaJimmy

    PakaJimmy JF-Expert Member

    #4
    Jun 16, 2010
    Joined: Apr 29, 2009
    Messages: 16,233
    Likes Received: 130
    Trophy Points: 160
    Gari hiyo ina thamani ya tshs 12M....Wabunge wanashangaa nini wakati ndo utaratibu wa maisha kwa Watanzania wa kawaida huo?...AU KWA VILE NI MTOTO WA WAZIRI?....Halafu ana bahati sana, mbona raia wengine wanaporwa na kutandikwa risasi za mfululizo, hakuna anaestuka?
     
Loading...